Kwa Wazazi ambao watoto wenu bado hawajapokelewa shule za English Mediums kwa sababu bado hamjalipa ada, pitieni hapa

Kwa Wazazi ambao watoto wenu bado hawajapokelewa shule za English Mediums kwa sababu bado hamjalipa ada, pitieni hapa

Mleta mada na wewe tafuteni Hela .

Wenye Hela hawalalamiki na Wala hawahitaji mleta mada lofa awasemee au kuwashauri na vi theory vyake Koko ohh production ohh what what atafute Hela

Maskini Huwa na vi theory vya ajabu ajabu na hujitia kuvielekeza Kwa Wenye nazo Eti ohh mabwege Wanapigwa.Hela zao wanalipa halafu lofa anajitia kuwa ohh mnapigwa Wakati uwezo wa kupeleka huko mtoto Hana

Uzuri Wenye pesa Huwa hawapokei ushauri Kwa mtu lofa Huwa wanapeana ushauri wao Kwa wao

Mleta mada lofa vi theory vyako peleka Kwa malofa wenzio
Hahaaaaa
 
Wakati tunasoma kijijini, majirani walikuwa wanamshauri mzee kwamba kwa nini anahangaika kusomesha watoto sekondari, kwa nini asituegemeze kwenye kilimo, mbona kinalipa? Mzee aliwajibu kuwa, alikuta babu yake analima, akamuona baba yake analima na ueye akaingia kulima, lakini haoni mabadiliko. So ameamua kusomesha watoto ili wajaribu kupata experience ya tofauti.

Nikirudi kwenye mada, wazazi tulio wengi tunesoma Kayumba. Tunajua raha na karaha zake, fursa na changamoto zake. Tunapojitutumua kuwapeleka huko English mediums, tunataka wapate experience, japo kidogo, tofauti na Kayumba.
Pili, kuchelewa kumlipia mtoto ada sio kushindwa. Ni suala la muda tu. Changamoto hazikimbiwi. Akisolve, mtoto akapokelewa shule, ndo kushinda changamoto huko.

Mwisho kabisa, dunia inabadilika. Msomeshe mtoto kulingana na mahitaji yake ya baadae, sio kwa mahitaji yako.
 
Jirani yangu alisoma Tanganyika international school,,,Ile shule husoma watoto ambao wazazi wao hutoka mataifa mbalimbali huja kufanyakazi Tz.Huyo jirani yangu Kwa Sasa ni dalali WA vyumba mjini.🤣

Jirani angu mwingine alisoma st Mary's school,,,Kwa Sasa ni mwinilisti haya makanisa ya mwendokasi.

Jirani WA tatu alisoma Uganda,,,,Kwa Sasa hajulikani anachofanya(Hana kazi)
 
imefikia hatua sasa ubora wa elimu anayopewa mtoto unapimwa kwa yeye kuongea kiingereza fasaha akiwa na baba yake au mama yake wakiwa matembezi weekend.

maarifa na uelewa wa mambo sio kipaumbele.

ndio sababu akina matumbotumbo mmewaona wameanza kuwaandaa watoto wao kwenye stream za uongozi kupitia ccm chipukizi,miaka 10 ijayo haitakuwa tena unajua kiingereza kiasi gani tukupe kazi(hazitakuwepo).itakuwa umejifunza nini shuleni kuja kupambana na masumbwi ya maisha???

anayewekeza $$ kwenye elimu ya mwanaye,asisahau kumuandalia na walau kiwanja\biashara au shamba atakaloanzia.
ur the true son of your father
 
Mleta mada na wewe tafuteni Hela .

Wenye Hela hawalalamiki na Wala hawahitaji mleta mada lofa awasemee au kuwashauri na vi theory vyake Koko ohh production ohh what what atafute Hela

Maskini Huwa na vi theory vya ajabu ajabu na hujitia kuvielekeza Kwa Wenye nazo Eti ohh mabwege Wanapigwa.Hela zao wanalipa halafu lofa anajitia kuwa ohh mnapigwa Wakati uwezo wa kupeleka huko mtoto Hana

Uzuri Wenye pesa Huwa hawapokei ushauri Kwa mtu lofa Huwa wanapeana ushauri wao Kwa wao

Mleta mada lofa vi theory vyako peleka Kwa malofa wenzio
Wewe pesa unazo mkuu?Au umejitolea kuwa msemaji wa wenye pesa?
 
