Mkristo wa wapi ambaye happening muislam na muislam wa wapi asiyempenda Mkristo?
Mi nimeona katika familia ya Kiislam na mke wangu anaitwa Aziza na sasa amebadikisha Jina anaitwa Eliza huku akiwa a.etoka familia ya kishehe.
Tumezaliwa na kukulia katika maisha ya Ukristo, Baba yangu akiwa mzee wa Kanisa la Lutheran ila Dada yangu kabisa ameolewa na muislam na amebadilisha Dino sasa ni muislam. Watoto wake ambao ni wajomba zangu ni Waislam. Watoto wangu ni Wakristo huku Wajomba, Mama zao wakubwa na wadogo, mababu na mabibi ni Waislam. Sasa hapo chuki ipo wapi? Tunapendana, tunaheshimiana na kuvumiliana huku tukichukuliana ila nyie vijana wa hovyo humu JF kwa kutumia fake ID ndio mnatoa comments za kuchukiana ila kiuhalisia humu mitaani tu Binadamu na tu watanzania.