Mwanaume hafumaniwi, ulitakiwa kumuomba msamaha kwa kuona mambo yake private kisha mkaendelea na maisha mengine.
Haya Sasa ameshakuonyesha kwenye mahusiano yenu, wewe sio kitu , hata ukisusa atakua na wengine wakati huo huo wewe unaishi ukimuwaza.
Mimi kuna demu aliwahi kunifumania live, alileta noma ile mbaya, ila kikubwa sikuruhusu washikane.
Baada ya mtifuano akaondoka tena kwa mikwara kibaoo, mie nikakausha zangu kimyaaa, baada ya kama wiki, mwenyewe akanitafuta.
Eti nimemkosea na hata msamaha simuombi, nikampa black and white, msamaha siwezi kuomba, kama unarudi rudi, kama umeamua kuanza upya pia sawa.
Siku sina hili wala lile napigiwa simu, funguo ziko wapi nataka kufanya usafi nyumbani, nikamjibu kuna vitu vya kutoa kwanza ndani hutakiwi kuviona, njoo kesho.