Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Uwepo wa Bahari au Baadhi ya Maziwa mengine hayakuumbwa kama unavyohisi Mkuu..

Kwa mfano zamani Afrika ilikuwa Imeungana na Asia upande wa Mashariki ya Kati ila walijenga Mfereji Kuipata Suezi kanali ambayo itafanya mto mkubwa au Bahari au mfereji mkubwa ambao utatenganisha hayo mabara mawili na haikujengwa zamani ni karne ya 20 tu..

So kuna Baadhi ya Vitu uwepo wake umefanywa na Mwanadamu..
baadhi ya vitu uwepo wake umefanywa na mwanadamu lakini mwana yeye kajireta mwenyewe duniani na kajitengeneza mwenyewe na hivyo vitu uwepo wake vilikuwepo kwa kajitengeneza wenyewe
 
Kwahiyo kitu kama hakionekani upaswi kukiamini, una pumzi una roho na unaviamini na nasfi unaamini kama unayo ushawai kuona hivyo vitu? lakini unaamini unavyo wewe uko timamu kweli, au unasema hivyo uliufanye vitu vyako pendwa bila kufata utaratibu
Ngoja kwanza hapo nimeona umetaja roho na nafsi. Nauliza
Roho ni nini? Nafsi ni nini? Pia nataka kujua tofauti ya roho na nafsi ni ipi!!!?
Karibu
 
Tofauti na kuwa atheist mnaamini kufanya baadhi ya vitu ni dhambi/kosa au most ya vitu mnachukulia sawa
 
Kama ukweli gani au ishara gani ambayo ingebadilisha mtizamo wako?
OK.

Mimi nawaza kimantiki. Logically.

Ukweli una tabia ya kuwa logically consistent.

Kwa mfano. Kuanzia na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote. Ukisema kuna Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, Mungu huyo kuumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya mengi, mauaji, magonjwa, majanga ya kiasili, uonevu, ni logically inconsistent.

Ni contradiction.

Hii logical inconsistency inaleta contradiction, hii contradiction inaonesha Mungu huyu hayupo, ni stories za watu tu.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu huu unaoweza kuwa na mabaya wakati alikuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu huu uwe hauruhusu baya lolote?

Kama huelewi hoja za kimantiki kama logical consistency, contradiction, the problem of evil, unaweza kupata tabu kuelewa nilichoandika.

Kama unaelewa haya ni mambo yaliyo wazi kabisa.

Kwa hivyo, ukitaka nikubali uwepo wa Mungu, angalau weka maelezo ya uwepo wa huyo Mungu ambayo yapo logically consistent na hayana contradiction.

Siyo unanipa stories za Mungu za kuungwaungwa ambazo ukizipima kimantiki unaona kabisa hazina logical consistency.
 
Athibitishe tu kwamba Mungu yupo.

Twende pamoja point kwa point kwenye uthibitisho.
Kwa kawaida kwa akili ya binadamu kila kitu kikiwepo sehemu ni juhudi za watu barabara zikichongwa watu wamepambana internet simu roboti nk Lakini hili la sisi kuwepo duniani amuamini kwa kuna juhudi ama mambo yamefanyika na hii dunia kuwepo hivi unavutia kiasi uoni hata kasoro si juhudi ama kweli natwanga maji kwenye kinu😭
 
Je mnaamini kwamba kuna kuadhibiwa kutokana na matendo mabaya mtu aliyoyafanya kwenye maisha yake au kuna kupata tuzo katika matendo mema mtu aliyofanya kwenye maisha yake?
 
hoja yao kubwa ni kwamba kila kitu ni nature hoja hii haina mashiko hata kidogo
kweli haina mashiko, hata sisi hatuielewi😂

hoja yetu ni kwamba hakuna uthibitisho juu ya uwepo wa mungu

uislamu na ukristo sio dini za watanzania, hazijachimbuka huku

kama kila kitu kinatengenezwa, nani kamtengeneza mungu?
 
baadhi ya vitu uwepo wake umefanywa na mwanadamu lakini mwana yeye kajireta mwenyewe duniani na kajitengeneza mwenyewe na hivyo vitu uwepo wake vilikuwepo kwa kajitengeneza wenyewe
Mkuu Umewahi Kupata Bahati ya Kusoma Hata Strings Theory hapo hata kupata Maelezo yake machache ya Uwepo wa Ulimwengu na Vitu vyote??

Umewahi Kujiuliza kuwa Kwanini Dunia Yetu Baada ya Kupimwa Inaonekana ina Miaka zaidi ya Bilion wakati Kwenye Vitabu vya Dini za Kikristo,Uyahudi na Waislamu wanasema Ina miaka 4006..?

Umewahi kujiuliza kwanini wahindi na Wabudha na dini zingine tofauti na Wakristo na waislmu na wayahudi (Abrahimic Religion) wao wanasema Dunia ina miaka za Milion Moja na watu walipitia kwenye Hiyo miaka Mingi kabla ya Kuumbwa yaani satya Yugas (4,000 years of the gods)ambayo ilikuwa na miaka 1,728,000 na Treta Yuga: (3,000 years of the gods) ambayo ni 1,296,000 na Dvapara Yuga(2,000 years of the gods)ambayo ni 864,000 years na Kali Yuga ambayo ndo inasadikika Binadamu ndo aliumbwa miaka 432,000 iliyopita ...

