Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!


Unapenda kula sana eeh?

Soma bandiko kuelewa. Umesoma vizuri kilicho andikwa? Kama hukuona pako hivi:

"Gharama za kuwaweka watu manyumbani salama wasife kwa njaa (peke yake) tu ni ndogo mno na zitazidi kupanda kadri siku zinavyopita."

Ni kuonyesha umbumbu kuliko pitiliza kujaribu kunukuu andiko aliloandika mtu kindivyo sivyo kwa malengo au maslahi yako binafsi.

Nukuu yako ya kimbumbumbu uliitoa wapi mkuu?
 
Uzuri wake muh Rais hajamuzuia mtu yeyote kujiweka karantini, wanaoamini kuwa maamuzi yaliyofanywa na muhe Rais hayako sahihi wanahaki ya kujiweka karantini wenyewe kwa uhuru wao.

Na sisi wengine tunaokubaliana na maamuzi ya Rais ya kumtegemea Mungu katika janga hili la corona tuachwe tuendelee na uhuru wetu na haki yetu ya kuamini kuwa muhe Rais yuko sahihi katika hili.

Nakama Mungu atatuacha tuangamie kwa corona kwa sababu ya kumtegemea yeye tutakuwa na hoja ya kumuhoji ni kwa nini alituacha tuangamizwe na corona wakati ametuahidi kutuponya na kutulinda tutakapo mugeukia na kumulilia yeye?.
 

Mkuu tatizo letu watanzania ikiwamo wewe ni kutokusoma kujua nini tayari kimeshaongelewa. Matokeo yake yanakuwa mtu unakuja sasa kama umetokea sayari nyingine.

Mkuu uliwahi kuyaona haya:



Hoja za wanaoona lockdown haifai ni zipi? Tuelimishane - JamiiForums

Au ndiyo unayaona leo mkuu?

Hatuwezi kujipanga kama taifa watu wasife njaa tuutokomeze huu ugonjwa?

Mbona Kenya, Uganda na Rwanda wanaweza hali hapo wengine hohehahe kuliko sisi?
 
Dunia nzima wanazungumzia corona na kuita janga na tunaona huko ulaya wakipukutika ila wewe unasema Tanzania ugonjwa umeingia kwa sababu ya uzembe! Wakati nasikia Russia aliwahi mapema kufunga mipaka yake ila hadi sasa washapukutika watu mia tatu na hali inazidi. Sioni tofauti ya aliyefanya uzembe na siyefanya uzembe. Na kama ni uzembe basi huoni kuwa tulitakiwa afrika tuwe tumepukutika zaidi ya Marekani au Italy hadi sasa?
 

Mkuu haipo sababu sana ya kutafuta mchawi na kuacha jambo nyeti kwa sasa la.kuzuia kusambaa zaidi kwa maambukizi. Hata hivyo, historia ya ugonjwa kuingia inajulikana na hata mwendelezo wa unavyosambaa sasa hivi ninavyoandika hapa inajulikana.

Miito mingapi kutaka ndege zisije kwetu kabla ya ugonjwa kuingia ilikuwapo? Hujasikia waliokuwa wamekataa kufunga anga au kuuzuia ndege tokea china kuja? Hukusikia waliokuwa wakiongelea utalii?

Mada kama hizi je nazo hukuziona?

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums

Kwamba ulaya au marekani ugonjwa uliingia hakuhalalishi kutokuwepo uzembe uliopelekea ugonjwa huu kuingia kwetu.

Kumbuka tulisikia na kuona ugonjwa ukiingia mataifa mengine baada ya China yakiwamo ulaya na marekani mapema mno kabla ya ugonjwa kutufikia. Tulikuwa na muda wote wa kujifunza na kuchukua hatua na bado hatukufanya hivyo.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi. Tumejifunza nini au kwa nani kuhusu huu ugonjwa? Nini tumefanya kufuatia kujifunza huko?

Labda niwe wazi zaidi hili la sala tumejifunza kwa nani?

Tumeshindwa kujifunza hili la hata tokea kwa baba askofu wetu Niwemugizi hapa hapa nchini.

Kama haya yote ndiyo unayasikia sasa utakuwa umewasili tokea sayari nyingine. Haitakuwa bure mkuu.
 

Mkuu uliwahi kuyaona haya:



Uhuru upi usiokuwapo unaouongelea ambao mh. rais kautoa wa kujiweka karantini isiyokuwapo?

Ni kweli hatuelewi au ni mzaha?

Hoja za wanaoona lockdown haifai ni zipi? Tuelimishane - JamiiForums

Hoja zenu ziko wapi?
 

Unakosea kumlaumu Rais kwa hili. Mpaka sasa msimamo na maamuzi yake ni sahihi kabisa na ni ya ki - Mungu

Hakuna mambo ya Lockdown hapa nchini kwetu.

å Kwa kazi ambazo hazihusishi kusanyiko la watu kuanzia 10 na kuendelea, ziendelee kufanyika kama kawaida bila kukosa. Watu wachape kazi!!

