Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

My favorite, hii drama na Descendants of the Sun ninazo album zake full na najua OST zote neno kwa neno.
Asee kumbe Song Joong-ki (Yoo Shi‑jin) na yule Dr wake walidate in real Life😃😃

Sikujua hichi kituu leo baada ya comment yako nikasema nikasikilze always maana ni muda sasa kupita kwenye comment nakutana na moja inasema Happy ending in K drama but sad ending in real life🙌🙌🙌
 
Wewe unasema walidate wakati walioana kabisa?

Sad ending in real life maana walikuja kutalikiana hawakudumu hata mwaka nadhani. Na sababu inasemekana Song Hye Kyo alikuwa na lisponsor lake la Kichina 🤣🤣 na Song Joong-Ki hakuwa na muda na ndoa sijui, ah!

Mambo yalikuwa mengi.
 
Huwa sifuatilii kabisa maisha yao labda nikutane nayo kama hivi

Dah ndoa ngumu sana😃🙌
 
Ndio Mzee , mimi nilifuatilia YouTube mkasa mzima wa Mwanangu Consigliere Song Joon Ki , nicheze kama Nifah nikupe udaku ...

Baada ya kutoa Descendants jamaa wakapata tuzo nyingi kwenye tuzo maarufu kubwa Korea za "KBS " kama sikosei wakapata tuzo ya "best couple" of the year kwenye Drama ya Descendants. Baada ya hapo fans wakawa Wana push na kutamani wawe wapenzi kweli wakisema kwenye ile movie couple Yao ilinoga na itakuwa dharau kama watamua watengane bila kudate kweli.

Mahaba yalianza usiku wa tuzo , mwamba wakati wa kuchukua tuzo alikuwa anamtaja kwa hisia Kali sana yule manzi doctor SHK kwamba yeye kamsadia sana kwenye ile series maana kutokana na kutokuwa mzoefu sana alikuwa anapata ugumu manzi ndio alikuwa anampetipeti na kumpa moyo wakati mwingine alikuwa analia mbele yake demu anamfuta machoki Kamanda , kiufupi mwamba alikuwa akideka na manzi aliplay part yake vizuri ndio maana chemistry ikawa hot 🔥 🔥 mpaka kwenye scenes....

Baada ya event ya tuzo tetesi zikazidi kushika Kasi lakini mwamba akawa anakataa kwenye media mwisho wa picha akaona si kweli chap akavuta jiko na Kufunga ndoa nae rasmi..

Baadae kukaja tetesi kuwa hawapo vizuri mwamba akakanusha kuwa wanaendelea vizuri ana enjoy baadae hakukaa sana jamaa akafanya umafia talaka alifuatilia na kuandaa kimya kimya alimuacha juu kwa juu bila kumpa taarifa yaani Manzi aliona taarifa mitandaoni kama kashaachwa jambo ambalo fans hawakupenda na ikamuumiza sana Manzi.

Mwamba akazidi kuwakera Raia alipotoka hadharani na kumsagia kunguni Manzi na kuanika sababu za kuachana na mabaya yake kwenye media huku mwenzake akiwa kimya mda wote na mwamba alidai kuwa Mwanamke hajali mambo ya ndoa na ushirikiano na wazazi wake muda wote busy na anajali mambo , akawa anadai alikuwa anaishi kama haishi kwenye ndoa na safari za manzi zimekuwa nyingi.
 
Baada ya kuachana na drama zilizoendelea kati yao Wakorea walikasirishwa na Mwamba Joong Ki kwa kuona kamuacha mwenzie kiholela na kuanza kumsema kwenye media badala ya kukaa kimya wakati mwenzie alikuwa amenyamaza .

Matokeo yako jamaa movies zake zikizofuatilia zile Hopeless , My name is ... waliziboycut wakawa hawazitazami na mauzo yakashuka pakubwa huku wakimsagia kunguni kwa comments mbovu mitandaoni na reviews za movies zake akawa na flop ya hali ya juu kabla ya kuibuka tena kwenye makali na series "Vincenzo" na " Reborn Rich" baada ya hapo zilizokuja movies " Bogota City" na nyingine zika flop tena .

Sasa ameoa mwingizaji huko Ulaya na ana mtoto mmoja ila wengi wanaona alijiharibia carrier yake na jinsi alivyodili na suala lake la ndoa .
 
Mkuu wewe kwel ni mtu wa movie unakubali mtu kazi maana Gender yenu kila siku wako busy na Lee Minho 😃😃
Wanazi wenzangu wa hili jukwaa wanajua namzimia sana Ill Guk Sung, baada yake ndio anafuata Kim Nam Gil.
Vinginevyo namkubali Kim Soo Hyun pia.

Napenda sana waigizaji halisi, yani wanaoigiza hadi unasahau kama wanaigiza maana wako relaxed kama maisha ya kawaida, ndio hao jamaa wawili hapo mwanzo. Soo Hyun kidogo unaweza kushtuka huyu anaigiza.
 
Jamani ile channel yetu ya kibongo imefungiwa kule Telegram siwezi kuweka chochote, nafikiria cha kufanya.

Imeniumiza sana, mimi na mdogo wangu hapa (kila siku anabadili ID sijui anajiita nani sasa hivi) tumeweka drama nyingi sana kule.
 
Jamani ile channel yetu ya kibongo imefungiwa kule Telegram siwezi kuweka chochote, nafikiria cha kufanya.

Imeniumiza sana, mimi na mdogo wangu hapa (kila siku anabadili ID sijui anajiita nani sasa hivi) tumeweka drama nyingi sana kule.
Wengine Telegram zinakataa hata kufunguka.

Pole sana mkuu, bila shaka utapata ufumbuzi.
 
Hii si ndio walibadilisha star actor ilikua nzuri ila walipobadili aah waliharibu ladha. Sijui jamaa ishu ya bullying iliishia wapi
Dah jamaa yule wa kwenye scarlet heart, ali shinda kesi hiyo ya bullying.
Sema career kama ili sheki kidogo.

halafu una jua wali rudia ku act zile 6 episode?, huyu mpya ali igiza mwanzoni hadi mwisho.
ana jua mno 🔥🔥
 
Kwenye list yako huna Lee Byung Hun😃😃

Kama una huyu mshkaji wa dream High soo Hyun huyo juu hawezi kosa😃😃
 
Jamani ile channel yetu ya kibongo imefungiwa kule Telegram siwezi kuweka chochote, nafikiria cha kufanya.

Imeniumiza sana, mimi na mdogo wangu hapa (kila siku anabadili ID sijui anajiita nani sasa hivi) tumeweka drama nyingi sana kule.
Hatimaye mkafikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…