Kwanini Aluminium furnitures ni ghali sana?

Naweza kukupa estimation kwa kipindi hicho gharama ya kutengeneza mfano dirisha la 5x6 kama unanunua kila kitu kwa bei halali ilikuwa si chini ya 280000. Na hiyo bei ya sqm ilikuwa inajumuisha usafiri na kupachika ni juu ya mtengenezaji kama mteja yuko dar es salaam.
Hii 280,000 ndio cost unayoingia kutengeneza dirisha moja?
 
Wewe unaona ni sawa utumie gharama za laki 3.5 halafu upate faida zaidi ya laki 4?? Ni biashara gani nyingine utaifanya upate faida maradufu ya gharama?!
We wadhani mafundi wanafanya kazi kila siku? Unaweza kukuta mwezi mzima fundi anafanya kazi moja au mbili au hafanyi kabisa.
Bishara ya aluminum iko hivi kwa wengi. Anakuwepo mtu ambaye anauza material. Anakuwa kafungua sehemu ya kuuza material na ameweka mashine ya kukata profiles na meza. MAfundi wanakuja wenyewe. So fundi ndiye anatafuta mteja, akimpata anamleta ofisini. Mteja anaambiwa hapa ndo ofisini ashapata na fundi sasa ni chaguo la mteja ela kuilipa ofisini au kumpa fundi itategemea wanaaminiana vipi.
Ssasa fundi atanunua vifaa vyote pale na atatumia umeme na mashine bure. Ela ni ya fundi si ya muuza profile hata kama mteja aliilipa kwa fundi.
So unakuta ni mafundi wengi na si kila fundi anayepata kazi kila siku inawezekana ikawa mara moja au mbili kwe mwezi na wakati mwingine hata mwezi unaisha hapati kabisa.
Assume kazi ya milioni 3.5 ni dirisha nane, wewe ulitaka mtengenezaji apate shilingi ngapi kama labor charge?
 
Facts zinaonyesha kuwa maeneo mengi ya baridi hapa nchini ndipo mbao pia huzalishwa. Yaani miti hustawi sana maeneo hayo.
Huko mbao Huwa bei SAWA na Bure mkuu.
Ajabu utakuta sakafu za nyumba za hayo maeneo wamekomaa na tiles na madirisha ni ya aluminium!
 
  • Thanks
Reactions: rr4
UPVC dirisha 6x6 vifaa likaja 240000? Basi umetenda miujiza kama ya mwamposa. KWanza hakuna fundi anayeweza kukupa bei ya dirisha la upvc 6x6 kuwa 350000 maana ni zaidi ya hapo.
Pili madirisha ya upvc yanaungwa kwa mashine maalum ya welding ya hayo maplastic ambayo mafundi wengi hawana maana bei zake zimeshiba sana.
Sasa wewe unasema fundi alikuja na grinder na bench. Mkuu una uhakika umeweka upvc kweli au umeweka aluminum?
Mashine nilienda kukodi kwenye kampuni ya wachina (vijana w kibongo wanaofanya huko kazi maana wao bei ya kampuni ilinishinda na hata hio materials kuna baadhi niliuziwa ya ishu.
 
We wadhani mafundi wanafanya kazi kila siku? Unaweza kukuta mwezi mzima fundi anafanya kazi moja au mbili au hafanyi kabisa.
Bishara ya aluminum iko hivi kwa wengi. Anakuwepo mtu ambaye anauza material. Anakuwa kafungua sehemu ya kuuza material na ameweka mashine ya kukata profiles na meza. MAfundi wanakuja wenyewe. So fundi ndiye anatafuta mteja, akimpata anamleta ofisini. Mteja anaambiwa hapa ndo ofisini ashapata na fundi sasa ni chaguo la mteja ela kuilipa ofisini au kumpa fundi itategemea wanaaminiana vipi.
Ssasa fundi atanunua vifaa vyote pale na atatumia umeme na mashine bure. Ela ni ya fundi si ya muuza profile hata kama mteja aliilipa kwa fundi.
So unakuta ni mafundi wengi na si kila fundi anayepata kazi kila siku inawezekana ikawa mara moja au mbili kwe mwezi na wakati mwingine hata mwezi unaisha hapati kabisa.
Assume kazi ya milioni 3.5 ni dirisha nane, wewe ulitaka mtengenezaji apate shilingi ngapi kama labor charge?
Mafundi aluminium wajiongeze kufanya kazi nyingine mfano kufuga kuku kuliko kutegemea wateja wachache wawapige faida maradufu walimu wanajiongeza kuuza kashata na karanga badala ya kusubiria mshahara mdogo tu.
 
Aisee...mbona 230,000-250,0000 ndio mafundi huku mitaani wanatuuzia?
Ina maana kwa bei hiyo dirisha la 5x6 kakupigia sqm shilingi 80000. sheet ya 5mm thickness ambayo futi 6 kwa 7 inatoa madirisha mawili na inauzwa 95000 ikiwa ina maana kioo tu cha hilo dirisha moja 47000.
Basi kama madirisha ya 5x6 mnauziwa bei hiyo huko mtaani kwenu mnatenda miujiza. pia.
Pia fundi unaweza kumbana akupunguzie bei akakuwekea kioo cha 4mm ambacho ni cheap but aluminium kwa kawaida inafaa uweke kioo 5mm na hata akikuwekea kioo cha 4mm bado nina mashaka na hiyo bei uliyotaja.
Nakuuliza mkuu hilo dirisha ulilotaja ni 5x6 au 4x4?
 
