Kwa wale ambao hamna maelewano mazuri na wazazi wenu

Kuna mda watoto hatuna time na wazazi sio kwa sababu walitutesa ila kuna vitu walivipuuza na ss tukajikuta hatuoni umuhimu wao.
Mm sikulelewa na baba mzazi wala mama mzazi(alifariki nikiwa mdogo) nilikulia kwa mazao mkubwa (huyu ndio kama mama vile) ila ku a vitu watoto wake (sio wote) walikuwa wananifanyia kama kaubaguzi flan hv na vipigo visivyo na sababu za msingi na sikuwahi muona akivikemea had ikafikia sehem nikajikuta na mm najitambua kuwa ayo yote ni kwa sababu pale sio nyumbani toka hapo mm sinaga time nao wao wala yeye nikiwa mbali naweza maliza ata miezi 3 sijampigia na alijisikia vibaya.
Kwa mzee napo nimeanza kuishi nae nilipo maliza form 4 najikuta huwa hakuna ile bond ya baba na mtoto kabsa (kwangu mm ) Yan kuna mda nikiwa mbali najilazmisha tu japo kumtumia sms ata mara moja kwa mwezi asijejiona yupo pekee ake ila sijawahi kukaa et nikammis
 
Aisee! nawaonea huruma sana, Poleni na tafuteni kupona.

Je inawezekana ukampenda mtu ukubwani mume/mke ikiwa haukupata upendo wa familia yako? Familia yako ilikuwa ina nafasi ya kukupenda ila haikufanya hivyo kwa makusudi au kwa kutokujua.

Binadamu wajifunze kutafakari na kujiassess kama kweli wanaweza kuwa wazazi. Kazi kuhamasishana kuzaa wakati uwezo wa kuwa wazazi bora hamna!
 
Mi naamini bond hutengezwa utotoni lkn ukubwani hakuna, mimi najitahidi kwenye dini na kumuomba mungu anifanyie wepes labda naweza kujaribu kumfikiria lkn moyo unakataa kabisa, hata nikiandika msg ya kumjulia hali wakati mwingin naona niifute nisitume tena, kwa sasa wanae wengine wanampiga matukio ndo anajaribu kujirudi lkn kiukwel sina nae mazoea kabisa
 
Hakika wengi hawajitafakari ktk hili, nashukuru kwa upande wangu nimeichukulia positive kiasi kwamba nalea binti zangu kwa ukaribu mkubwa , yani sitaki wapite nlopitia mimi kabisa
 
Hakika wengi hawajitafakari ktk hili, nashukuru kwa upande wangu nimeichukulia positive kiasi kwamba nalea binti zangu kwa ukaribu mkubwa , yani sitaki wapite nlopitia mimi kabisa
Ulipitia yap zuu sijaona sehemu umeandika
 
Halafu sijui kwann watu wa namna hii wanakuwa walalamishi baadae as if hawajui walichofanya. Hapo anataka umbwatukie tu ili aje kukulaumu na kulazimisha kupeana laana na mikosi wakati sio lazima.
 
Biblia hiyo hiyo imewaasa wazazi wasiwachokoze watoto wao

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Unajua wazazi hawajui kuwa pia matendo yao kwa watoto ndio hupelekea baraka za kuishi muda mrefu, kuwa na hekima na afya.

Hebu jiulize kwann wazazi wetu wa kiume yaani Baba pamoja na kujitoa sana kwaajiri ya familia ila muda wao wa kuishi ni mdogo na hata wakiwa wazee watoto huwatenga.

Ni matendo yao na ukaribu wao na watoto ndio chanzo. Mtoto akiwa na furaha na amani na mzazi kila siku moyo huwa unamuenda mbio kama hajaongea na mzazi na pia humuombea mzazi huruma na uzima kwa MUNGU ili aishi muda mrefu na kuwa na afya.

Mtoto au watoto wanapokuwa na connection nzuri na mzazi na kutokuwa na fikra au mawazo ya kudhurumiwa au kuonewa na wazazi hii hali hujenga bondi nzito sana na yenye nguvu na kusaidia mzazi kuwa na baraka za kuishi muda mrefu.

Ndio maana mama zetu wameishi miaka mingi sababu ndani ya mioyo yetu tumewapa hadhi ya utakatifu kutoka na kujitoa kwao kwetu.

But hawa wamama wa miaka hii sijui MUNGU ndie atajua. Maana matendo yao yanaonesha wazi yatafuta baraka zote za uzeeni.
 
Haya Mambo Kama mtu hayajawahi
Kumkuta anaweza akaona watu wanaolalamika basi wanachekesha au wamechanganyikiwa,aisee hakuna kitu inaumiza au kumfanya mtu aone maisha machungu Kama kukosa upendo autakaye mtoto kutoka kwa mzazi wake
naunga mkono hoja 💯
 
Aisee nimejifunza kuwa maisha yetu ni yale yale.

Binafsi sina shida na wazazi, lakini hawa Ndugu zao sasa, hasa Baba wadogo na Wazee wengine wa Ukoo.

Huwa siwaelewi kwa jinsi walivyokuwa wanambeza na kumtweza Mzee wangu kipindi hali yake kiuchumi imeyumba, mpaka anafariki. Ila leo hii wanathubutu kulalamika kuwa Watoto wa Mzee tunadharau na hatuwapi Ushirikiano, ilhali wao ndiyo walianza kutudharau sisi, wakajiweka kando na sisi.. Sasa leo hii naanzaje kujiingiza kwenye maisha yao, wakati hawajawahi kuwepo kwenye maisha yangu?
 
Unakaa nae mbali. Mtu mbea na mfitishi au mchonganishi mnyime fursa ya kupata taarifa zako atakosa cha kusema juu yako ghafla utaona anakonda kwa mawazo.
Anawagombanisha sana walio karibu nae kaka zake ,kaka mwenye pesa ndio anakuwa nae karibu anampa maneno
Mi nipo nae mbali aisee
 
Sina shida na mzazi wala ndugu.. ila nina changamoto ya kuwa mvivu kuwapigia simu.

Kuna mama wakubwa wakianza kunisemea kwa mdogo wao ambaye ndio mama sasa, mama anakuja ananisema. Nikijitahidi ni hiyo week niliyosemwa, kisha narudi kuwa vile vile.

Sijui hata natokaje kwenye hicho kisanga.
 
Nakuelewa.
 
Kumbe tupo wengi!!!!!

Ngoja niishie hapa
 
Hata Kajala Masanja,Baba levo na Mwijaku nao ni wazazi
 
Dejane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…