Kwahili la Mabasi kusafiri Usiku, nampongeza Mbunge Tulia Ackson

Kwahili la Mabasi kusafiri Usiku, nampongeza Mbunge Tulia Ackson

Mbona unakuwa so pessimistic? Kwa nini ufikiri au uamini ni mabaya tu yatatokea?
Kwa kweli mkuu nami huwashangaa sana watu wa hivi. Na ikitokea mtu wa hivi akapewa madaraka na fursa ya kufanya maamuzi basi ujue mtarudi kwenye ujima, they don't like changes and always they think of negativity.
 
Safari za usiku zilikuwepo katika nchi yetu Tanzania.Nakumbuka miaka ya 1986 tulisafiri sana kutoka Dodoma KWENDA Dsm.Tuliondoka saa mbili usiku Dodoma na kufika Dsm saa kumi na mbili asub.Safari hizo zilizuiliwa Mwaka 1992 na wazir mkuu wa Wakati huo Dr John Samuel Malechela baada ya ajali mbaya ya basi ,ambalo silikumbuki na kuwaua watu wengi sana.Sababu ya ajali ilielezwa kuwa ni kutokana na dereva kushindwa kuona vizuri.Kwa upande wangu mm nafikiri mheshimiwa spika wa Bunge kabla hajashauri kuhusu hizo safari angeangalia emprical review .Yaan nn kilisababisha zikazuiliwa.Je hizo sababu bado zipo?Je ajali tu za mchana zimepungua?Mm naona sababu za ajali za usiku kwa Sasa ni nyingi sana kuliko Mwaka huo 1992.Kwa Sasa Kuna malori yanayofeli breki mengi sana barabarani.Tutegemea vifo vingi vya Watanzania.Kama mchana tu malori yanafeli breki,usiku ndio vifo vitakuwa vingi sana.
Hayo ni mawazo yako tuu, na siyo lazima ya reflect ukweli wowote. Spika aliwahoji maofisa wa polisi kwenye kile kikao je mna any scientific evidence ya hilo zuio? Wao kimyaaa, mbona gari za maiti zinasafiri usiku? Wao kimyaa. In short wamekariri tuu na hata huo mwaka 1992 waziri mkuu alivyozuia it was mihemko tuu ya wanasiasa ya kutoa matamko kupata political millage kwa sababu ilitakiwa ufanyike utafiti kabisa wa kitaalamu kabla ya kuweka zuio.
 
Umesema vyema sana ila Kwa sasa 2022 na 1992 utakubaliana na Mimi kuwa Hali ni tofauti, sababu kubwa haikua barabara tu ila ni Ulinzi na usalama kutokana na mapori makubwa ila Kwa sasa, kwa mfano Kahama to Nyakanazi ya 1992 sio Kahama to Nyakanazi ya 2022, Eneo kubwa limejengwa na Eneo lote ni lami , sasa Kuna sababu Gani magari ya Bukoba kwa mfano, yalazimishwe kulala Kahama na sio Nyakanazi? Huu ni mfano.,..
Pia uhitaji wa abiria kusafiri Usiku umekua mkubwa sana, je tuwaache waendelee kudandia Malori na magari ambayo sio official kubebea abiria au tu-officialize?

Kumbuka, Kwa sasa, mabasi yapo yanayofika Dar asubuhi au Usiku wa manane kama Yale ya Kutoka Kigoma, Kasulu, Bukoba, Karagwe na Katavi, au Yale ya Mbeya to Mwanza, wanafika alfajiri, point Yangu ni kwamba hizi route ziruhusiwe, hazina madhara kama hayo makubwa kiasi hicho kikubwa madereva wawepo wawili kama wale wa Songea to Mwanza ambao hufika siku inayofuata......
Well said... Kingine kwa nini wasiende kujifunza kwa nchi nyingine ambako usafiri wa usiku ni kawaida kabisa?
 
Ndio, Kwa sasa ni Kigoma tu ndio Ina changamoto
Kipande kidogo sana kimebaki maybe 150 km majuzi nilipanda nice bus, nimesahau jina, yaani full kipupwe mpaka tukafika, ila tukalala sijui ni Kaliua pale kama sijakisea.
 
Uchumi utachangamka saa 24.
Vituo vya mafuta watauza saa 24,wausau chakula watauza saa24.wenye mabasi watasafirisha abiria mara 2 zaidi.

Uchumi utakuwa angalau mara 2,mchana na usiku ni kuendelea kulijenga taifa.

Miji itasafishwa mchana na usiku.
Ajira itaongezeka mara 2, wenye viwanda watafanya kazi usiku na mchana.
Na haya ndiyo maendeleo 24 hours watu wanafanya kazi...
 
Kwa madereva watanzania hawa gari kutembea usiku ni hatari

Wengi walevi na hawapati muda wa kulala
Kukiwa na options za bus za usiku na mchana nyie waoga wa kupanda Bus za usiku si mtapanda za mchana?? Tatizo liko wapi? Mbona kuna watu wanapanda mpaka gari za usiku za magazeti na coaster? Ninachosema ni kwamba tuache kupangiana maisha...
 
