Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umesema vyema sana ila Kwa sasa 2022 na 1992 utakubaliana na Mimi kuwa Hali ni tofauti, sababu kubwa haikua barabara tu ila ni Ulinzi na usalama kutokana na mapori makubwa ila Kwa sasa, kwa mfano Kahama to Nyakanazi ya 1992 sio Kahama to Nyakanazi ya 2022, Eneo kubwa limejengwa na Eneo lote ni lami , sasa Kuna sababu Gani magari ya Bukoba kwa mfano, yalazimishwe kulala Kahama na sio Nyakanazi? Huu ni mfano.,..Safari za usiku zilikuwepo katika nchi yetu Tanzania.Nakumbuka miaka ya 1986 tulisafiri sana kutoka Dodoma KWENDA Dsm.Tuliondoka saa mbili usiku Dodoma na kufika Dsm saa kumi na mbili asub.Safari hizo zilizuiliwa Mwaka 1992 na wazir mkuu wa Wakati huo Dr John Samuel Malechela baada ya ajali mbaya ya basi ,ambalo silikumbuki na kuwaua watu wengi sana.Sababu ya ajali ilielezwa kuwa ni kutokana na dereva kushindwa kuona vizuri.Kwa upande wangu mm nafikiri mheshimiwa spika wa Bunge kabla hajashauri kuhusu hizo safari angeangalia emprical review .Yaan nn kilisababisha zikazuiliwa.Je hizo sababu bado zipo?Je ajali tu za mchana zimepungua?Mm naona sababu za ajali za usiku kwa Sasa ni nyingi sana kuliko Mwaka huo 1992.Kwa Sasa Kuna malori yanayofeli breki mengi sana barabarani.Tutegemea vifo vingi vya Watanzania.Kama mchana tu malori yanafeli breki,usiku ndio vifo vitakuwa vingi sana.
Kujenga tu mazingira ya RushwaNakubaliana na wewe.Nilikuwa nashangaa magari yanazuisa moro ikifika saa 6 usiku kwa yanayoenda Dar nikabaki najiuliza Dar Moro kuna hatari gani?
Ewaaaaaaa Majinja alikua anaanzia Lindi nadhani, Dar then Mbeya pia alikuepo Rungwe na Osaka au Chakito kama sijakosea, akaja Dar Express au Kilimanjaro wote hawa wamezuiliwa ila coaster zinaruhusiwa...sasa hizi ni akili au matope?!Mwaka jana mwezi wa tatu, tarehe pendwa, 17.07.2021 nilipata bahati ya kusafiri kwenda Mafinga na basi la Majinja lililoanza safari ya kuelekea Mbeya saa 11 jioni pale Mbezi Magufuli. Hata ile breaking news niliipatia ndani ya basi.
Kipindi kile mabasi ya New Force na Majinja yalisafiri usiku kwa wiki moja kisha yakapigwa marufuku.
Tunataka safari za usiku zirudishwe kama miaka ya zamani
Hakuna shida kwenye barabara, ni kuongeza tu maderevaRoot ya usiku imekaa Poa…Japo kuna changamoto kwenye barabara zetu haziruhusu root hyo ifanyike kwa fasaha.
Changamoto nyengine ni mabasi na madereva.
Kenya na Uganda na Burundi hawanaga huu ujingaHii nchi tunapangiana ka boarding bwana
Ndio, Kwa sasa ni Kigoma tu ndio Ina changamotoBarabara zote ni nzuri na zinaruhusu kusafiri usiku?
You nailed it BroMbona mna maswali ya kipimbi sanaa? Hivi mnajua miaka ya 90 mabasi yalikuwa yakisafiri usiku? Ngorika, Lang'ata kutoka Arusha kuja Dar, tena barabara ilikuwa mbaya maeneo mengine. Pale Mbwewe tulikuwa kunapiga sana vyuku... Iringa, Mbeya kulikuwa na Zainabu bus, Scandinavia etc... Songea kulikuwa na Kiswere nk.. Yote yalikuwa yakipiga ruti za usiku. Sasa tunaenda mbele au tunarudi nyuma?? Hatuwezi kuingia uchumi wa juu ikiwa watu hawawezi kufanya kazi usiku, eti hakuna kusafiri usiku na asubuhi Bus zinapangiwa wote waanze saa 12 wakimbizane njia nzima, haya mambo ya kiwaki sana aisee daaah.
