Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Like seriously??
Kama mchana ajali ndio hivyo vipi ikiwa usiku??, jiulize ni kwanini imepigwa marufuku kusafiri usiku na je sababu ya katazo hilo imeondoka??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Like seriously??
Umewahi kusafiri Usiku??Kama mchana ajali ndio hivyo vipi ikiwa usiku??, jiulize ni kwanini imepigwa marufuku kusafiri usiku na je sababu ya katazo hilo imeondoka??
Bonge la summary, shukrani sana Sana! Eti muda huu Tanzania tumelala, huwezi kusafiri Usiku huu kwenda Tanga au hata hapo Moro, ukifika Stand mabasi yamepaki...... utadhani tuna utajiri uliopindukiaNi lazima tukubali kuwa Tanzania imeishafunguka ki nchi na kimataifa. Wananchi lazima wasafiri muda wowote bila kujali usiku au mchana.Uwe usafiri wa anga au Barabara au majini au reli.Usafiri wote uko huru ila Barabara.Vikwazo vinavyokwaza barabarani ni ni kama ifuatavyo:-
1.Ujambazi wa kuteka magari - Tatizo hili ni la duniani kote . Vyombo vya Ulinzi na Usalama ni kazi Yao . Tanzania haiwezi kusalimu amri kwa majambazi
2. Ratiba za magari zitapanuka - Kufukuzana barabarani kutaisha manake hakuna haja kwa nini ukimbize wakati utatembea usiku kucha
3. Mwendo wa 50 km kwa saa iondolewe usogezwe uwe 100 km kwa saa kwa kuwa Barabara zote safi na salama.Mkazo uwe kwenye vivuko tu.
4. Tanroads/Tarura buni utaratibu wa kuweka taa za solar maeneo yote korofi ikiwezekana unganisha mkoa kwa mkoa inawezekana
5. Serikali ibuni utaratibu wa kurasimisha coasters zibebe watu badala ya kubeba watu kwa visingizio km misiba au harusi nk
Hahaaaaa umeshaona fursa hapo sio! Muda huu uko kwenye Luxury Bus mnatoka Mbezi mnaitafuta Dodomaluxury buses mziki nene, Wafu waliwa kimasihara
Wala sio suala la kuwa pessimistic. Ni kweli anavyosema. Madereva wa bongo hawajitambui kabisa. Kutakuwa na over speeding sana. Wenzetu wa magharibi ni watiifu wa sheria. Kama speed inayotakiwa ni 80km/h watamaintain hiyo, kwa wabongo hapana aisee.Mbona unakuwa so pessimistic? Kwa nini ufikiri au uamini ni mabaya tu yatatokea?
Big point broo hilihalizuiliki wakati huu,mi mwenyewe nimdau mkubwa wa safari za usiku.
Umewahi kusafiri Usiku??
NDIO maana ukachangia hivo, nilikua sahihi kukuuliza Kumbe! Basi kama hujawahi kusafiri Usiku hii thread sio level Yako, soma tu maoniSijawahi na wala sitaki, katika nchi hii kusafiri usiku kama Wachawi ni risky kubwa.
Una umri Gani?Nyie mnataka shughuli zenu za ujambazi zirahisishwe
Sijui hizi akili za kijinga hivi mnazitoaga wapi, hivi hujui kuwa Kuna mabasi baadhi yanasafiri Usiku? Ile Ajali ya basi la Arusha juzi ilitokea usiku???Wala sio suala la kuwa pessimistic. Ni kweli anavyosema. Madereva wa bongo hawajitambui kabisa. Kutakuwa na over speeding sana. Wenzetu wa magharibi ni watiifu wa sheria. Kama speed inayotakiwa ni 80km/h watamaintain hiyo, kwa wabongo hapana aisee.
Tamu kama mke wa mjumbeSafar za usiku hapana .
Huna unalolielewa wewe. Nakuona juha tu fulani unaetaka kulazimisha ujuaji. Una mandate gani ya kushangaa akili zangu wewe juha? Tunakueleza kutokana na uzoefu wa huko nyuma halafu wewe unakuja kutukana hapa. Sasa hakuna cha safari za usiku, ukitaka jinyonge.Sijui hizi akili za kijinga hivi mnazitoaga wapi, hivi hujui kuwa Kuna mabasi baadhi yanasafiri Usiku? Ile Ajali ya basi la Arusha juzi ilitokea usiku???
