Huo u-nondo mnaowasingizia waliopita Diploma ni upi? Mimi binafsi nilipita Diploma ile ya miaka ya nyuma ambayo mnasoma hadi mnaanza kuwaambia wanaosoma Shahada hawawazidi kitu, lakini baada ya kwenda kusoma Shahada niligundua sikua na kitu cha ziada kwenye masomo ninayoyasoma (labda masomo machache saana ya miaka ya mbele ndo yalikua na mfanano), nimebahatika kufundisha chuo kuanzia ngazi ya Diploma ninafahamu hali ya wanafunzi wangu.
Sijaona faida yoyote aliyoipata mwanafunzi aliepita Diploma kwa kozi za Afya (hasa hizi za sikuhizi za Nactvet). Zaidi ya kujikuta mjuaji kwa vitu vichache alvyokalili.
Labda sababu pekee inayoweza kunifanya nimshauri mtu kwenda Diploma ni ongezeko kubwa la ufaulu kwa kidato cha sita. Hali ilivyo sasa kama mtoto hana uhakika wa kupata Div I ya point 5 kushuka chini, kozi za Afya ataishia kuzisoma kwenye kitabu cha Mwongozo cha TCU, ambapo kwa aliepita Diploma akipata GPA ya 3.5 anakua na uwezekano wa kupata Admission kwasababu vyuo huwa vina nafasi maalum za wahitimu wa Diploma.