Hatari zipo nyingi

Ilishawahi kutokea saa sita usiku dereva akasinzia kwenye usukani gari iliacha njia
Mungu saidia ilikuwa tambarare
Tupe statistics kwamba ajali ngapi kwa mwaka kwa usiku ukilinganisha na mchana? Tuongee kwa data, na kwa nini wasiwepe chuo cha taifa cha usafirishaji na UDSM watufanyie tafiti na kuja na majibu based on research??
 
Kabisa zamani barabara mbaya sana lakini magari yalikuwa safari za usiku. Mimi nadhani turudi kwenye zilezile sababu walizotoa kuzuia safari za usiku na tuziangalie je bado zina mashiko? kama hakuna basi kuwe na uhuru watu kupanga safari zao kwa mujibu wa matakwa yao na chagua la abiria. Nakumbuka wakati ule kulitokea ajali usiku basi wakaamka asubuhi marufuku kutembea usiku lakini kwani ajali ngapi zimetokea baada ya hapo, nyingi tu. Baya zaidi unasema mwisho saa 5 usiku sasa kuna tofauti gani saa moja usiku mpaka saa 5 na kuanzia saa 5 mpaka asubuhi? Mimi nadhani tuache mambo ya kucopy na kupaste mambo yamebadilika uchumi uko speed tuache biashara zifanywe kwa matakwa ya walaji wako watapenda usiku na wako watapenda mchana. Hili ni kama lile la kuzuia mirungi wakati haina shida yoyote ni starehe kama starehe zingine, unaacha pombe za kienyeji unazuia mirungi😛
Umeongea vema mkuuu.. Mimi katika vitu ambavyo nimemkubali spika ni hili la kukemea hili zuio la kijinga kabisa la bus zisisafiri usiku.
 
Mimi kwa Safari za usiku labda kwa sharti moja kubwa Tuu wanaondesha mabasi usiku lazima umri wao uwe kuazia miaka50 kwenda Juu ili Dreva awe na nidhamu kubwa usiku
Mkiwapatia awa madreva vijana kumbukeni hili ni muhimu sana
Utachagua bus za mchana, hakuna wa kukulazimisha... Hata sasa hivi kuna choices mbalimbali, bus la kawaida, semi luxury, super luxury lenye mpaka choo ndani nk it's your choice..
 
Acheni kufananisha miaka hiyo sasa kwa sasa vyombo vya usafiri vipi vingi sana
Malori ni mengi sana pengine karibu mara 1000 na yaliyokuwepo miaka ya 1990

Nasisitiza tuacheni Siasa kwenye hili lazima tuwe na mikakati muhimu

Mchana tuu basi linagongana na Lori uso kwa uso acheni hayo mambo
Sasa huko nchi zingine za Africa, hata jirani zetu Kenya tuu hapo wanasafiri usiku. Nyie huo uzoefu mnautolea wapi?
 
Kwa muda mrefu nilitaka kuandika hili la Sababu za "kitoto" za kuzuia magari yasisafiri usiku, hatimae Mbunge Tulia ameliona Hilo, tusubiri mamlaka zitekeleze. Mimi ni mdau wa safari za usiku sana, kwahio Wacha niwape experience....
1. Zile Coaster za Arusha zinazuiliwa pale Mkata wa saa Tano, matokeo yake, mkifika pale mnachangishana gari inaongeza wese mnazungukia Handeni, hii ni hatari.
2. Pale pale Mkata Kuna uchochoro, kwahio Dereva anazima Taa mnapita kwenye huo uchochoro kwenye makazi ya Watu, risk inazidi kuongezeka. Unajiuliza, hivi barabara ya Dar to Arusha Ina hatari Gani Hadi hizi gari zizuiliwe kama sio kutengeneza mazingira ya Rushwa tu?
3. Coaster za Dar to Mbeyaz wakifika Moro waliweka Picha ya Marehemu kuwa wanasafirisha msiba...tunajua kilichotokea, laiti ingekua ni route Hali.
4. Hivi kuna umuhimu Gani wa mabasi yote kuanza kufukuzana Pale stand kuu saa 12 asubuhi? Mfano, basi linalokwenda Kigoma, Kasulu, Musoma, n.k kwanini wasiondoke saa tatu asubuhi? Au saa Nne? Ili wasilale? Maana madereva ni wawili wawili, sasa watakimbizana kutwa nzima then watalala Kaliua saa nne usiku Hadi saa 12 asubuhi
5. Hivi kwanini Mabasi ya Bukoba, Ngara, Burundi, nk walazimishwe kulala Kahama na sio Nyakanazi? Siku hizi eneo lote liko salama.
6. Kwanini Mamlaka husika wasiruhu mabasi ambayo madereva wake na mabasi Yao yanatambulika kuliko hii ya kukata Kibali Cha Coaster Kila baada ya muda? Hatuna uhakika wa zile Coaster Wala madereva wake....

Inaendelea..

