Kwa utendaji kazi uliotukuka wa Rais Samia naanza kuziona dalili za upinzani kutafuta visingizio vya kumkimbia na kumkwepa katika Uchaguzi Mkuu ujao

Kwa utendaji kazi uliotukuka wa Rais Samia naanza kuziona dalili za upinzani kutafuta visingizio vya kumkimbia na kumkwepa katika Uchaguzi Mkuu ujao

Upinzani Hasa CDM Kwa sasa una nguvu kubwa kuliko wakati wowote tangu UHURU.

Sababu kuu ni udhaifu wa Chama tawala na Serikali ktk kuwahudumia wananchi Walio wengi wa kipato Cha chini.
Mandonga
 
Magufuli japokuwa alifanya mambo makubwa ikiwemo kuwadhibiti wapinzani lakini kwenye uchaguzi aliomba ...
Mh Rais wetu hatakuwa na upinzani wowote uchaguzi ujao, kwanza Ni kwa kuwa amefanya kazi kubwa ambazo kwa Mara ya kwanza tunaona mh Rais akigusa kila eneo pasipo kuachwa nyuma kwa eneo lolote au kwa kundi lolote

Hii ndio sababu ya kuona akipata uungwaji mkono toka makundi mbalimbali, ukienda kwa wakulima utakuta kawagusa, ukienda kwa vijana utaona kaweka baraka kwa vijana kwa kutengenezwa fursa za ajira lakini pia na kutoa ajira za moja kwa moja, ukienda kwenye biashara nako unakuta mh Rais kafanya kazi nzuri ya kuweka mazingira mazuri ya kibiashara na kiuwekezaji,

Mh Rais wetu Hana mpinzani, Nenda katika Elimu Afya maji umeme utakuta kazi kubwa Sana aliyoifanya Hilo kwote
 
Ndugu zangu hivyo ndivyo hali halisi ilivyo, kwasasa upinzani umefika hatua hauelewi ushike lipi na uache lipi,...
Mara nyingi tunajua lengo la watu wenye ID zenye real name kama wewe ni kukumbukwa na serikali kwa kuimba mapambio mitandaoni mkiamini kwamba mnauza majina lakini mara nyingi utafiti unaonyesha wengi wenu mnaishi kutoswa tu na kulalamika,sikudanganyi walikuwepo wengi sana humu kama wewe na walikuwa wanaweka hadi namba za simu lakini huwezi amini bado wanasugua benchi hadi leo system zina wenyewe hizi.

Kulikuwa na watu wake jiwe humu kibao lakini jiwe alipofariki watu walewale waliokuwa wanaimba mapambio wamegeuka wapingaji wakubwa wa huyu aliye sasa nadhani hata wewe roho inakusuta kwa ID yako yenye jina Fake unaponda upuuzi wa serikali yako hii hii unayoitetea kwa Id ya real name.

Ndugu zangu tuwatengenezee mazingira mazuri watoto wetu aisee wasije wakatia aibu kama hivi kuwasujudia mamlaka
 
Tozo Ni kwa Faida yetu wenyewe kuijenga nchi yetu, hiyo ndio njia waliyopita wenzetu

Hamna mtanzania anayejitambua atashiriki huo ushenzi uitwao uchaguzi. Kenya hapo tumeona uchaguzi wa ukweli. Huo uhuni shirikini na vyombo vya dola na watu wasiojitambua. Na ukitaka kujua kuwa watanzania wanajitambua na huwa hawaichagui CCM, subiri wapinzani wakisusia huo ushenzi uitwao uchaguzi kama wapiga kura watafika hata 5m.
 
Ndugu zangu hivyo ndivyo hali halisi ilivyo, kwasasa upinzani umefika hatua hauelewi ushike lipi na uache lipi, uongee nini na usimame na lipi, ubebe lipi na uache lipi, utembee na lipi na usimame na lipi.

