Kwahili la Mabasi kusafiri Usiku, nampongeza Mbunge Tulia Ackson

Nchi za kimaskini ni matatizo sana,usafiri wa kwenda sehemu yoyote unatakiwa kuwepo muda wowote na sio kupangiana wakati.
Inatakiwa kama Upo Dar na unasafari ya mwanza-uondoke hata sa 5 Mchana.
 
Sawa mkuu
 
Tujiandae na kulia sana
Ajali nyingi mchana Usiku itakuwaje
Wakati wa kuwekewa mawe barabarani/Kitonga ni nyakati za Usiku
Watakaoteseka ni wamama wazee na watoto
Hii nchi inazidi kurudi nyuma…
 
Wakati serikali ya Mwinyi inapiga marufuku mabasi ya abiria kutembea usiku nilikuwa Bado mdogo ila naikumba ile ajali ilikuwa mbaya sana kama sijakosea lile Bus lilichanika ubavuni abiria wakawa wanamwagika kama Michele

Changamoto za safari za usiku
1) Barabara zetu hazina taa hivyo dereva anategemea ta za Gali tu

2) Barabara zetu ni nyembamba sana

3) Maloli yanayo haribika barabarani huwa hayatolewi na kuwekwa katika road reserve kama nchi nyingine hapa kwetu Loli linakaa hata siku 3 barabarani

4) Kuna ukungu pia ni chanzo kikubwa sana Cha ajali kwa Magali yanayosafiri usiku

5) Mabusi ya siku hizi Yana speed sana madereva lazima watashawishika kutembea kwa speed kubwa

6) kwa Sasa barabara ya Dar to Dom ipo bize sana na ajali nyingi zitatokea hapo
 
Mbona Kuna coaster za Dar to Singida -Mwanza?! Zinasafiri usiku
 
Tujiandae na kulia sana
Ajali nyingi mchana Usiku itakuwaje
Wakati wa kuwekewa mawe barabarani/Kitonga ni nyakati za Usiku
Watakaoteseka ni wamama wazee na watoto
Hii nchi inazidi kurudi nyuma…
Seems huna taarifa sahihi, Mabasi kadogo na Malori yanatembea
 
Sa tatu watu wanaenda mbeya mwanza..wasubir tu pakuche wapande sauli
 
Upo nchi gani toka 2018 bus zote zina vts speed ni 85,kph
 
Juzi kati nilikuwa natoka maeneo ya kusini nilikuwa ktk speed ya 140KM/H Kuna busi lilinipita na likapotea kabisa machoni kwangu Ina maana yule Jamaa alikuwa katika 160KM/H au 170KM/H

Anyway usiku Kuna changamoto nyingi kama vile Maloli kuharibika njiani , wembamba wa barabara zetu na ukungu mida ya sa 10, 11 hadi sa 12
 
Safari za usiku zilikuwepo katika nchi yetu Tanzania.Nakumbuka miaka ya 1986 tulisafiri sana kutoka Dodoma KWENDA Dsm.Tuliondoka saa mbili usiku Dodoma na kufika Dsm saa kumi na mbili asub.Safari hizo zilizuiliwa Mwaka 1992 na wazir mkuu wa Wakati huo Dr John Samuel Malechela baada ya ajali mbaya ya basi ,ambalo silikumbuki na kuwaua watu wengi sana.Sababu ya ajali ilielezwa kuwa ni kutokana na dereva kushindwa kuona vizuri.Kwa upande wangu mm nafikiri mheshimiwa spika wa Bunge kabla hajashauri kuhusu hizo safari angeangalia emprical review .Yaan nn kilisababisha zikazuiliwa.Je hizo sababu bado zipo?Je ajali tu za mchana zimepungua?Mm naona sababu za ajali za usiku kwa Sasa ni nyingi sana kuliko Mwaka huo 1992.Kwa Sasa Kuna malori yanayofeli breki mengi sana barabarani.Tutegemea vifo vingi vya Watanzania.Kama mchana tu malori yanafeli breki,usiku ndio vifo vitakuwa vingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…