Kwahili la Mabasi kusafiri Usiku, nampongeza Mbunge Tulia Ackson

Kwahili la Mabasi kusafiri Usiku, nampongeza Mbunge Tulia Ackson

Nadhani umejifunza. Na usidhani wewe peke yako ndiye mwenye hati miliki ya kutukana watu. Ukiona hoja imekuelemea au hukubaliani nayo pita kimya. Watu tumeumbwa na mitizamo tofauti, sasa ukilazimisha sote tufikiri kama wewe, unaonekana kituko tu.
Wapi nimelazimisha? Au unataka ligi? Sipo kwa mood hio
 
Ungewahi kutekwa na kuvuliwa nguo mbele ya mkeo, watoto, wakwe na kupigwa hili wazo usingelipigia chapuo. Labda yawepo mabasi yanayosafiri usiku na ya mchana ili kila abiria ajichagulie muda wake wa safari.
Aiseeee
 
Hilo punguani linalilia safari za usiku haya ndio majambazi
Huna unalolielewa wewe. Nakuona juha tu fulani unaetaka kulazimisha ujuaji. Una mandate gani ya kushangaa akili zangu wewe juha? Tunakueleza kutokana na uzoefu wa huko nyuma halafu wewe unakuja kutukana hapa. Sasa hakuna cha safari za usiku, ukitaka jinyonge.
 
Gari za abiria kuruhusiwa kutembea usiku itakuwa sababu kuu ya ajali...

Kama wanataka huo utaratibu barabara ziwe mbili au zaidi kwenda na kurudi...

Wenye uzoefu wa kuendesha usiku watakuwa wanajua hatari za barabarani ambazo sababu kubwa ni uwepo wa giza, mfano kukutana na gari mbovu isiyoweka taa za tahadhari, wakulima wa alfajiri wanaoingia njia kuu hovyo na matrekta yasiyo na taa, usiku magari binafsi yanakimbia mno n.k
 
Night ndo mpango mzima Kwangu kutwa nzima kazi kazi jioni safari Dar Mwz masaa 10 Nairobi Mwz masaa 10 Musoma Makambako masaa 16 hakuna kero yo yote usiku hata Kama una makosa hakuna anakuhoji speed Kama zote raha sana night
 
Wapi nimelazimisha? Au unataka ligi? Sipo kwa mood hio
Unalazimisha kwa kutukana akili za wenzako kisa tu wana mtazamo tofauti nawe. Kasome comment namba 105 ukatukane tena.
 
Night ndo mpango mzima Kwangu kutwa nzima kazi kazi jioni safari Dar Mwz masaa 10 Nairobi Mwz masaa 10 Musoma Makambako masaa 16 hakuna kero yo yote usiku hata Kama una makosa hakuna anakuhoji speed Kama zote raha sana night
Ewaaaaaaa
 
Umeeleza vizuri sana na kweli wewe ni mdau wa safari, mabasi ya Kigoma, kasulu kulazwa kaliua ni kuonea abiria, kipande kile kama kuna shida ya usalama ni askari wajipange wakiwa na silaha, ina maana kila basi waingie askari wawili tu , hao walipwe posho zao kesi imeisha, haya kipande cha kahama nyakanazi nako kuwe na patrol ya maana, na escort ya magari nzuri maana kamanda Tosi alipambana na ujambazi wa pale hadi wakapotea wote, unapolaza watu kahama unaathiri mambo mengi kwa abiria japo wewe utafurahi kutengeneza pesa, ilitakiwa watu wakapumzike hata biharamuro ili mapema saa tatu watu wako Bukoba, mutukula saa nne na nusu,
 
Dada yupo sawa azungumzie na kupunguza kodi kwenye magari ili watu waagize magari bora kupunguza ajali...

Zambia, Botswana, zimbabwe, Swaziland, Namibia, Msumbiji, DRC , Angola, na Baba lao SA. Wewe bahati ushafika kote huko umevuruga hivi ukiona vyuma wanavyokokota barabarani unaweza kudhani sisi ndio hatuna bandari
 
Halafu hua kodi za Tanzania maajabu matupu Haiwezekani Rwanda simu iwe bei rahisi kuliko Tanzania yaani watu wanatoka Tanzania kwenda Rwanda kununua simu bei rahisi tena hawana habari ya fake hadi tunatia huruma
 
Utaratibu wa kutoka malawi au zambia unafika uyole saa nane unakuta basi lipo unatembea usiku unafika asubuhi mjini unaunganisha kwenye shughuli zako mapema unamaliza unawahi kibo kugeuza na basi la saa nane mchana alfajiri yake uko mbeya unaanza kufanya mengine urudishwe haraka huwezi kukuza uchumi kwa kupata muda wa kulala hovyo kila siku,
 
Mwanza nao wastuke usafiri uwepo muda wote haiwezekani jiji kama lile eti saa tano usafiri wa Dar haupati tena wana advantage hawalazwi njiani kama wenzao wa kigoma, kagera
 
Hatari zipo ila zimepoa tu, ngoja route zianze hutoamini mabadiliko yatakayotokea hadi waporaji wa usiku watarudi.
 
Viongozi acheni kutoa matamko ambayo baadae yataleta majuto makubwa kwa taifa.

Mabasi kusafiri usiku hayakuanza leo wala Jana.
Tangu miaka ya zamani basi yote yalikuwa yanasafiri masaa 24/7.

Je nini kilipelekea mabasi kukatazwa kutembea usiku?
--1.. Ajali zilikuwa nyingi sababu uzembe wa usiku ni mkubwa sn Kwa madereva barabarani.
-- 1..Usalama wa abiria na Mali zao kwenye baadhi ya mikoa.

Je kabla ya kuruhusu hilo la kutembea usiku kucha serikali imejipangaje kudhibiti hilo?
Wakati trafick police saa 6 o'clock hawapo barabarani?

Hivi kama mchana ambapo dereva anaona vizuri kabisa anasababisha ajali,
Hivi usiku itakuwaje?

Inchi ya hovyo sn hii..
 
Barabara zetu ni mbovumbovu, Labda kama wanataka tupunguzwe. Siungi mkono hoja ya kimauaji kama hiyo.
 
Back
Top Bottom