Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

waswezi unawakumbuka? nimesoma uyui na gongoni, uhazili nimecheza basketball, disco la muungano mess nimecheza. makokola je, vipi?

Nawakumbuka waswezi wakati niko mtoto walinitokea sehemu wakiwa wamejipaka marangi usoni Nika wa amkia shikamoo wakanijibu marahanyo ,walikuwa wana lugha ya ajabu ajabu sana, aise mboka Safi sana
 
Ntabaye namfahamu alikuwa jirani yetu. Ninachokumbuka, tulienda kwake kusali jumuiya akatutoa baru, kuwa hamuhitaji Yesu wetu. Lkn Mungu si ntabaye, mumewe Mungu alivyomchukua, akaanzaje kusali.

Duh! Wewe itakuwa tumeishi mtaa mmoja miaka hiyo! Hata mimi Ntabaye ni jirani yangu pia.Unaikumbuka Aposele guest house?
 
Nawakumbuka waswezi wakati niko mtoto walinitokea sehemu wakiwa wamejipaka marangi usoni Nika wa amkia shikamoo wakanijibu marahanyo ,walikuwa wana lugha ya ajabu ajabu sana, aise mboka Safi sana

Hiyo marahanyo nimecheka mpaka watu nilikaa nao wamenishangaa,waswezi noma aisee.watoto wa siku hizi wanakuwa kama watuwazima
 
Disco la mwanaisungu, tabora hotel.
Basketball kwenye grounds za uhazili.
Nani alisoma mwenge, kipindi cha mwalimu chiboni?

mida ya jioni tulikuwa tunatoka skani Kiloleni on foot mpaka Uhazili kufind mademu!
 
Kuna Matunda huenda yako Tabora tu, kwa mfano Ntalali, Mbuguswa, Mamtonga nk.
Nilijaribu kuyatafuta mikoa mingine lakini sikufanikiwa.

Ngubalu,Mfhulu,Nsalase,Ntondwa,Mikoma,Makuuwa,nk.bila kusahau uyoga wa porini kibao!
 
mkuu ntuzu

inalekea wewe ulikua unakaa national house, vipi kuna jamaa naitwa john shija bado yuko mboka nation ? Na famila ya kina simbakalia bado ipo tabora ?
pia kuna mchizi wangu tozi wa miaka ilee alikuwa anakaa national somebody kwilabya,sijui atakuwa dunia ya wapi leo,daah mboka raha sana,
 
Mkuu Ntuzu una kumbuka basi la Mpandawandigwa?
Urambo , tabora ,kaliua na uliyankulu @ picchu @ kahtaan

ndugu maviazi 1=makafu 1=manumbu 1 umenikumbusha miaka ya 90's kulikuwa na mabasi yanaitwa Kazuge,Mamro,Sudein,Kbs na huyu Nbs,yalikuwa na keria kubwa juu yaani mzigo wa fuso nzima ulikuwa unajaa,yalikuwa yanapiga route za tabora,ndala,mwisi,nkinga,igunga,nzega sijui yameishia wapi kwani amebaki Nbs tu!
 
Nawakumbuka waswezi wakati niko mtoto walinitokea sehemu wakiwa wamejipaka marangi usoni Nika wa amkia shikamoo wakanijibu marahanyo ,walikuwa wana lugha ya ajabu ajabu sana, aise mboka Safi sana

hahaha marahanyo, nilikuwa nawaogopa sana hawa waswez inilikuwa najua ni wachawi. kuna sehemu inaitwa kantaroli ukivuka reli ya kigoma kama unaelekea kiwanda cha maziwa unaikumbuka? nadhani walimaanisha control.
 
ndugu maviazi 1=makafu 1=manumbu 1 umenikumbusha miaka ya 90's kulikuwa na mabasi yanaitwa Kazuge,Mamro,Sudein,Kbs na huyu Nbs,yalikuwa na keria kubwa juu yaani mzigo wa fuso nzima ulikuwa unajaa,yalikuwa yanapiga route za tabora,ndala,mwisi,nkinga,igunga,nzega sijui yameishia wapi kwani amebaki Nbs tu!

pia kulikuwa na mpalaye basi servise, kirigito bus service, hii kirigito iliwahi kutumwaga siku moja tukienda urambo, kisa dereva alikuwa anakula muhindi wa kuchoma huku akiendesha gari. hahaha.
 
Duh! Wewe itakuwa tumeishi mtaa mmoja miaka hiyo! Hata mimi Ntabaye ni jirani yangu pia.Unaikumbuka Aposele guest house?

Aposele naikumbuka ingawa nimesahau ilikuwa wapi, mama mpuguso naye vipi? anakumbukwa? na wale wahindi kina mukesh na sailesh je? walikuwa na garage. mukesh alikuwa anaendesha pikipiki ndo ilikuwa icon yake. nani anakumbuka bizeta hotel?
 
Nani alikuwepo Tabora enzi za binti mmoja alikuwa anaitwa Suzy Mapepe,mcheza disko enzi za
Mwanaisungu na TH'??
 
Back
Top Bottom