Kwa maslahi mapana ya taifa na kwa kushirikiana na taasisi moja ya dini tumeazimia kufanya utafiti ili matokeo ya utafiti huo yaweze kuisaidia Serikali ya CCM, kupata mzizi iwapo kama kweli ugaidi upo na waliotuhumia na kukaa ndani zaidi ya miaka 5 kuna aliyekutikana na makosa hayo na kutumikia adhabu.
Jamii ya Kiislamu itaendelea kuuthibitishia umma kwa ni jamii isiyo na hatia kwa kuongozwa na:
• Kindness
• Trustworthiness
• Unselfish generosity
• Humility
• Great manners
• Self-awareness and courage
• Integrity and benevolence
Lakini pia ninyi ndugu zetu tungependa kwa pamoja muthibitishe kisayansi kupitia tafiti kujustify kamata kamata ya waislam kwa tuhuma za Ugaidi kama kuna usahihi wowote au kuna chuki na ubaguzi.
Wakili msomi Maledeka kwa kutumia weledi na ubobezi kaamua kuwasaidia waislam kuuthibitishia umma kuwa kuna hatari kama taifa na kutumia hisia kuwahukumu watu. Na matokeo yake nguvu kazi na pesa za walipa kodi inatumika kwa matumizi yasiyo na sababu zaidi ya kile waislam wanaona ni chuki za ubaguzi.
Wakili msomi anaeza zaidi ktk dkk ya 7 ya clip hii.
View: https://youtu.be/72rIuu-GSf0?si=YgXX61_IVXyjaAxT
Lengo la tafiti hii ni kutaka Maridhiano ya kitaifa ili kama ukamataji wa watuhumiwa uko una justification sheria hii uendelee, lkn kama kuna mapungufu basi sheria hii ifanyiwe marekebisho au ifutwe kabisa ili sheria ya uhalifu itumike kama MBADALA.
Utafiti huu tuwahusishe wadau wakuu wa kusimamia na kudhibiti ugaidi kama idara maalum ya kuzuia ugaidi, jeshi la polisi, jeshi la kimataifa (Interpol), ubalozi wa Marekani.
Naomba ushirikiano wako kwa kutueleza;-
1. Je, kisheria inaruhusia kwa taasisi ya kidini kuja na utafiti wa aina hii.
2. Unaweza dondoa ni maswali gani ya kuuliza kama dodoso katika utafiti huo.
Ili utafiti uje kutuletea majibu sahihi na thabit yenye kusaidia taifa
3. Nani anaishi katika mazingira ambayo jirani zake wamekamatwa kwa makosa ya ugaidi.
4. Je ungependa kushiriki kwa namna moja ktk tafiti hii.
Karibuni kwa michango yenye nia ya kujenga kwa maslahi mapana ya taifa