Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Kuna mijitu kweli ina roho mbaya waweza kuta kuna mtu alikuwa na wivu tu na maendeleo yako akataka akuondoe duniani
 
Kuna mume wa shangazi yangu alikuwaga ni "mtu asiyejulikana" alikuwa akifanya ambush zake huko anakimbilia nyumbani (tulikuwa tunaishi mikoa tofauti) na mi wakati huo bado bwana mdogo tu......nikawa namsindikiza kwa babu saa 7 za ucku tunaenda makaburini tukiwa uchi hata cjui tulikuwa tunaenda kufukia nini, na baada ya siku chache tu msala wake unasahaulika kabisa na anarudi huko anakoishi akiwa mtu huru kabisa, lakini mwaka 2006 alikufa kwa kupigwa mshale wa kifua halafu wananchi wenye hasira kali wakaja kummalizia kwa kipigo kizito......sasa cjui hapo ilikuwaje yule babu alishindwa kumsaidia
 
Mimi naendaga sana, hapa nasubili ombi la

Mshana Jr likubaliwe lile la jukwaa la wachawi
 
Waganga wengi ni waongo balaa
Kuna dada mmoja tulikuwa tunajua anaumwa nini lakini tuliamua kwenda kwa mganga ili tumsikie anasema nini
Mganga akaanza kumwambia umetupiwa jini na mchepuko wa mmeo na ndio linalokutesa
Daah tulicheka balaa baada ya kusikia uwongo wa mganga
 
Waganga wote ni wachawi (vigagula)

Huwezi kuwa mganga bila kuwa mchawi

Hata daktari anasomea magonjwa kabla ya kuanza kutibu, so it s obvious mganga kuwa mchawi ila ni mchawi protective. [emoji2]
 
I like it
 
ilikuwa ni darasa la sita mwanafunzi mwenzetu aliiba box la kalamu lote tena la mwanafunzi aliyekua mtoto wa mwalimu ikapita msako mkali hazikupatikana mwalimu akasema kesho asubh wote tuandike jina la mtu unaemhisi

Basi jioni tukajipanga wanaume kadhaa kama kumi na saba tukashauriana tuende kwa bibi mmoja ni mtaalamu huyu jamaa aliyeiba tutampata fasta

kikundi kikatimia tukatoroka moja kwa moja safari ikaanza tufafika kwa mtaalam na sare zetu za shule tukaingia wote kwa pamoja akaanza kutoa misauti yake akatueleza muna shida tofauti au ni moja mmoja akajibu ni moja

akasema haya mmoja aelezee jamaa akatiririka vya kutosha akasema andikeni majina yenu na ya baba yenu na shule mnayotoka kisha munipe ukishanipa unageuka nakuondoka hadi nyumbani kwako huyo mwizi asubuhi atapiga kelele nakuzirudisha mwenyewe sitawatoza hela nawasaidia tu kama wajukuu zangu tukafanya kama alivyosema

kumbe pale jirani kuna mwalimu wetu yupo karibu na yule bibi jioni akamfuata akampa na yale majina asubuh tupo paredi tukaanza kuitwa jina mmoja baada ya mwingine tukijiangalia ni wale wote tuliokuwa kwenye tukio ohoo kilochofuata siwezi ata elezea ngoja niishie tu hapa

na hapo ndipo nilopotokea kuwachukia hadi leoo
 
Mh mko wengi,haya endeleeni kutupa uzoefu wenu...
 



[emoji38][emoji38][emoji38]uwiii nimecheka
 
Rekebisha maelezo yako sasa kama hujawahi kwanini useme tulio wahi! Sema mliowahi kwenda kwa waganga njooni hapa. Inavyoonesha wewe ni mmoja wao wa kwa hizo imani ila umeamua ujitoe bila kujijua ukakosea kuandika.
Ulishawahi kwenda kwa daktari akakuambia, tuna tatizo gani leo?

Au akakuandikia dawa alafu akakuambia, tutatumia hizi dawa kwa siku tano, tukiona hali haijatengemaa, tutajua kingine cha kufanya.

Yaani Kuna kitu kinaitwa pragmatics na semantics. Ukivijua hivi huwez kutoa maelezo kama hayo kwenye andiko kama hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…