Hahahahahahahaaaaaa ACHA bangeHuna unalolielewa wewe. Nakuona juha tu fulani unaetaka kulazimisha ujuaji. Una mandate gani ya kushangaa akili zangu wewe juha? Tunakueleza kutokana na uzoefu wa huko nyuma halafu wewe unakuja kutukana hapa. Sasa hakuna cha safari za usiku, ukitaka jinyonge.
mbingi utaisikia tu😂Hahaaaaa umeshaona fursa hapo sio! Muda huu uko kwenye Luxury Bus mnatoka Mbezi mnaitafuta Dodoma
Ungewahi kutekwa na kuvuliwa nguo mbele ya mkeo, watoto, wakwe na kupigwa hili wazo usingelipigia chapuo. Labda yawepo mabasi yanayosafiri usiku na ya mchana ili kila abiria ajichagulie muda wake wa safari.Kwa muda mrefu nilitaka kuandika hili la Sababu za "kitoto" za kuzuia magari yasisafiri usiku, hatimae Mbunge Tulia ameliona Hilo, tusubiri mamlaka zitekeleze. Mimi ni mdau wa safari za usiku sana, kwahio Wacha niwape experience....
1. Zile Coaster za Arusha zinazuiliwa pale Mkata wa saa Tano, matokeo yake, mkifika pale mnachangishana gari inaongeza wese mnazungukia Handeni, hii ni hatari.
2. Pale pale Mkata Kuna uchochoro, kwahio Dereva anazima Taa mnapita kwenye huo uchochoro kwenye makazi ya Watu, risk inazidi kuongezeka. Unajiuliza, hivi barabara ya Dar to Arusha Ina hatari Gani Hadi hizi gari zizuiliwe kama sio kutengeneza mazingira ya Rushwa tu?
3. Coaster za Dar to Mbeyaz wakifika Moro waliweka Picha ya Marehemu kuwa wanasafirisha msiba...tunajua kilichotokea, laiti ingekua ni route Hali.
4. Hivi kuna umuhimu Gani wa mabasi yote kuanza kufukuzana Pale stand kuu saa 12 asubuhi? Mfano, basi linalokwenda Kigoma, Kasulu, Musoma, n.k kwanini wasiondoke saa tatu asubuhi? Au saa Nne? Ili wasilale? Maana madereva ni wawili wawili, sasa watakimbizana kutwa nzima then watalala Kaliua saa nne usiku Hadi saa 12 asubuhi
5. Hivi kwanini Mabasi ya Bukoba, Ngara, Burundi, nk walazimishwe kulala Kahama na sio Nyakanazi? Siku hizi eneo lote liko salama.
6. Kwanini Mamlaka husika wasiruhu mabasi ambayo madereva wake na mabasi Yao yanatambulika kuliko hii ya kukata Kibali Cha Coaster Kila baada ya muda? Hatuna uhakika wa zile Coaster Wala madereva wake....
Inaendelea..
Inaendelea....
Muda huu ninapoandika hili ni 21:45 ukienda pale Mbezi Kituo Cha Daladala au pale Ubungo Kimara Kuna abiria wengi sana, hawa wanakwenda Mbeya, Dodoma, Mwanza na kwingine, huu ni mfano tu lakini situation kama hio utaikuta Dodoma CBE, Singida pale Nje, Makambako, Mbeya, Moro, Mombo-Tanga, na kwingine.....
Hawa wote wana-risk maisha Yao, kwanini tusiukubali ukweli kuwa route za usiku haziepukiki? Tuhalalishe hizi safari tupunguze ajali za magari ya IT na zile za magazeti, mfano, ndani ya miezi 36 MAGARI ya magazeti yameondoka na maisha ya watu wasiopungua Kumi, coaster za Usiku zimeondoka na maisha mengi the same to IT na Malori. Tukihalalisha tutapunguza tatizo
=====
“SERIKALI IRUHUSU MAGARI YA ABIRIA KUSAFIRI WAKATI WOTE HADI USIKU”- DKT. TULIA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameitaka Serikali kuangalia upya utaratibu uliowekwa katika baadhi ya maeneo nchini wa kuyazuia magari ya abiria kufanya shughuli za usafirishaji nyakati za usiku kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi.
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Novemba 10, 2022 wakati aliposhiriki Semina kwa Wabunge kuhusu usalama Barabarani iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Amesema kuwa ni lazima ifike wakati sasa Wananchi waweze kufanya shughuli zao muda wote na kuondoa dhana iliyozoeleka ya magari ya abiria kuwekewa vikwazo vya kufanya kazi kwa sababu zizisokuwa rasmi wakati magari mengine yakiwemo ya mizigo yanaruhusiwa.
“Kunashida gani ya kuzuia gari ya abiria kusafiri usiku? Tunatamani nchi yetu kuchangamka Zaidi kiuchumi sasa kwanini magari haya yawe na zuio wakati magari mengine yanaruhusiwa kusafiri hadi usiku. Kama ni changamoto ya miundombinu basi ishughulikiwe na shughuli zifanyike” amesisitiza Dkt. Tulia
View attachment 2416034
Nadhani umejifunza. Na usidhani wewe peke yako ndiye mwenye hati miliki ya kutukana watu. Ukiona hoja imekuelemea au hukubaliani nayo pita kimya. Watu tumeumbwa na mitizamo tofauti, sasa ukilazimisha sote tufikiri kama wewe, unaonekana kituko tu.Hahahahahahahaaaaaa ACHA bange