Ma sha Allah Bi Zainab, nilikwambia umeweza, huyo mteja wako anahakikisha hilo. Mimi nnakwambia, nimeutumia huu udongo wako na nilikuwa nnatumia udongo natural nnaoununuwa nje kwa bei ya juu sana ukilinganisha na huu wako lakini toka last week nimeanza kuutumia huu wako nnadiriki kusema huu wako ni 100% mzuri zaidi na bei yako mama ni kama bure kama alivyosema
Heaven Sent.
Nakushauri anza kufikiria kuusafirisha nje ya Tanzania, unajuwa USA kuna soko kubwa sana la hivi vitu natural na huu kwa kuwa ni mali ya Tanzania 100% kuna mpango wa AGOA unaweza ukapata soko kubwa sana. Jipange dada jipange.
Bidhaa unayo tena safi sana sasa changamkia fursa.
Hongera sana.