Kyenyabasa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2023
- 247
- 715
Rais Samia pokea andiko hili linaloletwa kwako nasi askari wako wa Wizara ya Mambo ya ndani kutoka Magereza, Polisi nk .
Rais tunayo madai yetu ya muda mrefu ambayo kisheria tunastahili kulipwa.
1. Posho za maji na umeme zilipwe moja kwa moja kwenye mishahara yetu moja kwa moja tofauti na sasa ambapo posho hizo zinaliwa na wajanja wachache wizarani na ndani ya majeshi yetu, ifanyike kama inavyonyika JWTZ
2. Posho ya chakula ipandishwe kutoka 10,000 per day Hadi 15,000 per day kwa sababu gharama za maisha zimepanda hasa vyakula kutokana na wakulima kupandisha bei baada ya serikali yako tukufu kuwaruhusu nje ya nchi ili nao wafaidi matunda ya jasho lao, tunaomba posho hiyo iwe 450,000 kwa mwezi.
3. Posho ya pango (ngome) alipwe kila Askari kama ilivyo JWTZ ili Askari warekebishe nyumba chakavu wanazoishi kambini.
Rais madai yetu ni ya muda mrefu sana lakini yamekuwa yanadhibitiwa na viongozi wetu ndani ya majeshi yetu au wizarani kwa manufaa yao wenyewe.
Aidha tunakuomba utuondoe utumishi na utupeleke mfuko maalumu (consolidated fund) maana sheria zetu haziendani na utumishi.
Rais tunajua unayo mambo mengi ya kufanya lakini tunaomba uyaangalie mambo hayo kwa huruma na upendo ili kuboresha maslahi ya Askari wako. Kama unavyoelewa askari hana chama cha kumtetea bali chama chake ni wewe Rais hivyo ndivyo tunavyofundishwaga mafunzoni.
Tunakutakia afya njema mama, bajeti hii tunaomba utufikirie kwa mambo hayo kadhaa tuliyoyaainisha hapo juu.
Tunakusalimu kwa jina la jamhuri tukufu ya muungano wa Tanzania.