So Ipi ni Imani sahihi Kwanza Kuhusu Uumbaji Maan Dini zingine zote Kasoro Ibrahimic Religions (Jews,christian na Islam)., haziamini kama Kuna Mungu Mmoja aliyeumba Kila Kitu na kiumbe cha Kwanza Hakuwa Adam na Eva
 
Mfano mimi nilikuwa nasali nipate kitu fulani na nikakipata what is your thoughts on this?Au mtu kaombewa shida husika ikaondoka
Mkuu,

Ukisali na ukapata kitu fulani utajuaje umekipata kwa sababu Mungu yupo kasikia sala zako na kakupa hicho kitu na si kwa sababu yoyote ile nyingine?

Na vipi kuhusu mara zote unazosali kutaka kitu halafu hupati, hilo nalo linathibitisha Mungu hayupo?

Ukiombewa shida ikaondoka, unajuaje imeondoka kwa sababu ya Mungu kasikia na kaiondoa, na si kwa sababu nyingine yoyote?

Na vipi kuhusu siku zote unapoombewa na shida haiondoki, hilo linathibitisha Mungu hayupo?

Unaelewa kitendo cha kusali na kuomba chochote kwa Mungu kinathibitisha Mungu hayupo?

Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote angekuwepo, angejua utakachohitaji kabla wewe hujakijua, na angekupa kabla wewe hujakiomba, na kama hakikufai asingekupa hata tamaa ya kukitaka.

Ukijiona una uhitaji mpaka ukafikia hatua ya kumuomba Mungu akupe kitu, huo uhitaji ni uthibitisho kwamba Mungu hayupo.

Angekuwapo, usingekuwa na uhitaji kabisa. Angekupa unachohitaji kabla hujajua unakihitaji.
 
Sahihi mkuu, ni kupoteza muda tu maana hao jamaa hawapo sawa kiakili
Alafu wao wanajiona smart.

Wanapinga uwepo wa deities, akati imani za kiroho zimekuwepo tangu kale dunia nzima, wakati jamii hazijafahamiana wala kuchangamana.

Je, hua hawajiulizi ni nani alisambaza imani ya aina moja kwa jamii zote duniani zisofahamiana wala kuchangamana?
 
Kuna mmoja nilimwambia siku akifa ndyo atajua nini maana ya MUNGU, saiv acha wakaze mafuvu kwani pumzi wanayo.
 
Uko serious Hujui Sukari Inafikaje kwenye Nanasi na Unajiita Daktari??
Nikurudishe Ujifunze Mambo ya Monosachirides na Complex Sugar Structure kama Starch na Jinsi zinavyopatokana kwenye Ripen Fruits??
Kwani binadamu alitoa wapi akili adi akajua monosaccharides... disaccharides
 
OK.

Mimi nawaza kimantiki. Logically.

Ukweli una tabia ya kuwa logically consistent.

Kwa mfano. Kuanzia na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote. Ukisema kuna Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, Mungu huyo kuumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya mengi, mauaji, magonjwa, majanga ya kiasili, uonevu, ni logically inconsistent.

Ni contradiction.

Hii logical inconsistency inaleta contradiction, hii contradiction inaonesha Mungu huyu hayupo, ni stories za watu tu.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu huu unaoweza kuwa na mabaya wakati alikuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu huu uwe hauruhusu baya lolote?

Kama huelewi hoja za kimantiki kama logical consistency, contradiction, the problem of evil, unaweza kupata tabu kuelewa nilichoandika.

Kama unaelewa haya ni mambo yaliyo wazi kabisa.

Kwa hivyo, ukitaka nikubali uwepo wa Mungu, angalau weka maelezo ya uwepo wa huyo Mungu ambayo yapo logically consistent na hayana contradiction.

Siyo unanipa stories za Mungu za kuungwaungwa ambazo ukizipima kimantiki unaona kabisa hazina logical consistency.
Yaani huyu akili zake ukweli mimi sijasoma lakini nakuona nakuzidi uelewa pakubwa sana, mungu kaumba watu, na kwa mantiki yako ulitaka aumbe watu waliokuwa perfect wasio na kasoro hata kidogo si ndio, ndo unazo zitaja uzuri ubaya n.k, katuumbia sifa zote izo na kutuwekea uwelewa mpana wa kufahamu juu ya yale tutendayo anae fanya uzuri anajua kwamba huu uzuri na huu ubaya na uwezo wote wakuzuia anao, uoni kama sifa za mungu ni kubwa sana, na kubwa tuko dunia kama mtihani ambao tunapaswa tufanye vizuri kwa juhudi ili uko ahera hivyo vitu perfect unavyo vitaka vipo umeelewe?
 
Back
Top Bottom