Kwako Rais Samia, sisi Askari tunaomba utuongezee maslahi

Kuna watumishi wafaa kuongezewa maslahi Ila sio maaskari. Waalimu wanafanya kazi katika mazingira magumu kuliko maaskari polisi. Kuna watumishi wa halmashauri maslahi ni duni sana tena Sana.
 
Tamaa zinawasumbua tu,huo mshahara mnaolipwa na allowance zinawatosha
 
Kuna watumishi wafaa kuongezewa maslahi Ila sio maaskari. Waalimu wanafanya kazi katika mazingira magumu kuliko maaskari polisi. Kuna watumishi wa halmashauri maslahi ni duni sana tena Sana.
Mazingira gani hayo mwalimu hatarishi kumzidi askari?
wenzio wanaenda oparesheni za kuimarisha amani,wanapambana na magaidi/majambazi wakati huo sisi walimu tunakula chaki tu halafu unasema tuna mazingira hatarishi?

Nisiwe mnafiki askari wana njaa mno,maslahi yao ya hovyo.(rejea comment yangu huko nyuma)niliandika jinsi jamaa walivyo na kinyongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja, mpewe tu. Nchi hii kuna wanaokula bila faida Bora mle nyie mnatulinda.
 
Mazingira ya waalimu wengi ni magumu ..maslahi duni bila posho . Katika kuongeza maslahi waalimu ndio ingefaa wafukiriwe Kwanza. Kwanini Kada ya waalimu inadharaulika kwasababu maslahi yao ni duni sana. Nafikiri wewe sio mwl kabisa
 
Ni kweli mkuu.
Mfumo wa Polisi ni mbaya sana Kwa sababu Kada ya juu yaani inamaslahi makubwa yanayomaliza Fungu la Wizara wakati watendaji Wana maisha Duni sana .
Wakati huo huo kada za juu ndiyo inayopanga maslahi ya Polisi. Matokeo yake ni kuwanyima wale wa chini stahiki zao na kujilimbikizia wao ikiwemo kula pesa za rambi rambi,uhamisho ,majanga kazini bila hata kujali.

Lakini pia ubaya wa mfumo wa Polisi ni kuwa mabosi wao ndio wanaopanga nani apate cheo ambacho ndiyo Daraja la kuongezewa Mshahara.
Polisi mwenye Elimu ya form four anaweza akafanya kazi miaka 37 Kwa mshahara wenye Daraja Moja yaani cheo kimoja tuu. Nifumo mbaya sana na wakati huo huo kikokotoo hakijaangalia Bali umefuata mfumo sawa wakati Kada ya Majeshi Ina mifumo tofauti ya ajira na mishahara na stahiki nyingine bila kuwa na Chama Cha kutetea haki zao.
Miaka 37 kama ni Mwalimu au nesi atakua amepanda madaraja mara Kumi na mbili hivyo Mshahara kukaribia Milioni Moja na laki 7 , Wakati polisi atakua anachezea Mshahara usiozidi laki Tano Kwa miaka 37 anastasfu na kiinua mgongo Mili 27[emoji1787].

Afrika wanasiasa wamefanikiwa sana kuwapuuza watumishi wa umma wakiwemo wa vyombo vya Dola ambapo wanacheza na mabosi wa juu kuwatisha wa chini na kuwafukuza kazi Kwa kujiona kuwa ajira wanayotoa Kwa Vijana wa maskini kulinda nchi yao ni huruma yao,hivyo wanapaswa kuridhika na chochote wanacholipwa bila kujali kuwa wao wanapata maposho na maslahi halali na yasiyohalali Kwa kushirikiana na wanasiasa wahuni

Suadani kumechafuka lakini waliochafua nchi ni wale waliokua wanalamba asali ,wanaoumia ni askari ambao wengi ni watoto wa maskini na wenye mishahara Duni . Mabosi wenye mishahara minono wanaficha familia zao Ulaya na Dubai. Maskini wanarushiana risasi Kwa manufaa ya wakubwa na matajiri ambao hawajali maslahi yao wakati wa amani Wala uhai wao wakati wa vita .
 
Hoja zako hazina mashiko.
Mbona gharama za maisha zimepanda kwa wanan hi wote, kwa nini mnataka nyinyi Askari tu ndio muongezewe pisho na mishahara??? Kwa nini usiitake Serikali iimarishe hali za maisha ya wananchi wote kwa kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…