Kwa wale ambao hamna maelewano mazuri na wazazi wenu

Pole sana broo,huu uzi unasikitisha sana.
 
Mzee mbona kama unaandika kinyume chake,yaani baraka zitoke kwa watoto ziende kwa wazazi??hata mzazi akosee vipi mtoto anawajibika kwa mzazi wake kulinda hadhi yauungu aliyopewa na mwenyezi Mungu.ndio maana imeandikwa waheshimu baba namama yako siku zako zipate kuongezeka,nasio mzazi aheshimu watoto wake.sipingi kua kuna wazazi vimeo sana,ila mambo haya nadhani yanamiongozo flani ya kuepusha mkanganyiko ktk jamiii ndio maana hata kama mzazi hakumtunza vyema mwanae wakti wautototoni mzazi huyo anaweza asipate laana,lkn mtoto kutokumtunza mzazi wake ktk uzee wake laana inamuhusu.
 
30 min mnaongea nini, yani mm nikiongea nae mda ukiwa mrefu ni sek 46 na mara nying ni sekunde 23, ujambo sijambo shikamoo, nawajulia hali shukran tumemaliza[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Daahhh???!!sec23???!!jitahidi uweke mazingira mazuri nababayako kwa ajili yafaida yako ww mwenyewe na nafsi yako.
 
Daahhh???!!sec23???!!jitahidi uweke mazingira mazuri nababayako kwa ajili yafaida yako ww mwenyewe na nafsi yako.
Wazee wachache sana wanaongea muda mrefu kwenye simu na hapo napo ukute ni baba na mtoto wa kike au baba na mtoto wa kiume ambae ana HELA wanashauriana juu ya mambo ya biashara au vitu flani vya maisha.. Ila wengi ni salamu na blaa blaa chache dakika 1 huwa haiishi may b kama kuna mambo ya kifamilia hayajakaa sawa pia mnayaongelea.
 
I hope mna mahusiano mazuri na wadogo zako mpaka saahii,maana ulivoandika looks like they're not a problem. Ni mzee wenu tuu ndo kukosa busara ya kuwalea kwa usawa.
I hope you have them.pole sana.
 
Pole Sana mkuu, naomba niku pm
 
Natambua sana mkuu jinsi wazazi wetu walivyo changamoto ndio maana nimeandika mada hii
Inauma mno

Hivi nama akiwa changamoto si ndio inauma zazid??
How did you cope with???
Siko karibu nae so sijui mengi kuhusu yeye. Mkuu,kuna baadhi ya hali unajikuta tu automatically uko hivo.
Hii hali imepelekea mpaka huwa natafuta kitu cha msingi sana katika maisha yangu ila sikioni,hapa namaanisha kitu ambacho hata ukikipoteza wenyewe wanadai utaumia kihisia.
Kwa kifupi nimeharibika sana psychologically,na nishakomaa katika hali hiyo ya uharibifu.
 
Hapo shida inawezekana ni utamaduni ambao wazazi wako wameutengeneza wa kutowaweka karibu na ndugu zenu ikiwamo kutowashirikisha katika shughuli mbali mbali za kifamilia. Hii itakuja kuwaathiri ninyi watoto wao hamtakuwa karibu hata kidogo.

Unajua mnaweza ona wachagga kama wachawi vile wanakwenda kila mwezi wa kumi na mbili kwa gharama kubwa ila lengo ni kuweka ukaribu wa watoto watambuane na ndugu zao, wahimize upendo kati yao, kujaliana na kuheshimiana na kusaidia popote wanapokuwa mbali.

Pia inasaidia hata kutazamana tabia sio mtu anakuwa na matukio ya kipuuzi puuzi kama wizi, magendo sijui uhalifu gani kila wiki yupo polisi, au dada zetu kuzaa hovyo na wanaume wasioeleweka mwishowe wanashindwa kumudu gharama za maisha wanaanza kusumbua ndugu kwann sasa wasikukimbie na kukuona kero.

Ukaribu ni muhimu sana ila unaharibiwa na wazazi kutokuwa na utamaduni wa kusema fulani haya jiandae weekend hii tunakwenda kwa baba mkubwa au kwa mama mdogo kutembea. Au tunakwenda kuwatembelea akina binamu.

