Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

Kwa nini tuna serikali na Rais akiwa mkuu wa nchi!!!? Acha dhana potofu.
 
Mkuu kama unapenda kukaa nyumbani kaa tu nyumbani, hakuna atayekuzuia.
 
Una hoja ya kipumbavu kama ile Polepole ya kupambana na korona kama mnavyopambana na wapinzani!!! Yaani mnatumia ghiliba hata kwenye korona!!!?
 
Kwa nini tuna serikali na Rais akiwa mkuu wa nchi!!!? Acha dhana potofu.

Rais ni kiongozi wa nchi ila hawezi kuwa kila kitu na ndio maana anawekewa wasaidizi hadi wajumbe wa nyumba kumi kwa kila mtaa. Kila mtu ana muhimu kutokana na level yake mkui

Kama kwako Rais ni mtu anaetakiwa kuangalia hadi maslahi ya familia yako bhasi utakuwa useless father/mother..
 
Ndugu, labda una akili ndogo hivyo inakuwiya vigumu kuelewa kinachozungumziwa. Tuko katika Vita vya kupambana na korona, amiri Jeshi mkuu Ni lazima aonyeshe njia ya mapambano. Mimi nitaiongoza familia yangu, lakini hiyo haiondoi uongozi wa kitaifa kuchukua hatua madhubuti
 

Mkuu nilikutonya mapema mchawi kama lazima tumtafute baadaye baada ya kuudhibiti huu ugonjwa. Huuoni umuhimu huo?

Lakini kwa hakika, haya hapa chini yalijulikana mapema na kabla sana na ugonjwa usingeingia kama yangezingatiwa:

1. Funga mipaka.
2. Zuia ndege na wasafiri toka nchi zilizo athirika.
3. Weka quarantine wageni wote wanaotaka kuingia nchini toka nje kwa siku 14.
4. Nk nk

Majibu toka serikalini nani hayakumbuki? Nani hajui nani alisema nini? Au unataka tukukumbushe Prof Kabudi alisema nini?

Mkuu kuiandika upya historia ya kilichotokea siyo rahisi sana.

Ni kwa sababu hizo hizo mh. rais angejitathmini sana hasa hapa tulipo. Kwa maana anajielekeza kuliko na lawama kubwa zaidi. Kwa hakika historia itakuwapo hai mno kumhukumu.
 
Mkuu umejikita kwenye lawama nani alikosea wakati mie nakueleza jinsi uhalisia wa hali ilivyo kuhusu huu ugonjwa, kwani huko kote ulaya palipo athirika na corona hakukuwa na washauri kama wewe au ndiyo walishauriwa ila hawakufuata ushauri ndio maana corona ikaingia? Hao warusi walifunga mipaka kama mlivyoshauri kwa Tanzania ila bado hali mbaya sasa huko.
 
lockdown haiepukiki, inaweza kuwa sasa au baadae lakini ili ugonjwa uishe hapa nchini itabidi tujifungie ndani tu ndio njia inayotumika kama kweli tunataka tuumalize huu ugonjwa. Labda kama kuna mtu anayejua njia nyingine yakumaliza gonjwa hili aje atuambie
 
Kuna haja kweli ya kuhamasisha mikusanyiko kipindi hiki misikitini, makanisani na hata huko kunakoitwa makazini ??!!.

Kuna shindikana nini Dar na Zanzibari kuwekewa vizuizi ili ugonjwa usienee nchi nzima ??!!

Kweli tunazidiwa kiasi hicho na nchi kama Rwanda na Uganda ?! Mbona wameweza wao na maambukizi yao hayana madhara . Pia wanahudumia watu wao . Sisi inashindikana nini ?!

Odhis *
 
Acha ugoro. Huwezi kumuweka lock up mtu asiye na hatia. Lock down ni sawa na lockup.
Kwanza kwa uchumi upi tulionao? Kibaya zaidi hujui tatizo litaisha lini, ni uchizi! Je tatizo likikaa mwaka mzima?
Usikariri njia moja ya kusolve tatizo,
UpUnaakiri timamu sio hadi ushikiwe bakora, jitahidi kuepuka maambukizi either kwakuji- lockdown, kunawa kwa usahihi mara kwa mara au kuvaa barakoa. Itapendeza kama utafanya vyote kwapamoja.
 
Uganda wamefanyaje kwani au hao siyo binadamu?Afya ni muhimu pamoja na hilo la kufuata riziki huko mjini kwa wale ambao hawana ajira
Mleta uzi unapodai lockdowns vile vile dai na mikakati ya kiuchumi kuwasaidia hao mnaotaka wafungiwe ndani!!
Msipokuwa makini njaa, sonona n.k vitaua watu wengi zaidi ya #Covid-19

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point yako ni nini



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunatakiwa kufanya Lockdown sio kwa sababu wengine wanafanya bali kwa sababu ndio njia kuu inayoshauriwa na wataalam wa afya katika kupunguza maambukizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…