Kwaheri Tulia, karibu sana Sugu jimboni Mbeya

Mafuriko yaliyotokea uyole ya kati hapa,waathirika wote wa mafuriko wamepewa mahindi debe mbili mbili na godoro foot 2 na huyu Tulia...sasa wapiga kura ndo hawahawa maskini....sa itakuwaje? Sijui labda
Uyole ni kama 5% ya population ya Mbeya mjini. Msaada kwaajili ya wahanga wa mafuriko ni jambo jema lakini haiwezi kuwa tiketi ya kupata ubunge. Kwani huo msaada ilikuwa hongo?
 
Siku hiyo hakikishen hesabu mkononi na kura zinalindwa kwa nguvu zote, ile team ya goli la mkono iko kazini

wanakwambia uchaguzi uliibiwa 2020 na dhalimu,kwa sasa watashinda tu maana haki imetawala
IMG_0264.jpg
 
hapo mbeya mjini hakuna mwanachama mwingine wa chadema mwenye uwezo wa kugombea ubunge lazima awe sugu , kama ni hivyo basi wote nyie hapo mbeya ambao ni wanachedema ni ng'ombe , yaani aende bungeni arudi tena aende huyohuyo wengine ni kushabikia tu huu utakuwa ni ujinga, na umenikumbusha jambo demokrasia ndani ya chadema lilikuwa ni tatizo na likiendelea hivo basi chama hakifai
Kugombea kupitia upinzani ni sadaka hasa, si wengi wenye uwezo wa kujitoa sadaka. Unaweza kugombea, ikawa ndiyo njia yako ya kwenda jela, ni wangapi wapo tayari kwa hilo?

Wachache walio tayari kuyabeba hayo madhira waendelee kugombea kuoitia upinzani.
 
Uyole ni kama 5% ya population ya Mbeya mjini. Msaada kwaajili ya wahanga wa mafuriko ni jambo jema lakini haiwezi kuwa tiketi ya kupata ubunge. Kwani huo msaada ilikuwa hongo?
Huwajui wamama wewe😂
 
Uhalisia ni kwamba Tulia 'alishindishwa' na wenye maguvu tu siyo chaguo la wana mbeya
Kwa ujumla hao wanaoitwa wabunge wa sasa hivi, ni wateuliwa wa marehemu. Wengi wao hata kwenye kura za maoni ndani ya CCM, kupita ni kazi. Robo tatu yao, walikataliwa na wajumbe kwenye kura za maoni, dikteta marehemu aliwapachika kama alivyotaka.

Kwa Mbeya mjini ambayo ni mkoa jirani, kwa ninavyoifahamu, Tulia akishinda kwa uchaguzi wa haki, itakuwa miongoni mwa miujiza ya karne.
 
Kwa kweli mheshimiwa sugu asichome pesa zake kwenye kampeni. Iwe kwa halali au wizi wa kura, tulia lazima arudi bungeni. Chama dola cha ccm hakiwezi kumwacha spika wake aangushwe. Watahonga kila kaya na watatumia polisi.
Yani afee beki afe kipa sugu hawezi kutangazwa
Huo ujinga wa Magufuli ulizikwa naye kaburini tarehe 27/03/21. Tulia arudi Rungwe kwao, hatutaki kinyago Mbeya
 
Kufuatia shughuli za siasa kuruhusiwa rasmi nchini sasa rasmi sisi wana Mbeya tumeshamuaga Tulia na kumkaribisha mh Sugu.

Namaanisha kuwa tulipatiwa mbunge ambaye halikuwa chaguo letu sisi wana Mbeya.

Sasa wakati umefika wa wana Mbeya kuonyesha hasira zetu kwa kumchagua mbunge ambaye atakuwa ni chaguo letu mh Sugu.

Tulia rudi kwenu wanako kufahamu maana hapa uliletwa kwa lazima.
Spika ang'okenkirahis sidhani
 
Huo ujinga wa Magufuli ulizikwa naye kaburini tarehe 27/03/21. Tulia arudi Rungwe kwao, hatutaki kinyago Mbeya
Waulize ACT kinachowakuta chaguzi za zanzibar.
CCM ni ile ile
 
Kufuatia shughuli za siasa kuruhusiwa rasmi nchini sasa rasmi sisi wana Mbeya tumeshamuaga Tulia na kumkaribisha mh Sugu.

