Qurani imefaradhisha jambo hilo kwa waumini yaani waisilamu walioiamini dini,na wala Qurani haijamtenza nguvu mtu mwingine kwamba ni lazima asile na hata hadharani.
Qurani iliyokuamrisha kufunga wewe muisilamu wapi Qurani hiyo imemkataza asiye muisilamu kula hadharani,aya ipi ?
Ndio Maana Qurani imeamrisha watu tumuabudu Mungu ila amri hiyo haitufanyi sisi tuwazuie wengine wasifanye ibada zao tofauti na za uisilamu.
Huwezi kusema kwamba kwa kuwa sisi waisilamu tumeamrishwa kusali basi tunawakataza wasiokuwa waisilamu wasisali kwa sababu sisi tunatekeleza ibada yetu.
Basi ndio katika funga iko hivyo hivyo,sisi tunaofunga ramadhani isitufanyd tukawakataza wasiokuwa waisilamu kula mchana tena hadharani,uisilamu hauko hivyo kama ndio tunaoufuata,ila kama tumeamua kwa utashi wetu ni vizuri tukawaeleza watu ili jambo hili lisilo na logic lisinasibishwe na uisilamu