What's reality? Wewe unachukulia reality kuwa subjective kwa sababu unaendeshwa na emotions na personal opinion, lakini ukweli ni kuwa kwenye suala la mahusiano reality ni objective, yaani ukweli wake hauwezi kubadilishwa na mtazamo mpya.
Ndoa ni UTEGEMEZI, kwamba mke amtegemee mume na mume amtegemee mke, watoto wawategemee wazazi, PASIPO UTEGEMEZI HAKUNA NDOA. Mke anamtegemea mume katika mambo YOTE yampasayo kuishi, mfano chakula, mavazi, afya nk. Mume anamtegemea mke katika kumfanya atekeleze shughuli zake kwa amani, kwa mfano akitoka kwenda kutafuta hataki kuwaza watoto watalelewa na nani, nani atakabili changamoto za nyumbani kabla hazijamfikia. Akirudi anatarajia afarijiwe, akutane na atmosphere ambayo itampa nguvu ya kuendelea kutafuta.
Sasa dunia ya leo imeondoa utegemezi kwenye ndoa, hivyo kuondoa MHIMILI wa ndoa. Maninti wakiwa mashuleni wanafundishwa kujitegemea (INDEPENDENT) ndio maana siku hizi kuna WAHUNI wamejioenyeza mpaka makanisani wakiwafundisha wanawake kutokuwa TEGEMEZI kwa waume zao. Kwamba ni kosa kubwa MKE WW NDOA kuomba kwa mume sidiroa ama chupi!! Kwa akili nyepesi hili laweza kuonekana jema, lakini kiuhalisia mwanamume anayekubali mtazamo huu hajui kwamba ndio anaandaa kifo cha ndoa yake.
Mwanamke amepaswa kumtii mume, hivi mwanamke mwenye OPTION ndani yake ndoa anawezaje kumtii mumewe? Hii ni ngano ya kufikirika zaidi. Mashuleni mabinti zetu wanafundishwa kuwa independent, wajitafutie kipato chao wenyewe, wawe na nguvu za kiuchumi ndani ya ndoa. Hili limemwondoa mwanamke kwenye nafasi yake kama mama na mlezi wa familia, na hiki ndicho unakiona ni REALITY. Ndio maana leo hii wanawake wengi licha ya kupewa mitazamo yao uongo kuwa wamekuwa na nguvu za kiuchumi bado wamezidi kuwa wenye huzuni, hawana furaha halafu hawaelewi kwa nini wanaume siku hizi hawaoi. Hata wanaooa hawakai kwenye ndoa zao, zimegeuka jehanamu ya moto. Hiyo REALITY iko wapi?
Wako wengi tu ambao wanaishi na familia zao kwa mfumo wa asili ambao ndio REALITY, kama ilivyokuwa kwa wazazi wetu. Kwa watu wa hivi ndoa zaweza kuwa hazina mali nyingi lakini zina utajiri wa furaha na amani tele. Watoto wanalelewa kwenye misingi halisi ya malezi, sio kufundishwa na mahausigeli. Hii ndio reality, hayo mengine ni illusions to ndio maana hayadumu.