Mashine nilienda kukodi kwenye kampuni ya wachina (vijana w kibongo wanaofanya huko kazi maana wao bei ya kampuni ilinishinda na hata hio materials kuna baadhi niliuziwa ya ishu.
Na profile moja ukanunua shilingi ngapi? Maana umetenda miujiza huenda nina la kujifunza kwako. Kuchoma dirisha kwa amshine hata si ela nyingi ni 10000 tu kwa kila dirisha. Issue ni profiles. Ulinunua bei gani?
 
Mafundi aluminium wajiongeze kufanya kazi nyingine mfano kufuga kuku kuliko kutegemea wateja wachache wawapige faida maradufu walimu wanajiongeza kuuza kashata na karanga badala ya kusubiria mshahara mdogo tu.
Mkuu mbona mafundi wanafanya kwa labor charge? Wewe nenda akupgie hesabu na mwambie kabisa kazi utafanyia site ili asiongeze material. Kanunue mzigo kaumwage site aje na watu wake apige kazi. Nakuhakikishai utasave pesa lakini si kwa ratio ya 50000 material 200000 baki.
na nikuulize, wewe unadhani fundi kwa labor charge kila dirisha anafaa akudai bei gani?
 
Labour charge iwe 30% ya gharama ya material
 
Ina maana kwa bei hiyo dirisha la 5x6 kakupigia sqm shilingi 80000. sheet ya 5mm thickness ambayo futi 6 kwa 7 inatoa madirisha mawili na inauzwa 95000 ikiwa ina maana kioo tu cha hilo dirisha moja 47000.
Basi kama madirisha ya 5x6 mnauziwa bei hiyo huko mtaani kwenu mnatenda miujiza. pia.
Pia fundi unaweza kumbana akupunguzie bei akakuwekea kioo cha 4mm ambacho ni cheap but aluminium kwa kawaida inafaa uweke kioo 5mm na hata akikuwekea kioo cha 4mm bado nina mashaka na hiyo bei uliyotaja.
Nakuuliza mkuu hilo dirisha ulilotaja ni 5x6 au 4x4?
Huyo fundi labda ndio ana miujiza. Ila ndio bei ananipa na nishajenga nyumba zaidi ya moja average price ya dirisha moja ni 230,000 anakuja kufunga yeye au vijana wake.
 
Labour charge iwe 30% ya gharama ya material
mkuu sisi enzi hizo labor charge ilikuwa 35000-40000 kwa dirisha... sijajua now. Now huenda pia imeshuka labor charge kwa sababu material zimepanda, mafundi wengi sana so competetion kubwa. Wewe patana na fundi ila ukipatana kazi lazima fundi ahakikishe chochote kitakachotokea ataweza kucover. Maana ikitokea vioo vimepasuka si hasara yako ni yake kwa sababu mmepatana kazi hadi dirisha linafungwa.
Yani ni sawa wakandarasi wanavyopiga kujenga ghorofa 500k kwa sqm ukiamua kumkabidhi kazi, ila ukiamua kutafuta mafundi wenyewe gharama inashuka? Kwanini? Kwa sababu anakupgia hivyo akijua chochote kitakahotokea ataweza kukicover.
By the way mimi si fundi ila nilikuwa na workshop, so nilijifunza, kupima, kupiga hesabu za vifaa baada ya kupima au kupewa vipimo vya madirisha. Nilitengeneza hadi spread sheet naweka vipimo inanipa kiasi cha materials kipindi hicho.
Nataka nirudi kwenye hii biashara mwaka huu ila kwa sasa nikuuza materials tu.
 
Huyo fundi labda ndio ana miujiza. Ila ndio bei ananipa na nishajenga nyumba zaidi ya moja average price ya dirisha moja ni 230,000 anakuja kufunga yeye au vijana wake.
Tatizo unasema dirisha moja. Dirisha moja la ukubwa gani. Kama ni 4 kwa 5 hiyo sawa kabisa maana hata akipiga kwa 120000 kwa sqm bado itaangukia humo au hata pungufu.
Nauliza tena, hayo madirisha yana ukubwa gani? Ni 5x6? haiwezekani maana wewe unaishia kusema dirisha moja hutaji kipimo cha amdirisha hayo.
labda nisema hivi 4x4 hata 180000 inatoa faida tena sqm hapo imepigwa kwa 120000
4x5 220000
5x5 akipiga kwa 120000 inakuja 270000 siku hizi hadi 115000 watu wanafanya.
ila 5x6 haiwezi kuwa 250000 hata akikuwekea kioo cha 4mm hatoboi labda kama anatenda miujiza.
 
Madirisha yangu ya kawaida ni 5*5 mengine machache ndio 5*6 na kuendelea.
Ya vyooni anafanya bure kwasababu vipande vinavyobaki ndio anatumia.
 
Hawa wajanja wajanja. Haya madirisha hayana bei kihivyo huwa nalipia 230,000 iwe 5*6 iwe 6*6 hawakatai na madirisha ya vyoo au stood anakufanyia bure.
😄

Ova
 
Back
Top Bottom