Kwa Wanandoa: Bila tendo la ndoa hakuna ndoa(?)


Nakuuliza wewe mleta thread! Hivi wewe ukimfumania mke wako na mwanaume mwingine waweza kuendelea kumpa haki yake ya ndoa wakati mnaendelea kutafuta suluhisho?
 

Kwanza fahamu kuwa tendo la ndoa ni sehemu tu ya ndoa lakini siyo kwamba ndilo linaloshikilia ndoa,upo ushahidi wa ndoa nyingi zilizovunjika kwasababu nyingine tu wala si kunyimana.
Pili naomba nikuulize,mahakama ilitoa hukumu lini?Je huyo bwana alikutwa na hatia pasi na shaka yoyote juu ya tuhuma hiyo ya ubakaji?Kama ndivyo,ni sahihi kwako kumtumia kama case study,kinyume chake ni kosa na wewe huwezi kuwa na moral authority ya kumpigia yeye mfano ile hali ukijua kuwa hizo ni tuhuma tu.
Elewa kuwa Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure..
 
vitabu vya dini vinasema 'bila ndoa hakuna tendo la ndoa' wewe unasema 'bila tendo la ndoa hakuna ndoa' kwani wewe ni mpinga dini?
 
nasema na nasema tena ukishampa mwanamke nafasi akamiliki pesa kuliko mwanaume umekwisha.

Ndiyo sababu tunasema tafuteni hela kwa bidii ninyi wanaume! Kumiliki fedha na mali ni sifa ya Mtawala yeyote! Na ninyi Mungu aliwapa zawadi ya UTAWALA! Amkeni!
Ila mnapozembea nafasi zenu lazima mnaowatawala watawapiku!
 

Thank you! Kula 5! Mapenzi au ndoa haina cha maarufu au asiye maarufu, masikini au tajiri mwenye akili sana au zuzu, watumishi wa Mungu au wa shetani! Wala hayana mjanja wala kungwi! Kwanza makungwi wengi ndiyo walishindwaga na ndoa ama hawazipati kabisa!
 

Hakika 1 Tim 6:10 Ukipenda sana pesa ndiyo chanzo cha maovu yote.
 
Tendo la ngono kwa mwanamke linakwenda sambamba na utulivu wa akili.sio ukute mume ni mwingi wa kuiba route halafu mke anajua kisha ukasimamia msimamo huu wa kuendelea na unyumba huku sululu ikitafutwa sahau hilo.

Nimeuliza swali hapa yupo mwanaume atakayemfumania mke wake halafu aendelee kutoa huduma ya tendo la ndoa mpaka suluhisho la mgogoro lipatikane?
 

Umesema vema mkuu.
 
Mimi pia naamini hivyo, kubwaka gani siku mbili mfululizo..I'm sure hadi mauno alikuwa anakata huyu binti, basi tu terms and conditions hazijazingatiwa.


Sent from my iPhone using JamiiForums app
Kwa Sheria ya kujamiiana kama kweli ana miaka 17 alikuwa anabaka. Swali langu je mbona (Bofya) hakuchukuliwa hatua CC Miss Chagga
 
Nimeuliza swali hapa yupo mwanaume atakayemfumania mke wake halafu aendelee kutoa huduma ya tendo la ndoa mpaka suluhisho la mgogoro lipatikane?
Wapo wengi hasa Mamario. Kama household economic power ipo kwa sie. Issue kubwa hapa ni nani anamiliki uchumi wa kaya. Au kwa maneno mengine ni yupi akimwacha yupi atateseka kiuchumi au kijamii
 
huo ndio ukweli
No consumation no marriage.

Lakini hiyo haihalalishi mtu kwenda kubaka hata kama angekuwa mkewe.

Hiyo statement ina maanisha kuwa hapo ndoa hiko matatani na uhalali wake unapotea kwakuwa hakuna tendo la ndoA.

Hivyo alichotakiwa kufanya huyo jamaa si kubaka na wala kunyimwa tendo wala hakuna uhusiano na kubaka hii ni tabia yake huyo mhusika.

Alaf kibaya zaidi ukute walikubaliana na huyo mtoto lakini kinacho leta tafsiri ya kubaka ni kuwa huyo msichana yuko chini ya miaka 18:

Pia jamaa kitendo chake cha kubaka ni ushahidi usio tia shaka
kuwa ametoka nje ya ndoa.

Hivyo basi pengine huyu jamaa ange tafuta wanawake wengine lakini si shemeji yake, hii ni aibu kabisa.


No conssumation no marriage statement haihalalishi kubaka bali kurekebisha ndoa yako.
 
Nakuuliza wewe mleta thread! Hivi wewe ukimfumania mke wako na mwanaume mwingine waweza kuendelea kumpa haki yake ya ndoa wakati mnaendelea kutafuta suluhisho?
watu wengine bhana.hivi mnajua tendo la ndoz ni hisia.au mnajua ni kuchomeka na kutoa tu
 
watu wengine bhana.hivi mnajua tendo la ndoz ni hisia.au mnajua ni kuchomeka na kutoa tu

Thank you! Sasa swali hili lielekeze kwa mleta thread! Yeye ndiye anawaza namna hiyo! kuchomeka na kutoa!
 
Wapo wengi hasa Mamario. Kama household economic power ipo kwa sie. Issue kubwa hapa ni nani anamiliki uchumi wa kaya. Au kwa maneno mengine ni yupi akimwacha yupi atateseka kiuchumi au kijamii

Huyo naye ni mume au ni sex tool? mi nasema mume kama mume mwenye akili na utashi, aliye na uchungu na mkewe na anaye mpenda kwa dhati! Siyo hao walioko kiajira zaidi!
Atavumilia kwavile ni kibarua na si mapenzi ya dhati!
The same applies to us women! Kama mume ndiye mshika hatamu utaishia kulia kubembelezwa na kusamehe kirahisi!
Kama ndiyo wewe unamlisha na kumtake care mara nyngi ni kumfurusha na mabegi yake asikanyage tena nyumbani kwako
 

Kama alimfumania basi alikuwa na uwezo wa kuachana nae (dini inaruhusu) na sio kumyima unyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…