Namaanisha kuwa tulipatiwa mbunge ambaye halikuwa chaguo letu sisi wana Mbeya.

Sasa wakati umefika wa wana Mbeya kuonyesha hasira zetu kwa kumchagua mbunge ambaye atakuwa ni chaguo letu mh Sugu.

Tulia rudi kwenu wanako kufahamu maana hapa uliletwa kwa lazima.
Kwake wapi?
 
Huyu maza aliachie jimbo alivamia Lina wemyewe ...akitaka ubunge akagombee dodoma mjini...naoo si guarantee.

Mama Samia kama kweli umeamua haki bin haki CCM harudi mtu.
Hawezi kuamua haki bin haki maana hata yeye ataliwa kichwa asubuhi na mapema
 
Habari ya Asubuhi wana jamii,

Leo Mh. Waziri mkuu anatarajia kufanya ziara mbeya mjini/mbeya city. Moja kati ya kero kubwa hapa mbeya mjini ni bajaji ambazo hazina utaratibu maalumu kama vyombo vingine vya moto.

Hii imekuwa kero kubwa sana hapa mjini tofauti kabisa na majiji mengine, utaona utaratibu wa bajaji zipite njia ipi, na kwa utaratibu fulani.

Hapa Mbeya hakuna utaratibu wowote, bajaji zinaamua zipite kwa namna zinavyojisikia, na wakati mwingine, traffic wanapewa fimbo eti kuzicontrol bajaji zipite njia gani. Hii kwa kweli si haki kwao traffic na inatengeneza uadui na vijana waendeshao bajaji. Zaidi sana vijana hawa wamekuwa wababe sana barabarani, mpaka kupelekea ajali za mara kwa mara, tumeshuhudia mtelemko wa simike ajali kadha wa kadha waanga wa ajali hizo sana sana ni bajaji kutokana na ukaidi pindi wanapopewa tahadhari. Lakini kwenye mataa ya mafiati baajaji hazifuati utaratibu wowote wa mataa, wao mda wowote wanapita kwenye mataa.

Ni wazi kwamba, bajaji hizi haziguswi kwasababu zinasadikika ni za kiongozi mmoja wa mhimili mkubwa wa nchi hii. Na zingine baadhi ni za polisi na watumishi sekta fulani. (Minong'ono ya mtihani). Tetesi hizi zimekuja baada ya kuona hakuna hatua zozote zinachukuliwa kwenye bajaji hizi, zaidi ya kuwapanga traffic mida ya jioni kuwashukia fimbo bajaji wapite pembezoni mwa barabara, of which zoezi hilo limekuwa gumu na la mateso kwa traffic hao.

Jambo jingine ni BARABARA. tunashuhudia wenyewe barabara kuu iendayo zambia kweli ni nyembamba sana, hivyo kuleta foleni kubwa zamani ilikuwa jioni, sasa ni toka asubuhi kuna foleni, mojawapo ni bajaji, ambao hupita njia moja na magari, huku wakipakia abiria katikati ya barabara of which pia imekuwa ikitengeneza foleni sana ya magari makubwa na madogo.

Jambo lingine, ni uwepo wa mikokoteni barabarani, hii imekuwa kero nyingine. Kuna service road pembeni. Lakini baadhi ya watu wanapita katikati barabara, bila wasiwasi na hata mamlaka zipo kimya..Hili laweza kuleta madhara makubwa ya ajali n.k.

Jambo lingine, Ni service road kuwekwa udongo, bila ya ukarabati, hivyo kupelekea shida ya matope na kutwama maji.

Wadau, na wakazi pamoja na watu wote wenye mapenzi mema na mkoa huu. Tusaidiane kufikisha hizi kero. Kwani Mbeya kuitwa jiji hakuendani na hadhi ya ujiji kwa haya yanayoendelea.

Sote kwa pamoja katika maenedeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Ndimi,
Asumwisye Amenye Mwaipopo
 
Wacha wafe tu maana wanajitakia kwa ujeuri wao
 
Back
Top Bottom