Imefika hatua hata kuaminiana wao kwa wao wameacha, maana kila mtu anahisi mwenzie anadalili za kusaliti chama na kwenda kumuunga mkono Mh. Rais wetu mpendwa, hapa unaweza kurejea habari za Mch. Peter Msigwa namna alivyo tukanwa na vitoto vidogo kiumri kisa tu kusimamia mtizamo wake katika kuiunga mkono serikali juu ya suala la Loliondo.

Ndugu zangu kwa sasa hata wenyewe hawaoni wakuweza kushindana na Mh. Rais Samia maana kila waliyemuona awali kuwa ndio kamanda wa kuongoza mapambano, wanakuta amerudi mstari wa nyuma akiunga juhudi za Mh. Rais na hata kama ni kukosoa anakosoa kwa kushauri baadhi ya maeneo kwa heshima na staha, jambo linalozidi kuwa changanya na kuwalaza na viatu vijana wa upinzani.

Hii yote ni kwa kuwa Mh. Rais kafanikiwa kugusa kila eneo kiutendaji, watanzania wana matumaini makubwa sana na Mh. Rais kwa kuwa wanaona juhudi zake katika kujenga nchi yetu, wanaona namna kila mtu, kila kundi na kila eneo linavyoguswa kiutendaji. Hakuna anayeachwa nyuma wala kutengwa au kubaguliwa, wote wanapata huduma sawa.

Kila mtu anapata huduma sawa,kila mtu anasikilizwa, kila mtu anathaminiwa,kila mtu anaona anayo nafasi ya kuchangia ujenzi wa Taifa hili na kila mtu anaona anaweza kutimiza Ndoto na malengo yake katika nchi hii kwa kuwa fursa zipo wazi kwa kila mtu mwenye kuzitaka.

Sasa hapa ndioo mtihani mkubwa walionao upinzani kwa sasa katika kuweza kusimamisha mgombea kiti cha Urais maana hawaelewi watamsimamisha nani? Kwa sera na ajenda zipi, hawaelewi watawashawishi kipi watanzania, maana Mh. Rais amefanya kazi zilizogusa maisha ya watanzania hasa wanyonge wasio na sauti.

Wameona namna Mh. Rais alivyo shapu kuchukua hatua katika kumsaidia mwananchi pale panapojitokeza tatizo la kidhalula kama alivyo fanya kutoa Ruzuku katika kilimo na nishati ya mafuta, kiukweli kasi hii ya Mh. Rais imewaweka pabaya sana kisiasa.

Ushauri wangu kwao ,kwa kuwa wameonyesha kukubali utendaji kazi wa mh Rais Basi hawana budi Kuendelea kumuunga mkono Mh. Rais wetu, waendelee kutoa ushauri watakapoona panafaa kwa lugha ya heshima na staha.

Maana mama ni msikivu na mnyenyekevu anayemjali na kumsikiliza kila mtu, kwa sasa mama amekaa katika mioyo ya watanzania. Watanzania walitaka maendeleo na mtumishi mnyenyekevu atakayewasikiliza, sasa amepatikana Mh. Rais Samia anatekeleza kwa vitendo ndoto za watanzania.

Kazi iendeleee.
Pigo moja la tozo za Madelu linatosha kumuangusha achilia mbali maisha yanavyo wapiga wananchi mitaani
 
Pigo moja la tozo za Madelu linatosha kumuangusha achilia mbali maisha yanavyo wapiga wananchi mitaani
Fuatilia utafiti wa Twaweza unasema Nini juu ya Tozo na maoni ya wananchi,

kwa ufupi Ni kuwa wananchi wengi wanaunga mkono juhudi hizo za serikali katika kuijenga nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe, wananchi hawataki tuwabebeshi mzigo wa madeni vizazi vijavyo, wananchi wanataka wajibu na mzigo wetu tuubebe Wenyewe katika mabega yetu pasipo kuwaangushia wengine
 
