Kwako Rais Samia, sisi Askari tunaomba utuongezee maslahi

Kwa hiyo na posho ya chakula mnapewa na mnataka kuongezewa....huo mshahara wenyewe wa kazi gani. Mama samia usiwasikilize hawa, wanatunyanyasa sana huku mtaani.....
 
Kimsingi una hoja.
Ni wakati muafaka Serikali kushughulikia jambo hili kwa kadri ulivyolielezea l.
 
Nadhani magereza wako ICU kabisa,ukikutana nao na uniforms zao na wao utadhani wafungwa kabisa,wako Hoi bora traffic na hawa wengine wanapata vijisent, angalau ni nadhifu kidogo

Jirani yetu ni mkuu magereza mkoa x ila anatabia za kiwaki sana,Ana stress kila siku kutuletea maugomvi.
Mama Samia angalia hawa watu huku mtaani wanatusumbua najua shida ni maisha kuwa magumu
 
Hapo asikali magereza sawa nyiyi wakina polisi mnazo hela nyingi za bule mbona nyiyi ni matajiri tu
 
Jirani yetu ni mkuu magereza mkoa x ila anatabia za kiwaki sana,Ana stress kila siku kutuletea maugomvi.
Mama Samia angalia hawa watu huku mtaani wanatusumbua najua shida ni maisha kuwa magumu
Ni shida sana
 
MAGEREZA WANAISHI NYUMBA ZA BATI PALE UKONGA MAGEREZA . HADI HURUMA WAO WAONGEZEWE ILA ASKARI WA KAWAIDA-BIG NO!!!!
 
wanajitiaga ujuaji tu lakini ni matacle matupu hawana lolote madeni kwa mangi mpaka ya chumvi na viberiti yaani hao jamaa uwaone tu mtaani kujifanya wananyanyasa raia, wakati mwingine ni wivu na frustration ndio vinawasumbua.
 
Mwalimu mwenye miaka 25 kazini na polisi mwenye miaka 25,hawalingania kama mafua na ebola[emoji28][emoji28]

Kikokotoo kitamtoa polisi na 17milion,ila mwalimu na 60mln.
Baada ya miaka 30 ya kazi.
Hilo nilikuwa sifahamu kwa kweli kwani ,kwa sasa basic salary ya police anayeanza kazi ni bei gani.!
 
Ila ni balaa na kikokotoo hujakisema.
Kuna watu wamefanya kazi miaka 30+ na kustaafu kisha pensheni million 12 hadi 15! Hii ni balaa hasa kwa askari hao na
 
Hujui ukisemacho binti mrembo,,,mipaka yetu tunaijua wewe unataka wao walalamike wakati wanaona wanachopewa kinakidhi angalau,,,tulia binti wenye akili wajadili na wenye mamlaka wafanyie kazi,,hakuna nidhamu mbele ya njaa
Nimenda hapo mwishoni, "hakuna nidhamu mbele ya njaa"
Huo ni ukweli kabisa.
 
Mheshiwa Raisi boresha maslahi ya askari magereza hawa wengine. Piga chini kwanza wana laana za watu wanao waonea na rushwa kila kona.
 
Mtoa mada nikupongeze endapo hautakuwa mmoja wapo wa wale wenye tabia za polisi. Katika taifa hili kitengo ambacho ni kiovu kuliko vyote ni polisi. Sijawahi na kamwe sitawahi kuwa na imani na kitengo hiki....
1. Polisi mnadhurumu haki za watu waziwazi
2. Polisi mnalinda wezi ilimradi tu mwizi awe na pesa
3. Polisi mnasumbua sana vijana wa bodaboda
4. Polisi mnalinda maovu ya wana siasa
5. Polisi wakati mwingine inatumika kudhuru na kuwanyima watu haki za kuishi
6. Polisi mnajigeuza miungu watu haswa muwapo ofisini kwenu
7. Polisi ni watu wenye unafiki wa kiwango cha hali ya juu
8. Polisi hamna huruma nyie mnajali tu pesa...
9. Faini zote zinaishia mifukoni mwenu na hapa sijui kwanini serikali isiwasimamie kwenye hili jambo
10. Mwenye pesa iliyozidi kwenu ndiye mshindi
11. Polisi mnatumika kutisha watu badala ya kuwa chombo cha kuleta msawazo
12. Polisi hamna siri, ikitokea mkapewa taarifa labda za kusaidia katika uchunguzi, basi aliyetoa taarifa ajiandae kugeuziwa kibao.
Mbali na uchafu wote huo kuna askari wachache sana ambao wana utu, wanajiheshimu na kufuata miiko ya kazi zao japo ni kwa nadra sana kuwapata. Walimu ndo wa kuonewa huruma lakini si kitengo hiki.
 
Ni kweli hayo yapo lakini huwezi amini Askari polisi ni watu wema wachache wanatia doa
 
Una uchunguuuuuuu 🤣🤣 ndo hao hao wanakulinda na kufanya unakuwa salama kwa muda mwingi. Uchafu wao mwingine ndio amani ya nchi hii
 
Mishahara inaenda kuongezwa so stay tuned
 
Binafsi sijawahi chukia kazi ya mtu ila nachukia tabia ya mtu.
Tabia ya kishetani haifai popote pasipo kujali aina ya wito ama kazi
 
Mlipwe nini nyie ni polisisiem?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…