Mbona mna maswali ya kipimbi sanaa? Hivi mnajua miaka ya 90 mabasi yalikuwa yakisafiri usiku? Ngorika, Lang'ata kutoka Arusha kuja Dar, tena barabara ilikuwa mbaya maeneo mengine. Pale Mbwewe tulikuwa kunapiga sana vyuku... Iringa, Mbeya kulikuwa na Zainabu bus, Scandinavia etc... Songea kulikuwa na Kiswere nk.. Yote yalikuwa yakipiga ruti za usiku. Sasa tunaenda mbele au tunarudi nyuma?? Hatuwezi kuingia uchumi wa juu ikiwa watu hawawezi kufanya kazi usiku, eti hakuna kusafiri usiku na asubuhi Bus zinapangiwa wote waanze saa 12 wakimbizane njia nzima, haya mambo ya kiwaki sana aisee daaah.