Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

mnamktmbuka Papa wemba? alikuwa na gari limeandikwa "mokili ya nzambe"mitaa ya chekilaini ya kiloleni mbele ya town skul.
 
uyui mkuu alikuwa mr diaz au bab d.Ulikuwa fm wani gani?
 
Dah napakumbuka saana Tabora!maana ajira yangu ya kwanza nilianzia pale mwaka 2006
 
uyui mkuu alikuwa kasonta,,baadae katanga then mama shani to now
 
[emoji23][emoji23][emoji23]nzega ndio om mkuu nimesoma nyasa one ,
Hahahaaaa Nyasa Mapangon ndugu, unazkumbuka zile habar za Pango jimunye!!! Mi jiran yako pale shule ya Kitongo
 
Km ulikua unakaa Cheyo,Kitete,Gongoni, Kanyenye miaka ile ya 90 lazima Utakua ulisikia habari zao!

Kulikua na Dr pale Kitete Hospital alikua Maarufu Dr Kobello! Hujapata sikia Hilo jina?

Dr Dassy
Dr Mgumia
Dr Gobbo
 
Mdogo wao Edward Kobelo ni classmate wangu na ni deskmate pale Cheyo "A" Primary. He was a friend indeed ilikuwa kila inapofika muda wa mapumziko tunaenda kupiga chai ya maziwa na mikate kwa mama yao wa kizungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheza basket ball na hao akina Major na akina Bakari Chaima!

Kumbe Major ni marehemu?

Ntuzu,
Umecheza basket na kina Marehemu major ?
ulikuwa unatumia jina gani?
umesoma shule gani ?
umecheza uwanja gani ?
Ulishawahi kucheza kwenye umissetta ?
uzuri wa wacheza basketball kipindi hicho, sote tulikuwa tunajuana vizuri kabisa.
mimi pia ni zao la Uyui Sec.
 
Huyo Kalovya kama sikosei alikuwa anakaa nyuma ya Kazima Sekondari. Nimesoma na Dada yake mkubwa kabisa akiitwa Kulwa Kalovya.
 
Alikuwa shabiki labda
 
Mbona umepaniki... tulia kidogo basi,
kuwa mkubwa sio tatizo,maana kwa kipindi hicho tu kuwa High level inatosha kuonyesha kuwa ulikuwa mkubwa tu,Ila hapa tunakumbushana tu utamu wa Tabora hususani kwa watu tuliokuwa hatujuani .
Haujakosea, akina kalovya ndipo walipokuwa wanakaa, na ni kweli HK alikuwa ana dada zake na kaka yao mkubwa( majina nimesahau).Nilichogundua ni kuwa, ulikuwa shabiki wa Basketball lakini haukucheza.nimekuwekea picha ya miaka hiyo uangalie na kutambua wachezaji( Wengi wao wametajwa kwenye uzi huu.Ukizungumzia High level, walikuwepo akina Salehe Kimenya na wengineo.Hakuna sehemu nimeleta ubishi, rudia post yangu.naamini sote tulikuwa watoto wa "DUGU" PATEL, R.I.P, chini ya mkuu msaidizi Mwl.Mkatakona R.I.P na walimu kama , Mr Mbosori R.I.P, Mr Machibwa,Mr Mrisho (Mtaalam wa Hesabu),Mwalimu mmoja wa Biology, alikuwa na jina gumu tukampa nickname Agama Agama nk hawa wote walikuwa baadhi ya walimu wa O level.
 
😀
unajua uzi wa zamani ndio mtamu hasa.
nimeuchokonoa kwakuwa kama miezi kadhaa iliyopita, mwenzetu mmoja alifariki, tulikuwa nae kwenye basket Uyui,
aliitwa Benedictor Jacob ( R.I.P) natamani kuwajua wengine na wengine.Michezo ilitufanya tukawa marafiki bila kujali unasoma wapi, unafanyakazi wapi, unaishi wapi nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…