Kwa Wazazi ambao watoto wenu bado hawajapokelewa shule za English Mediums kwa sababu bado hamjalipa ada, pitieni hapa

Bora waongee kiingereza kibovu kuliko kutokuongea kabisa.. mtoto wako anaambiwa "happy birthday to you"anajibu "the same to you"utajisikiaje kama mzazi?
Kwa taarifa yako siku hizi bongo hadi bodaboda wanajua kiingereza.

Ukitaka kujua nenda kwenye mabanda ya mpira. Mechi ya ligi ya Uingereza wachambuzi wanachambua kiingereza na wabongo wana respond kwa sababu wanajua kinacho ongelewa. Au mtangazaji anatangaza kwa kiingereza na watu wana follow up.


Hukumbuki enzi za Morrisson. Morrison anachukua mike anaongea kwa kiingereza pale kwa Mkapa na uwanja mzima una lipuka kwa sababu wanaelewa anacho kisema..

Hiyo ya kutojua kiingereza ilikuwaga zamani miaka ya 90 sio sasa hivi
 
Hao wanaojua ndio matokeo chanya ya Hizo shule unaziponda.....si umesema wengi wapo mitaani hawana kazi za serikali ndio hao wanaomwelewa Morrison Sasa .
 
Niunganishe namie na hicho kidemu Basi namie niwe nakiwezesha hata mlo mmoja wa uhakika per day. Binafsi ninapenda mwanangu nisomeshe nje from kindergarten to university level Ila Kama Ni hapa hapa bongo no change of environment.
Mie kwenye kusoma naomba mno mtt apende kujisomea na kuwa mdadisi kuwa na curiosity ya kujua dunia na binadamu.

Mie natumia iPhone 20 max pro, nipeni heshima. Yaani nimenunua simu kisa tu ku demand respect or ku command it na sio kuwa kwa matumizi yangu.
Kuna jamaa mmoja alijenga akawa anawaambia wake za marafiki zake wamtembelee waone anapoishi ama alipojenga ili apate respect baadaye sijui awale kirahisi marafiki zake walipojua tu wakamwambia so na sie tukijenga tumwambie mke wako atutembelee.
Yaani mtu hufanyi Mambo kwa manufaa yako Bali kwa show off.
Wanasema ukinunua gari hata kwenda madukani ama gengni kununua mhindi utaenda na gari na hutoshuka na utamwambia kuwaa niletee huo huo hapo hapo pembeni ya huo hapo.
Baadaye unaichoka ndani ya two years ukianza kutoa hela nyingi kuliko unazotoa home kwa chakula Sasa bana utaanza kuwaza kuiuza Mana utakuwa unatoa hela nyingi za spear kisa show off na kuchakatia mbususu ama ku boost self image or high self esteem.
Ila Kama ulinunua Kama una mahitaji na gari nadhani itakusaidia kwa mambo Ila kisa your peer group wote wamenunua na wewe ununue uwe nao sawa hapo utajua why kuku hakojoi pia hukuwa na uwezo Bali ulijibana Kama mama anavyobana watt wake chakula wanakula ngogwe ili tu asuke ama anunue nguo fulani
 
sio tu kukata viuno. hata sokoni hana maajabu hana hit songs. kayumba wanamkimbiza.

juzi alikuwa analia Mario kamyima Korabo. mario mtoto wa buza kayumba analiliwa na mtoto wa Hopac ambebe kimuziki kwa collabo
Muziki ni kipaji haina uhusiano na ulisomea wapi. Na mara nyingi vipaji vya ukweli vinatokaga familia maskini.. Fally Ipupa, Diamond, Ali Kiba, Ferre Gola na wengine wametokea kwenye umaskini. Jengeni hoja acheni hisia
 
ni kayumba pekee ambapo mtoto anajua

kuna kukosa hela(nauli na ya kula),
usafiri ni changamoto haswaa,
kuadhibiwa sio kwamba unachukiwa,
usitegemee kazi pekee,hata waalimu wanauza visheti,
nk

Kwa kweli wanaandaliwa kuwa wananchi ambao wako tayari kukabiliana na changamoto halisi za maisha.
 
Nachoumia nikiwa huko English media nasikia watt wanabwabwaja kiswahili nikimuongelesha mtt English hola.
Bora peleka hata Ghana ama Cameroon mtt atajua English nzuri mno pia pamoja na french
Unaota watoto Wanaongea kingereza kizuri sana ndio maana waliacha kupeleka Kenya na Uganda

English Medium ndizo kitaifa huongoza mitihani ya shule za Msingi ya NECTA wako vizuri mno
 
Muziki ni kipaji haina uhusiano na ulisomea wapi. Na mara nyingi vipaji vya ukweli vinatokaga familia maskini.. Fally Ipupa, Diamond, Ali Kiba, Ferre Gola na wengine wametokea kwenye umaskini. Jengeni hoja acheni hisia
Ni kweli na wacheza ngoma kuanzia za kienyeji Hadi muziki wengi Huwa watu maskini au watoka familia za kimaskini
 
Ni maneno machungu kama chloroquin ila ndio ukweli wenyewe. [emoji1531]
 
[emoji1541]
 

Attachments

  • 1697309589534.jpg
    59.3 KB · Views: 1
Kama pesa unayo poa tu siyo mbaya kumpeleka mtoto shule za gharama, shida inakuja kuna watu uwezo hawana halafu wanalazimisha kuwapeleka shule za ghali matokeo yake wanaanza kuwasumbua ndugu na jamaa kwa kuwaomba waongezewe pesa ya ada ya mtoto wake anayemsomesha shule za ghali.
 
Na hao ndio wengi mkuu kifupi hao ni masikini wanao jaribu kuuficha umasikini wao kwa kuwasomesha watoto wao English Mediums wakiamini kwamba watu watawaona wana hela..ni utoto tu ndo unawasumbua
 
Mimi nashauri peleka private

Muda mwingine akili ya mwanadamu inachangamshwa na majukumu.

Ukianza kutajiwa zile milion milion za kulipa lazima uongeze kasi ya utafutaji hata kule ambapo hukuwahi kufikiria.

Unaweza kupata faida ya kuona uwezo wako halisi wa kupambana na maisha.

Kumtupa mtoto kayumba kisa unakimbia gharama utajikuta una relax na hari ya kutafuta zaidi inapungua.

Ushauri wangu msiogope changamoto

Changamoto zinatujenga zinatufunza mengi sana.

Usiseme uwezi, simama pambana.

Leo ada inakukatisha tamaa, kesho utaambiwa unahitaji milioni kadhaa kulipia matibabu yako au mwanao.

Point yangu ni kwamba tutafute zaidi na zaidi bila kuogopa.

Ikishindakana kabisa basi rudisha mpira kwa kipa, ujipange upya.
 
I support you kuwa don't seek to reduce or minimize cost of living but rather seek to maximize earning or investment Ila ukiwa na hii hii discipline why usiwekeze, yaani Ile 4M unayolipa kwa mwaka nurture discipline ya kumuwekeza mahala hata Germany Bund
 
Asante sana ndugu yangu yangu.
Nitazingatia sana ushauri wako huu, Asante tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…