Yes, hakika umeeleza vyema?Uchumi utachangamka saa 24.
Vituo vya mafuta watauza saa 24,wausau chakula watauza saa24.wenye mabasi watasafirisha abiria mara 2 zaidi.
Uchumi utakuwa angalau mara 2,mchana na usiku ni kuendelea kulijenga taifa.
Miji itasafishwa mchana na usiku.
Ajira itaongezeka mara 2, wenye viwanda watafanya kazi usiku na mchana.
Mchana wapuuzi wengi wanasumbua kusimamishana hovyonilishaacha kusafiri.mchana bila sababu ya msingi,safari kwangu ni usiku,mchana kwangu ni dharura
Akili za polisi utaziweza? Sasa zikutane na za wanaccm wenye uchu wa madaraka na kupenda sifa wasizonazo wala wasizozistahilu, hapo unategemea nini?Ewaaaaaaa Majinja alikua anaanzia Lindi nadhani, Dar then Mbeya pia alikuepo Rungwe na Osaka au Chakito kama sijakosea, akaja Dar Express au Kilimanjaro wote hawa wamezuiliwa ila coaster zinaruhusiwa...sasa hizi ni akili au matope?!
Ukiwa unasafiri fungua kioo cha dirisha tazama nje,vuta hewa ya nje hiyo ndiyo dawa ya kuzuia kutapika.Mimi hiyo ndiyo dawa yangu siku hizi sitapiki tena.Kweli kabisa, mimi nikisafiri hua natapika sasa hua nalala ili kuzuia hiyo hali. Safari ikiwa usiku ni raha mana ntakuja na net kabisa na dawa ya kuua mbu.
Kwa muda mrefu nilitaka kuandika hili la Sababu za "kitoto" za kuzuia magari yasisafiri usiku, hatimae Mbunge Tulia ameliona Hilo, tusubiri mamlaka zitekeleze. Mimi ni mdau wa safari za usiku sana, kwahio Wacha niwape experience....
1. Zile Coaster za Arusha zinazuiliwa pale Mkata wa saa Tano, matokeo yake, mkifika pale mnachangishana gari inaongeza wese mnazungukia Handeni, hii ni hatari.
2. Pale pale Mkata Kuna uchochoro, kwahio Dereva anazima Taa mnapita kwenye huo uchochoro kwenye makazi ya Watu, risk inazidi kuongezeka. Unajiuliza, hivi barabara ya Dar to Arusha Ina hatari Gani Hadi hizi gari zizuiliwe kama sio kutengeneza mazingira ya Rushwa tu?
3. Coaster za Dar to Mbeyaz wakifika Moro waliweka Picha ya Marehemu kuwa wanasafirisha msiba...tunajua kilichotokea, laiti ingekua ni route Hali.
4. Hivi kuna umuhimu Gani wa mabasi yote kuanza kufukuzana Pale stand kuu saa 12 asubuhi? Mfano, basi linalokwenda Kigoma, Kasulu, Musoma, n.k kwanini wasiondoke saa tatu asubuhi? Au saa Nne? Ili wasilale? Maana madereva ni wawili wawili, sasa watakimbizana kutwa nzima then watalala Kaliua saa nne usiku Hadi saa 12 asubuhi
5. Hivi kwanini Mabasi ya Bukoba, Ngara, Burundi, nk walazimishwe kulala Kahama na sio Nyakanazi? Siku hizi eneo lote liko salama.
6. Kwanini Mamlaka husika wasiruhu mabasi ambayo madereva wake na mabasi Yao yanatambulika kuliko hii ya kukata Kibali Cha Coaster Kila baada ya muda? Hatuna uhakika wa zile Coaster Wala madereva wake....
Inaendelea..
HahahaUsafiri wa ndege ni bora sana sababu kubwa ni kuwa hauna vizingiti vya wapumbavu wote.
Hahaha 😂 ila kweli kabisa aiseeeeAkili za polisi utaziweza? Sasa zikutane na za wanaccm wenye uchu wa madaraka na kupenda sifa wasizonazo wala wasizozistahilu, hapo unategemea nini?