Watoto wakikuzwa na hizi tabia utaona wanakuwa pamoja na wanakuwa karibu sana.
 
Kumbe tupo wengi!!!!!

Ngoja niishie hapa
Funguka tupe hata kidogo majanga yako, uzuri unaposhare story yako unawafanya na wengine kupata faraja na kupunguza depression maana watajua kumbe hawapo pekee yao katika kupitia misukosuko ya kifamilia na mwisho wa siku tunapeana hata mbinu za kusurvive hizi hali.

Imagine kuna mtu anajiuliza mimi hii familia yangu siwezi kuitenga sasa naishi nayo vipi ila anakuja hapa anaona story ya namna watu kadhaa ambao familia zao zimewaletea mazengwe na mbinu wametumia kukabiriana nazo na kuwaweka kando ili wasiwaletee upuuzi wao. Na cha zaidi utapata namna za kuishi kwa kujitegemea bila muingiliana na wanafamilia wasiojitambua bila kujihisi unahatia yoyote tofauti na jamii wanavyosisitiza kuwa damu ni nzito kuliko maji.

Kimsingi kushare kunakusaidia wewe na wale wanaokuzunguka kuwa salama. Lakini muhimu zaidi kunakuondolea hatari ya kupatwa na msongo wa mawazo yaani kuwa depressed bila sababu za msingi.

Toa shaka sababu hakuna mtu ambaye anaweza kukujua au kukufuatilia personal life yako nje ya hapa kwasababu umetoa story yako. So toa shaka kuwa free. Kuwa kama mtu anayekojoa kwenye bahari wakati yupo ndani ya maji, au mtu ambaye amebanwa na shuzi halafu kasimama katikati ya uwanja wa mpira na hakuna mtu yoyote uwanja mzima namna atakuwa huru kuliachia hilo shuzi.

Au kama mtu anayekojoa kichakani huko porini raha yake na uhuru wake katika kujiachia. Ni raha sana. Wewe toa shaka.
 
Tanzania ina watu wengi ambao kila mtu anakua kwenye mfumo tofauti na mwingine, wewe kama umekua kwenye familia bora yenye upendo basi ni vyema sana ila sio huu utoto unao andika hapa ni aibu mno. Grow up man
Kuna watu kwasababu yeye anakula anashiba, wazazi wake wapo hai wote, na wanawasaliana vizuri na ana ushirikiano mzuri na ndugu zake wa familia yake aliyokulia na wanasaidiana vema basi anaamini dunia yote watu wote wanapitia the same life style yaani hakuna changamoto kwa wengine na kwamba hawa wanaoleta story hapa na confessions zao basi wengi wao haya maisha wamejitakia na pengine wanachangamoto zao binafsi ila hakunaga familia inaweza kuwa tatizo kwa mojawapo wa mtoto.


Kwa kifupi kuna watu hawana exposure. Wanaishi in an eggshell so hawajui nini kipo nje ya maisha yao yenye comfort.

So huyu ni wa kumsamehe na kumuombea aje kujionea kwa watu wakaribu ili ajifunze na sio kuja hapa kukanusha experience za wahanga wa hizi changamoto ambao wamezipitia. TOXIC AND NARCISSISTIC FAMILIES ARE REAL.
 
Hakika kabisa. Lowama siku zote zinapelekwa Kwa watoto. Piga picha baba aliyetelekeza Mtoto ambaye hajitambui na hajui lolote Na hawezi jambo lolote.. anahitaji msaada. Mtoto anakua Hadi anafika mkubwa baba Hana habari naye. Siku akifanikiwa Baba anajitokeza anahitaji asaidiwe. Hili hapana aisee

Hata kwenye biblia tunaona wazazi karibia wote tunawaona wanatunza na kujali watoto wao. Manabii na mitume. Hata wafalme walikua wanaandaa watoto wao.

Sasa hii unayoitetea hapa Haina maana. Kuna wazazi hawana sofa za kuitwa baba na mama kutokana na matendo Yao Kwa watoto.



Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Mali imeleta shida, imagine bila mali kungekuwa na matokeo mabaya kimahusiano kama uliyonayo sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…