å Kila mtu achukue tahadhari zote za kiafya kama zinavyotolewa na wataalamu was afya i.e kunawa mikono, kivaa barakoa, kutotoka ndani na kuepuka safari zisizokuwa na ulazima

å Above all, 2Mambo ya Nyakati.7:14 inatuhusu sote. Suluhu ya haya mambo ni kuacha Dhambi, kujinyenyekesha mbele za Mungu na kuomba toba kwa ajili ya taifa na nchi yetu

Chanzo cha haya yote i.e tauni (corona), mikosi, laana, umasikini, magonjwa ni DHAMBI ama kumuasi Mungu

Tunapoghairi njia zetu ovu na kmgeukia Mungu, atatuponya na kuiponya nchi yetu

Soma pia ISAYA 59:1-2. Hii ndiyo ahadi ya Mungu. Tukimuona hawezi kutusaidia na kukakamaza shingo zetu, hakika tutakufa wote
 

Mkuu haipo hata nchi moja yenye mtazamo kama huu. Hilo tu halitoshi kukupa homa? Mbona majambazi hatuyakabidhi kwa Mungu?

Zipo nchi zilizofanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu kwa jitihada thabiti wakitumia raslimali zao na wengine wao hao wala hawana raslimali nyingi kama sisi. Hili nalo halikupi matumaini? Mbona majambazi tunapambana nayo kwa kutumia raslimali zetu?

Umemsikia au kumfuatilia au kumwelewa baba askofu Niwemugizi?

Mkuu tupo tunaompenda sana mtukufu rais lakini kwa hili aah aaah, kwa hakika hawezi kukwepa lawama za moja kwa moja kwa kutokuwajibika.

Nchi hii haina dini. Wananchi wanazao na wengine hawana. Kimsingi hatuna hata haja ya kujuzana dini hizo. Kumbuka dini hizo bado zinakinzana zenyewe. Twalikabidhi hili kwa Mungu kwa dini ipi?

Mkuu huoni kuwa suala hili la msingi mno tunalifanyia mzaha mkubwa?
 

Mkuu ingekuwa TB au ukimwi self protection ingewezekana. Lakini huu, kwa kasi ya maambukizi yake, ugeni wake (nani ajuaye 100%?), kasi yake ya kuuwa, kwamba siyo airborne per se, nk nk.

Mkuu mbona self protection is actually queueing silently waiting for ones' turn?

 
Ushauri wangu kwa kuwa umekwisha kuenea, serkali isijikite kutoa elimu ya kujikinga tu bali jinsi ya kuhudumia wagonjwa majumbani
 

Kabidhi maombi yako kwa Mungu wa dini unayomwabudu siku zote

Jambazi mtu hawezi kuathiri mfumo wa uendeshaji wa nchi yote. Jambazi anashughulikiwa na watu maalumu wenye jukumu hill

Tauni - Corona huyu ni kitu kingine kabisa. Binadamu kwa NGUVU na AKILI na MAARIFA yake hawezi kushughulika naye na kumshinda huyu adui

Njia pekee ya kumshinda huyu adui, huyu jambazi Corona, ni intervention ya Mungu mwenyewe aliyeumba viumbe wote, mwenye nguvu zote.

Hili limeachiliwa kwa kusudi maalumu na Mungu mwenyewe ili watu wapate kuoona ukuu na utukufu wa Mungu.

Limeachiliwa ili kutenga NGANO na MAKAPI. Ngano ni wale wanaomwabudu Mungu wa PEKEE, na wa KWELI ktk YESU KRISTO. Walio na miungu yao ya uongo, hawatabaki Salama, Corona itawapitia tu na kuwaua kabisa!!

Tazama huko ktk dunia ya kwanza USA, China, UK, Germany, Italy, France, Spain nk ambao ni wababe wenye kiburi cha nguvu za kiuchumi na kijeshi na kiteknolojia, kwa hili wamekwama, ubabe hauja wasaidia kitu. Ndiko wanakokufa kama nzige pamoja na kuchukua hatua unazozipendekeza wewe!!

The choice is whether to say I go to YEHOVA or to the Devil!+)
 
Ushauri wangu kwa kuwa umekwisha kuenea, serkali isijikite kutoa elimu ya kujikinga tu bali jinsi ya kuhudumia wagonjwa majumbani

Mkuu elimu ipi serikali iliyojikita kwa kujikinga mle feri, kwenye masoko, ibada, kwenye usafiri wa umma, nk.

Siyo kuwa tunatwanga maji kwenye kinu?

Muda huu si wa elimu tena. Sasa hivi ni maamuzi magumu. Tumejifikisha hapa mwendo sasa ni wa Rwanda, Uganda au Kenya in that order.

Mkuu anaweza bado kuendelea kutouona ukweli huo.

Kwa hivyo wala asijidanye kwa sasa tumechoka na waziwazi tutamfahamisha kuwa kwa maamuzi yake yasiyo na mashiko kama hayo hatumwuungi mkono.
 
Dar inatakiwa siku nyingi iwe lockdown na Zanzibar lkn hawataki au wanaona wakisema itakuwa aibu kwa sababu walishasema upinzani kabla
Mikusanyiko kama ibada na mambo mengine vilitakiwa visiwepo lkn pia hawataki wanatafuta kura makanisani ugonjwa na wenyewe una wamaliza waumini hii ni vita nyingine
Amebaki Mungu tu kuwatetea na kuwapigania wadanganyika
 
Nimekwambia huko ulaya nchi nyingi watu wanapukutika haijarishi aliyefanya uzembe au asiyefanya ila wewe bado unashikilia habari za uzembe na huko Russia watu 300 washapukutika na wakati wao walifunga mapema tu mipaka yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…