Hamna mtanzania anayejitambua atashiriki huo ushenzi uitwao uchaguzi. Kenya hapo tumeona uchaguzi wa ukweli. Huo uhuni shirikini na vyombo vya dola na watu wasiojitambua. Na ukitaka kujua kuwa watanzania wanajitambua na huwa hawaichagui CCM, subiri wapinzani wakisusia huo ushenzi uitwao uchaguzi kama wapiga kura watafika hata 5m.
Ndio maana nikasema utendaji kazi huu wa mh Rais wetu umesha wachanganya Sana na Kuna uwezekano mkaogopa kuvuna aibu iliyo wazi kabisa baada ya kuonekana kuwa kwa Sasa mmekosa Sera na ajenda za kueleweka kwa wananchi
 
Chawa katika ubora wake sijui analipwa sh ngapi
Silipwi chochote kile zaidi ya kuvutiwa na kuridhishwa na utendaji kazi wa mh Rais wetu , utendaji ambao umewafanya watanzania kumuunga mkono mh Rais wetu na kuwa naye bega kwa bega , Baada ya kutambua kuwa wapinzani Ni wababaishaji tu wasio na Sera Wala ajenda za kugusa maisha yao zaidi ya maneno ya uongo uongo
 
Wanajitoa UFAHAMU, wakitaka kujua nguvu ya upinzani, wapuuze HOJA ya TUME HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya.

2024 uchaguzi wa Serikali za mitaa Si mbali.
Tume haichagui Wala kupiga kura Bali kazi ya tume Ni kumtamgaza sauti na maamuzi ya wananchi, Sasa nyie Nani atawapigia kura? Kwa Sera na ajenda zipi? Kwa matusi hayo? Nani kawaambia wananchi wanataka kusikia matusi yenu?
 
Mara nyingi tunajua lengo la watu wenye ID zenye real name kama wewe ni kukumbukwa na serikali kwa kuimba mapambio mitandaoni mkiamini kwamba mnauza majina lakini mara nyingi utafiti unaonyesha wengi wenu mnaishi kutoswa tu na kulalamika,sikudanganyi walikuwepo wengi sana humu kama wewe na walikuwa wanaweka hadi namba za simu lakini huwezi amini bado wanasugua benchi hadi leo system zina wenyewe hizi.

Kulikuwa na watu wake jiwe humu kibao lakini jiwe alipofariki watu walewale waliokuwa wanaimba mapambio wamegeuka wapingaji wakubwa wa huyu aliye sasa nadhani hata wewe roho inakusuta kwa ID yako yenye jina Fake unaponda upuuzi wa serikali yako hii hii unayoitetea kwa Id ya real name.

Ndugu zangu tuwatengenezee mazingira mazuri watoto wetu aisee wasije wakatia aibu kama hivi kuwasujudia mamlaka
Naitetea serikali yangu kwa kutoa ukweli wa mambo unaoonekana machoni pa kila mtu asiyekipofu, halafu lazima ujuwe na kutambua siku zote kuwa uongozi huwa unatoka kwa Mwenyezi Mungu pekee, yeye ndio huwa anajuwa amnyanyue Nani na kumshusha Nani na kwa makusudi yapi,

Yeye humnyanyua mtu anayejuwa atawatumikia watu wake kwa upendo na unyenyekevu mkubwa Kama ilivyo kwa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani anayewatumikia watanzania kwa upendo na unyenyekevu mkubwa Sana unaogusa maisha ya watanzania wanyonge
 
Hawezi kukujibu kwa sababu keshakabizi Ubongo umewekwa Stoo pale Lumumba.
Kwanini nisimjibu, Kuna swali gani gumu hapo ndugu yangu Mtanzania mwenzangu unayeendelee kupata furaha na fursa ya kuinuka kiuchumi kutokana na kazi nzuri ya mh Rais wetu katika kuhakikisha maisha ya watanzania yanakuwa Bora Zaid ya jana
 
Back
Top Bottom