Kwa wale ambao hamna maelewano mazuri na wazazi wenu

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚wine leo siwezi kunywa. Labda kesho mrembo wangu
 
uhusiano ni kama daraja kama hukunipenda na kuweka uhusiano mzuri na mimi utotoni usidhani ukubwani nita kupa time wala nafasi Never
Hapa ndo kwenye tatizo mkuu, bond mbovu kati yangu na mazaa inatutesa sasa hivi.
Nahisi anaumia lakini na mimi nakosa la kufanya coz sijaishi nae mda mrefu, sijamzoea sana.
 
What i choose after seeing nasticism. Is to walk away
 
Dahh! Pole sana ndugu yangu... bin-Adam sisi... mhhhh! Kesho kwa mungu kutakuwa na mengi sana hadharani πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”
 
Mzee hakutaka majukumu... alitaka zake kula mtungi na kugonga tu! πŸ˜…πŸ‘πŸΎ
 
Ata kushindwa kuchukia unapochukizwa au kuendelea kujikomba kwa watu wasio kuthamin ni tatizo la akili pia
 
Maisha ni mitihani. Kuna wazazi ni mitihani na kuikabili unahitaji uvumilivu wa Hali ya juu. kama hakuna mahusiano mazuri Kati yako na mzazi , wewe maintain your distance. Akiwa na shida msaidie pale unaweza. Ila kamwe usijihusishe na maisha yake kwa ukaribu. Akipiga simu anasema ana shida, mrushie salio. Mengine mwaachie mwenyewe.
 
Aiseee, pole sana inaumiza mno.!
 
Haya mambo ya familia sometimes acha vitu viflow kama vilivyo yani hata kama unaona sio sawa hasa MAMBO YA HELA yani utagombana na wazazi mpaka ndugu. Kuhusu upendo kwa watoto hilo lipo kila familia hamuwezi kupendwa sawa pia kuna mambo yanafanyika unaona kabisa kuna upendeleo ila kama unapambana unapata riziki yako haviwezi kukupa tabu kabisaa unaishi maisha yako.. Mengine kubali kukosolewa kama kijana kweli unaweza jisahau hata kuwapigia wazazi simu hasa mama zetu wanapenda sana kupigiwa simu hata kama mara moja kwa week na sisi watoto tokana na majukumu tunajisahau kabisa so akilalamika mwambie tu ntakupigia mama sio kwamba nafanya makusudi. Kama mzazi alikuwa na uwezo wa kukusaidia akakutelekeza na kukukaushia aisee KARMA imtafune japo kwa muda flani mpaka ajute na umwambie kabisa ukweli kama atakasirika asuse shauri yake kama anajielewa ataomba radhi MSAMEHE msonge mbele.

USIKUBALI PAST YAKO IKUTESE NA KUKUFUNGA KUISHI MAISHA YA KUUMIZA WENGINE KISA WEW ULITENDEWA.
 
Mkuu wakati mwingine siyo akili zao,,,tusiwalaumu sana,,,aliyelishwa Limbwata hajijui kama karogwa
 
Mimi mpaka kufikia umri huu sijawahi kushuhudia wala kuona upendo wa dhati kutoka kwa mtu yeyote. Kwanza sijalelewa kabisa na mzazi yeyote yule. Nilibahatika kuishi na mlezi kidogo tu nae nikaona ananiongezea mapicha picha tu katika maisha yangu nikatemana nae.

Ninae mzazi mmoja, wenyewe mnamuita "Mama", ila kuhusu huyu Mama naomba niishie hapa hapa.
 
Mkuu hongera kwa bandiko bora sana,ila tambua kwamba kuna wazazi ni changamoto sana yani. Sitaki kusema sana ila tambua hivyo,mpaka likukute ndipo utajua ni nini namaanisha.
Natambua sana mkuu jinsi wazazi wetu walivyo changamoto ndio maana nimeandika mada hii
Inauma mno
Hivi nama akiwa changamoto si ndio inauma zazid??
How did you cope with???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…