Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Wewe huelewi kuwa hiyo hoja yako ni hoja ya kuonesha Mungu hayupo.Kwa kawaida kwa akili ya binadamu kila kitu kikiwepo sehemu ni juhudi za watu barabara zikichongwa watu wamepambana internet simu roboti nk Lakini hili la sisi kuwepo duniani amuamini kwa kuna juhudi ama mambo yamefanyika na hii dunia kuwepo hivi unavutia kiasi uoni hata kasoro si juhudi ama kweli natwanga maji kwenye kinu😭
Yani ukichoandika, kwa ntu mwenye kufikiri kwa kina, ni hoja ya kukataa uwepo wa Nungu.
Ila wewe hujajua tu, kwa sababu hufikiri kwa kina.
Kimsingi umeweka hoja kwamba order cannot come out of disorder, vitu haviwezi kuwepo tu vimejioanga, lazima kuwepo na aliyevipanga, na aliyevipanga lazima awe na order au intelligence ya zaidi.
Sasa, unalazimisha Mungu awepo na awe ndiyo huyo akiyepanga (hata kama hoja hii ina non sequitur fallacy kutoka kwako, nitaiendekeza tu kwa sasa).
Tuseme Mungu yupo, na ndiye kaumba haya tunayoyaona.
Bado, kwa kufuata kanuni yako ya order au ibtelligence haiwezi juwapo tu, ni kazima iwe imeumbwa na order au ibtelligence ya juu zaidi, utakuwa umejipa hoja kwamba Mungu naye hawezi juwapo, itabidi awe ameumbwa na Mungu wake.
Na Mungu wake hawezi kuwapo, naye lazima kaumbwa na Mungu wake.
Ad infinitum, ad nauseam.
Hapo utaona msururu usioisha wa miungu wanaoumbwa na miungu wao.
Hapo hakuna Mungu muumba vyote.
Hoja yako inaonesha Mungu hayupo.
Of course unaweza kusema Mungu yeye hajaumbwa.
Which is special pleading logical fallacy.
Na hii special pleading logical fallacy inaharibu hoja nzima kuwa order haiwezi kuwapo bila kuumbwa.
Naandika lakini sina hakika kama unaweza kufuatilia mantiki ya ninachoandika.