Je wanataka kumpindua Raisi na serikali yake kwa njia za Panya ? Sasa imekuwa si aibu wala siri hili genge linatajwa kila kona na linahusisha viongozi waandamizi ndani ya Chama Cha CCM.
Zinaweza kuwepo njia nyingi za kuipindua Serikali,zile za kizamani huwa hazina nguvu tena,ila hizi za kisasa ambazo tunaziona ni kuidhoofisha Serikali na kuifanya iwe hoi bin taabani ,kwa kuonekana kila inapoziba ufa kunatobolewa kwengine,tunasema kuisaboteji serikali,aidha kwa kutumia walio ndani ya serikali na hata walio inje ya serikali.
Ukienda Bungeni hali si shwari,ukiangalia polisi mambo varange ukiingia serikalini kila mmoja na kauli yake,kuna netiwaki hazipo sawa na zinavuruga kiaina kwa kutumia vichocheo vya hali ya uchumi na kuviza maendeleo.
Tunasikia kuna makundi ndani ya CCM na kila mmoja lina King Chawa wake ambae akiutwaa uRaisi mambo yatakuwa poa,Hivyo mapinduzi ya kileo hufanyika katika kumpata Mgombea Uraisi,mapinduzi daima ni kuwekwa kando Samia,kwa shinikizo kazi imemshinda,si mpiganaji na sababu lukuki na makubaliano kufikiwa kuwa asimamishwe mgombea mwingine,haya yaliyopo sasa ni mapigano ya kumzorotesha Samia ili achoke na atupilie mbali kutaka kugombea,ajiengue kabla ya kuenguliwa katika kikao ,ya kwamba wakiingia kwenye kikao basi tayari kazi imekuwa rahisi.
Haya makundi yachunguzwe na mmoja mmoja kukamatwa na kuwekwa mahabusu huku uchunguzi ukiendelea ,Mwalimu Nyerere alisema tusimuonee haya mtu,hawa ni wazembe wanayoiua nchi kwa kutaka kujenga himaya yao,kwanza kujiita au kuwepo kitu Sukuma gang huu ni zaidi ya ugaidi ni uhaini ni kuigawa nchi kwa misingi ya ukabila ,kesho na kesho kutwa kutakuwepo na Makuwa gang .
wakamatwe na kufunguliwa mashitaka.