Hoja ya mleta maada juu imeegemea zaidi juu ya soko la hawa graduate wa procurement baada ya kuhitimu, amesema wazi, soko lao kuu la ajira liko hasa serikalini, kwa maana wizarani, katika idara na taasisi za serikari na hata katika halmashauri.
Kwa mtiririko wa wachangiaji katika maada hii, wengi mmeungana na mtoa maada maana mnatetea hoja zenu kwa kuzingatia majukumu ya wagavi katika uwanja huo huo wa ajira serikalini. Tujiulize kama ambavyo maada inataka, serikali inaweza wabeba wahitimu wote wa ugavi na kuwaajiri katika nafasi hizo?!