Jirani yangu alisoma Tanganyika international school,,,Ile shule husoma watoto ambao wazazi wao hutoka mataifa mbalimbali huja kufanyakazi Tz.Huyo jirani yangu Kwa Sasa ni dalali WA vyumba mjini.🤣

Jirani angu mwingine alisoma st Mary's school,,,Kwa Sasa ni mwinilisti haya makanisa ya mwendokasi.

Jirani WA tatu alisoma Uganda,,,,Kwa Sasa hajulikani anachofanya(Hana kazi)
Duh inasikitisha sana aisee
 
Wazazi wengi hupenda kupeleka watoto wao shule za bei kubwa sio kwamba wapate elimu bora tu(ambayo kimsingi si kweli) ila pia wapate connection yaani kuwaandalia connection mapema. Sijui nimeeleweka hapa🤔🤔

Maisha yameshabadilika sana tokea enzi hizo aise connection ni muhimu sana.
🤣🤣🤣 kwa hiyo wanacheza kamari?

Anyways basi watakuwa vilaza hao wazazi kwa sababu hakuna connection yoyote anayo ipata mtoto kwenye shule za English Mediums.

Bora hata Kayumba walau atatengeneza network ya watu wengi
 
Usitegemee mwanao asome senti kayumba afu aje awe na connection nzuri baadae ( hapa tunaangalia badae na sio sasa).

Kama una uwezo wa kufanya hivyo fanya maana sio kwaajili yako bali ni kwaajili yake, yaani kwaajili ya maisha yake ya badae.
Hakuna connection yoyote shule za English Medium mkuu Narudia tena hakuna.

Bora hata Kayumba atatengeneza network ya watu wengi.

Mtoto anatakiwa apate maarifa yatakayo mfanya atafutwe na watu.
 
Msome upya mleta mada, mleta mada ana hoja tena hoja ya msingi sana.
Hajamlazimisha mtu asimpeleke mtoto wake kwenye English medium bali amewashauri wazazi wasio na pesa ya uhakika huku wanateseka sasa kuwapeleka watoto English medium. Ule woga itakuwaje ikiwa mtoto atakwenda St Kayumba uwaondoke.
ur the true son of your father
 
Maisha Yao Yako sawa na hao wabeba vidumu na mifagio shule za kayumba? Are they equal with them?
Hamisa Mobetto kasoma Kayumba kuanzia Msingi na sekondari kasoma shule ya kata.

Hao kina Paula wamesoma hizo English Mediums lakini wanadanga. Huna hoja mkuu
 
Mleta mada umewapa ushauri mzuri sana watu wasio weza tena hizi shule ila nipende kukuambia swala la mtoto kutokua na akili na kasoma shule za bei sio Matatizo ya shule tatizo linaanzia kwa mzazi hata mtoto umpeleke ist kama huna ufuatiliaji mzuri mtoto atajua kiingereza ila swala la uelewa kwake itakua ngumu..... Alafu unataka mtoto awe na akili mama na baba yake wana akili hizo unazotaka au mtoto azitoe wapi wakati wazazi ni punguone
 
Kila mtu asomeshe kulingana na uwezo wake.
Usiumie kisa mtoto kwenda shule
Mleta hajielewi ana pepio la umaskini

Aende hoteli za kitalii watu wananunua soda chips elfu Tano Wakati mtaani inauzwa mia Tano na Wanajua hawahitaji mtu awaambie

Wanaenda supermarket wananunua nyanya sawa na fungu elfu sita Wakati magengeni zinauzwa elfu moja fungu na Wanajua hawahitaji mtu awaambie nyanya zile zile gengeni uswahilini elfu moja

Waweza mporomoshea matusi ya nguoni kuwa hawaendi hata zingeuzwa mia au kutolewa bure
 
Back
Top Bottom