Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

😹😹😹 Kweli hatuna uhuru mi nataka kufika 2090 ila siwezi
Mtu anakwambia Mungu katupa uhuru wa kuchagua wakati hata siku yake ya kuzaliwa hajaichagua yeye, hata hajachagua azaliwe au asizaliwe.

Kajikuta tu analamba makamasi.

Sasa hapo ana uhuru gani?
 
Mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyethibitisha Mungu yupo.
Hakuna mtu ambae ata kuthibitishia uwepo wa mungu hapa, hilo ni juu yako duniani tumeletwa ili tupimwe yupi ana akili za kufikiri njia sahihi ni ipi na kuiendea kama
Akili zako zime fikia hapo kuamini hakuna mungu basi hiyo ndio njia uliyo jichagulia subiria malipo yake
Usipoteza muda kuelewesha kitu ambacho huja ruhusu moyo wako ukipokee.
 
Unahakikishaje duniani tumeletwa iki tupimwe? Tumeletwa na nini au nani?

Kwa nini unaongelea suala la kuamini wakati mimi sitaki kuamini, nataka kujua?
 
Nasema hivii,

Mpaka sasa hakuna aliyethibitisha Mungu yupo.

Kama kuna mtu anabisha na kusema Mungu yupo, aje hapa atupe uthibitisho.
Basi kaka inatosha, nimeona huko juu umewapelekea moto mpk wamepoteana..😹
 
Mtu anakwambia Mungu katupa uhuru wa kuchagua wakati hata siku yake ya kuzaliwa hajaichagua yeye, hata hajachagua azaliwe au asizaliwe.

Kajikuta tu analamba makamasi.

Sasa hapo ana uhuru gani?
Hata wazazi hajawachagua, amejikuta ametokea kwa wazazi walevi 😹
 
Basi kaka inatosha, nimeona huko juu umewapelekea moto mpk wamepoteana..😹
Nikichogundua ni kwamba watu wengi wana uwezo mkubwa sana wa kujitungia hadithi za uongo za kujitekenya wenyewe kisha wakacheka wenyewe.

Yani wakishaamua jambo lao kulitetea, hata kama ni la uongo, utakuja na logic zako zote za kuonesha ukweli, lakini watajiondoa akili kutetea uongo wao walioukubali.

Yani ni kama vile wanasema "uongo wetu mtamu tulioukubali ni muhimu utetewe kwa gharama yoyote dhidi ya ukweli wenu mchungu tusioutaka".

Ndiyo maana hapa utabishana sana na watu, utawaekea logical fallacies zote, immanent critique zote, utawaonesha deus ex machina zote.

Lakini ni kazi bure tu.

Kwa sababu washaamua kukubali na kutetea uongo wao.
 
Hata wazazi hajawachagua, amejikuta ametokea kwa wazazi walevi 😹
Naam,

Kuna watu wengi wamezaliwa kwa bahati mbaya tu wazazi hawakupanga, walikuwa wanafanya starehe zao tu, ila wazazi hawasemi.
 
Unahakikishaje duniani tumeletwa iki tupimwe? Tumeletwa na nini au nani?

Kwa nini unaongelea suala la kuamini wakati mimi sitaki kuamini, nataka kujua?
Qur-an (76:02) maamuzi ni yako jinsi gani utumie akili zako hulazimishwi na mtu

Unaweza kujua kitu bila kuamini.?
 
Qur-an (76:02) maamuzi ni yako jinsi gani utumie akili zako hulazimishwi na mtu

Unaweza kujua kitu bila kuamini.?
Quran imejaa contradictions. Nikikuwekea hapa huwezi kumaliza kuzitatua.

Kama maamuzi ni yako jinsi gani utumie akili yako, ikiwa huna akili, bado hapo maamuzi ni yako utumie akili ambayo huna?

Kujua nini na kuamini ni nini na tofauti yake ni nini?
 
Hizi habari kuhusu Mungu, HAKUNA anayeweza kuzielezea kwa ukamilifu.... Wote wanaoabudu au kusema kuhusu Mungu Bado wameaminishwa TU, kwa sababu, kama ni kutegemea maandiko mf. Biblia... Hata biblia yenyewe HAIAMINIKI!...
Ukweli ni kwamba, HAKUNA KITU HALISI (PHYSICAL BEING) KINACHOITWA MUNGU... HAKUNA! Neno Mungu lilipewa "Uhai" ili kuelezea au kutambua NGUVU YA ASILI ambayo ipo kwa daima. Ndani ya hii nguvu ya ASILI ndiko iliko chimbuko la Sayansi na teknolojia, Maarifa ya asili (intuition) ya kiumbe hai na kisicho hai na uhusiano wao katika Hali halisi na fikirika (Realism and Idealism)
Ndivyo Maana hii nguvu inaweza kuwa positive kumfavor mtu au negative kumharm mtu, SASA... waliotuaminisha kuhusu Mungu, wanasema Kuna Mungu ktk mambo positive na yakija negative wanasema Shetani wakati ukweli nguvu ya ASILI (nature) ni Moja TU inayoact in all ways.
Hebu mshangae binadamu alivyo kigeugeu... Akifanya uhalifu akashindwa kukamatwa anasema Mungu memsaidia, lakini akikamatwa atasema Shetani alimpitia.
Wanaoamuni Mungu, wao wenyewe hawajielewi, Hivi inapotokea Simba anacheza na Yanga, Simba wakasema wanaomba Mungu wamshinde Yanga, na at the same time, Yanga wakaomba Mungu wamshinde Simba... Huyu Mungu atakuwa upande Gani?
 
Quran imejaa contradictions. Nikikuwekea hapa huwezi kumaliza kuzitatua.

Kama maamuzi ni yako jinsi gani utumie akili yako, ikiwa huna akili, bado hapo maamuzi ni yako utumie akili ambayo huna?

Kujua nini na kuamini ni nini na tofauti yake ni nini?
Hizo contradictions unaziona kutokana na akili yako inavyo fikiri, hilo sio lengo nime sime hivyo sababu ndio kitu nacho amini mimi,

Sitaki kuamini kwamba huelewi nini wasema
 
Hizo contradictions unaziona kutokana na akili yako inavyo fikiri, hilo sio lengo nime sime hivyo sababu ndio kitu nacho amini mimi,

Sitaki kuamini kwamba huelewi nini wasema
Sasa kama hizo contradictions hazipo ila naziona kwa jinsi akili yangu inavyofikiri na akili hiyo nimepewa na Mungu, hapo kosa ni langu au ni la huyo Mungu kunipa akili isiyoweza kuelewa vizuri?

Kwa nini Mungu hakunipa akili ambayo ingeweza kuelewa na kutoona hizo contradictions?
 
Back
Top Bottom