Kwa zama tulizopo ni bora mtu kwenda Ordinary diploma au Advance Education (Form 5 na 6?)

Kwa zama tulizopo ni bora mtu kwenda Ordinary diploma au Advance Education (Form 5 na 6?)

Wote huchekelewa kupata kazi na kuteseka, au kutokupata kazi kabisa na kuwa machinga, au kulima Matikiti, au kuteseka na bidhaa za alovera
 
Hili linatokeza hasa Kwa vijana waliozaliwa 1990s hadi Sasa hivi.

Nimeshuhudia kukiwa na chuki na kejeli za wazi baina ya vijana wa diploma wakiwaambia vijana wa A-level kuwa wanapoteza muda huko na hakuna faida yoyote ya kitaaluma wanayopata.

Sasa naomba tujadili Kwa hoja, je Diploma ni bora kuliko A-level katika kuandaa wataaluma katika kozi za SAYANSI, teknolojia, injinia na hesabu (STEM) wanaojiandaa kuingia level ya degree?

Au diploma ni njia tu rahisi ya kupata kazi na haitaji nguvu nyingi sana za kusoma kuliko A-level.

Kwamaoni yangu diploma inarisk ndogo ya kufeli lakini haiandai mtaaluma competent hasa kwa hapa Tanzania

Je ww unamaoni Gani?
Je ww ni zao la diploma?

Mwisho, ukinitajia Best students wa vyuo vya serikali kuanzia mwaka 2015 hadi 2024 aliepitia diploma nasio A-level kuna elfu 50 ya supu ya chap hapa 😄
Labda umekutana na watu ambao hawaja mature, suala la wivu ni ni subjective sio suala la kundi fulani, so chunguza mazingira yako

Lakini kwa maelezo yako kusema A-level ni ngumu kuliko diploma ni pathetic approach

Diploma za engineering kwa vyuo vinavyoeleweka ni tight

I know (nimesomesha) , na nilisoma chuo nikiwa na watu walipitia diploma back in the days and kuna utofauti sana
 
Tunahype sana degree
Degree ambazo zimebase kwenye theory.
Diploma ilibase kwenye utendaji zaidi
Wakati degree ilibase kwenye management.

Huko duniani wanachojua wao ni lazima mtu afike high school hivyo ukiishia form four hajafika high school.

Ila sio sababu unazotoa wewe.
N.B hata Jiwe alikuwa na diploma ya elimu
 
Kuna Fani lazima upite advance mfano MWALIMU wa SECONDARY advance inakuhusu maana mbali na kusoma pia uko Live Field kuona Topic zinavunjwaje na walimu,wanaanzia wapi wamalizie wapi,udhaifu wa walimu ni upi ili na wewe uje uboreshe.

Upo darasani lakini pia unaendelea na tafiti za nini uje ufanye utakapokua mwalimu wewe.

pengine kote asee Matokeo yakiruhusu uende Diploma Nenda DIPLOMA

Mwanafunzi wa DIPLOMA ni nondo mno, mtu aliepata Degree kwa kuanzia Diploma na aliepata degree kwa kuptia 5 na 6

Wa Diploma yuko Nondo mno na experience kubwa sana.

Diploma Vs Advance = Diploma
 
Tunahype sana degree
Degree ambazo zimebase kwenye theory.
Diploma ilibase kwenye utendaji zaidi
Wakati degree ilibase kwenye management.

Huko duniani wanachojua wao ni lazima mtu afike high school hivyo ukiishia form four hajafika high school.

Ila sio sababu unazotoa wewe.
N.B hata Jiwe alikuwa na diploma ya elimu
Ni kweli kabisa mkuu.
 
HESHIMA MBELE wakuu.

Kama mnavyojua kuwa mwezi wa saba umefika na tayari wale wanafunzi ambao walifaulu kwenye mtihani wa NECTA mwaka, wengine wanaenda kidato cha tano na cha sita huku wengine wakianza mipango ya kuingia chuo kwa maana ya Ordinary Diploma.

Sasa nilitaka kujua iwapi level hizi za elimu hizi zina ubora sawa ama kuna moja ina ubora kuliko nyingine.

Kati ya elimu hizo mbili ipi ni nzuri zaidi kwa mtoto, bora asome chuo cha kati au bora asome kidato cha 5 & 6?

Na kwa zama tulizopo ni bora mwanafunzi aende Diploma baada ya kumaliza kidato cha 4 au aende Advance kwa maana ya Kidato cha 5 na 6?
Bora chuo ili kuwahi kupata kipato binafsi. Akiwa na kipato cha uhakika atasoma anachokipenda kwa ngazi za juu
 
kwa upande wangu aliyeenda diploma ndiyo ana kitu cha zaidi, yaani alosoma diploma akija kuendelea Degree na yule alotoka Advance wa Diploma anakuwa na maujuzi kibao
Kupata nafasi ya digrii kwa diploma anakiwa mtu awe na ufaulu wa juu mno tofauti na wa advance
 
Inategemea na Career kama ni Upande wa Afya nenda 5 and 6 ila Kwa field zingine zote zilizobaki anza na Diploma faida ni nyingi sana. Sana kwanza employer saivi majority Wana ajili watu wa diploma kuliko degree holders ivo nafasi za kazi za Diploma ni nyingi sokoni kuliko degree.
Uongo
Kazi za diploma ziko wapi? Toa mifano michache
 
Tunahype sana degree
Degree ambazo zimebase kwenye theory.
Diploma ilibase kwenye utendaji zaidi
Wakati degree ilibase kwenye management.

Huko duniani wanachojua wao ni lazima mtu afike high school hivyo ukiishia form four hajafika high school.

Ila sio sababu unazotoa wewe.
N.B hata Jiwe alikuwa na diploma ya elimu
Engineer ni kazi ya management? Ni theory'?
 
Wa advance anatakiwa awe na ufaulu wa chini ama?
Ndio
Diploma wanaopenya kusoma digrii kama za Engineering au udaktari pass zao huhitajika kuwa juu mno Hivyo wachache sana hupenya

Diploma mara nyingi kama huna mpango wa kusoma digrii za sayansi basi kasome Diploma
 
Ndio
Diploma wanaopenya kusoma digrii kama za Engineering au udaktari pass zao huhitajika kuwa juu mno Hivyo wachache sana hupenya

Diploma mara nyingi kama huna mpango wa kusoma digrii za sayansi basi kasome Diploma
Principle pass mbili kwa kila degree na vigezo vingine, hio engineering unayoisema kwa advance LAZIMA mwombaji awe nazo mbili + angalau B kwenye Mathematics, huo udaktari hata sihitaji kukueleza MUHAS, CUHAS, UDOM, KCMC wanavigezo na mchujo mzito kwa waadvance sawa tu na hao wa diploma.
 
Back
Top Bottom