Inaendelea....

Muda huu ninapoandika hili ni 21:45 ukienda pale Mbezi Kituo Cha Daladala au pale Ubungo Kimara Kuna abiria wengi sana, hawa wanakwenda Mbeya, Dodoma, Mwanza na kwingine, huu ni mfano tu lakini situation kama hio utaikuta Dodoma CBE, Singida pale Nje, Makambako, Mbeya, Moro, Mombo-Tanga, na kwingine.....

Hawa wote wana-risk maisha Yao, kwanini tusiukubali ukweli kuwa route za usiku haziepukiki? Tuhalalishe hizi safari tupunguze ajali za magari ya IT na zile za magazeti, mfano, ndani ya miezi 36 MAGARI ya magazeti yameondoka na maisha ya watu wasiopungua Kumi, coaster za Usiku zimeondoka na maisha mengi the same to IT na Malori. Tukihalalisha tutapunguza tatizo

=====

“SERIKALI IRUHUSU MAGARI YA ABIRIA KUSAFIRI WAKATI WOTE HADI USIKU”- DKT. TULIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameitaka Serikali kuangalia upya utaratibu uliowekwa katika baadhi ya maeneo nchini wa kuyazuia magari ya abiria kufanya shughuli za usafirishaji nyakati za usiku kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Novemba 10, 2022 wakati aliposhiriki Semina kwa Wabunge kuhusu usalama Barabarani iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

Amesema kuwa ni lazima ifike wakati sasa Wananchi waweze kufanya shughuli zao muda wote na kuondoa dhana iliyozoeleka ya magari ya abiria kuwekewa vikwazo vya kufanya kazi kwa sababu zizisokuwa rasmi wakati magari mengine yakiwemo ya mizigo yanaruhusiwa.

“Kunashida gani ya kuzuia gari ya abiria kusafiri usiku? Tunatamani nchi yetu kuchangamka Zaidi kiuchumi sasa kwanini magari haya yawe na zuio wakati magari mengine yanaruhusiwa kusafiri hadi usiku. Kama ni changamoto ya miundombinu basi ishughulikiwe na shughuli zifanyike” amesisitiza Dkt. Tulia
View attachment 2416034
Nafikiri nia ya serkali kutoruhusu magari kutembea usiku ilikuwa njema, hasa ukizingatia sababu za kiusalama. Ni kweli nchingi zilizotuzunguka magari yanatembea saa zote. Lakini kwetu kimekuwa na matatizo ya kiusalama hasa yale maeneo yaliyopakana na Rwanda, Congo, na Burundi. Pia kwa ile njia ya kati kumekuwa na utekaji mwingi na raia kunyang'anywa kila kitu. Mimi mwenyewe kidogo linipate hili, bahati nzuri tulijulishwa mapema. Hili likiruhusiwa lazima tuangalie utekelezaji wake. Pia kuna hili tatizo la mwenda kasi na ajali. Kama madereva wataendesha kwa kasi na kupata ajali itakuwa kazi kupata msaada. Mara nyingi ajali zikitokea raia huchangamkia mali za majeruhi badala ya uwasaidia. Tujiulize, je tukiruhusu mwendo wa usiku tumejitayarisha vipi kutoa msaada iwapo itabidi.
 
. Pia kuna hili tatizo la mwenda kasi na ajali. Kama madereva wataendesha kwa kasi na kupata ajali itakuwa kazi kupata msaada. Mara nyingi ajali zikitokea raia huchangamkia mali za majeruhi badala ya uwasaidia. Tujiulize, je tukiruhusu mwendo wa usiku tumejitayarisha vipi kutoa msaada iwapo itabidi.
Yaani Tanza-nia peke yetu ndio tunaojua kuendesha speed? Hili hapana, suala la usalama Hilo ni udhaifu wa Jeshi la Polisi ila Kwa sasa maeneo mengi ya nchi Yako salama Baada ya Ujenzi wa barabara, kwa mfano mtu anayekwenda Arusha, anapita Wami (lilikua Eneo hatari) then anafika Mkata unamzuia! Hili nalo tunaliwekaje?
 
Tupe statistics kwamba ajali ngapi kwa mwaka kwa usiku ukilinganisha na mchana? Tuongee kwa data, na kwa nini wasiwepe chuo cha taifa cha usafirishaji na UDSM watufanyie tafiti na kuja na majibu based on research??
Yaani wanaamini kwenye ajali Zaidi kuliko usalama, ni sawa na Mtu aseme "sitaenda kazini/kibaruani Leo mvua inaninyeshea maana nje Kuna wingu". Ndio AKILI za Wabongo Wengi
 
Kilimanjaro waliruhusiwa siku mbili tu nadhani

Nilisafiri kwa raha Jamani, Mara ghafla wakanyimwa kibali

Tukarudi kwenye coaster zetu zilizojaa usumbufu na pia ni very uncomfortable.

Serikali iachilie mabus yasafiri usiku tu Manake Kama ni ajali hata mchana zipo Za kutosha.
 
Back
Top Bottom