Kwanini asilimia 98 ya watanzania wanaojua Kingereza wanaongea Broken!! Tumerogwa au

Usimlaumu sana Nyerere. Humtendei haki. Alifanya sehemu yake sana tu. Nchi kama Zimbabwe na SA, kwa mfano, lugha mama ni lazima hadi vyuo vikuu, but angalia ngeli yao kwa sehemu kubwa ^imenyooka,^ tofauti ya Bongo ^imenyonyoka.^
Sikatai Nyerere alifanya makubwa. Lakini pia haiondoi ukweli kwamba kuna maamuzi yake mengine yameleta athari hasi tena za muda mrefu katika baadhi ya mifumo yetu kama nchi ikiwemo kwenye sekta ya elimu kama kuondoa kiingereza kama lugha ya kufundishia na sera ya elimu ya UPE

Sayansi ya lugha inasema mtoto wa miaka 0-12 ndio anaweza aka acquire(sio akajifunza) skills za native speaker wa lugha husika na akawa kama aliyezaliwa nayo

Juu ya hapo mtoto anajifunza lugha mpya kama foreign language na kuna uwezekano akashindwa kui master 100%. Ndio maana unaona tunakua na ma professor ambao wakiongea kiingereza wanashindwa kabisa kujieleza na hoja zao unaona kama za kwenye debate ya watoto wa form one!

Hayo ni matokeo ya kuiondoa lugha ya kiingereza kua lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya awali, sera ambayo iliasisiwa na Nyerere na bahati mbaya ikarithiwa na awanu zote zilizofuata

Hizo nchi unazosema wanatumia kiingereza kqma lugha ya kufundishia lakini wana sera ya ku preserve native and local languages zao ili zisifutike. Kiswahili hakiwezi kufutika hata kama ingekua hakitumiki kufundishia
 
Ungeanza kuwataja na majina ili tuwajuwe.
 
Kujua hiyo lugha kisiwe kipaumbele sana...tupende kiswahili chetu
 
Kuna mahala tulikwama toka enzi za uhuru...

Uamuzi ni wetu either tuchague kiswahili msingi mpaka chuo kikuu au kienglish msingi mpaka chuo kikuu.. tukiendelea na huu unafiki tutaendelea kuishi kama wachawi milele..
Yaani wewe, badala ya kuunda usafiri wako mwenyewe, unakimbilia kumsaidia jirani yako ilhali wako umeutelekeza!??? Kiswahili mbona ni lugha makini sana. Kinapendwa na kuzungumzwa na mamilioni ya watu ulimwenguni. Sadly, tumewaachia Wakenya ndio wanakifundisha huko ^angani^ kama ndiyo Kiswahili fasaha. Na brokens za Wakenya mnazijua.
 
Lkn pamoja na hayo yote, kiswahili kinatambulika duniani kote. Ndiyo maana hata UNESCO wametangaza kuwa July 7, ni siku ya kiswahili duniani. Ulimwengu umeona fursa za kijamii, kielimu, kiuchumi, nk ndiyo maana kimepewa siku rasmi ya kukitangaza. Suala ni je siku sisi kama Tanzania tumejipangaje kuelekea hili? Maana dunia imeonesha njia.
 
Kwanza lazima ujuwe kuna lahaja za lugha karibia 160,ya lugha ya kiingereza duniani.Kuna Accent na dialect,na zote twaweza sema ni lahaja.
Kuna British english,US english.Ndani ya Uingeteza peke yake kuna lahaja 29,bila kuingiza Wales,Scotland,Northern Ireland,Man,Channel Islands.
Amerika kuna lahaja 27,India kuna lahaja 14,Ireland 13,Australia 9.
Bado hapo lugha za kiingereza cha kisasa.
Kwa mtu asiyefahamu,anaweza kumkosoa msemaji wa lugha ya kiingereza bila kujuwa kama kuna lahaja tofauti karibia 160,na inasemekana hii idadi inazidi kuongezeka,na zote zinakubaliwa kwa kwa waingereza na waamerika .
 

Naheshimu hoja zako, ila hakuna hata moja ninayokubaliana nayo. Hatuna walimu. Hili ni tatizo mama. Hatuna mfumo mzuri wa elimu. Hili ni tatizo mtoto. Nchi yetu haijui inakoenda. Haijui miaka 100 na zaidi itakuwa wapi. Inajiendea tu kama jiwe linaloporomoka mlimani kuelekea bondeni. Likifika limefika. Likikwama mahali, ndipo hapo.
 
Asikudanganye mtu. Unapomiss lugha, unamiss opportunity. Haya mambo ya kujiliwaza kwenye uzembe na uvivu uletao hasara kwa taifa vimepitwa na wakati. Mr Nothing More, Nothing Less asingekuwa anajua ngeli, huenda leo hii angekuwa amejificha kule Singida Mashariki.
 
Si ajabu nawe ni mmoja ila mimi kidogo huwa naking'eng'ena
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Waziri wetu wa elimu anasemaje?
 
Boss jibu ni rahisi; hawajui Kiingereza. Huweza kujua lugha husika afu ukaongea broken. Haiwezekani! Kwa wasiojua Kiingereza nchi hii Profesa Ndalichako ni namba 2, namba 1 sitomtaja. Walishamsema sana humu JF
 
Boss jibu ni rahisi; hawajui Kiingereza. Huweza kujua lugha husika afu ukaongea broken. Haiwezekani! Kwa wasiojua Kiingereza nchi hii Profesa Ndalichako ni namba 2, namba 1 sitomtaja. Walishamsema sana humu JF
Au balozi Mula Mula Mana nae nasikia kinamsumbua
 
Watanzania tunatumia muda mfupi sana (wastani kwa siku)kuongea lugha hiyo.Jambo Hilo husababisha:
-kutozoea kutoa matamshi sahihi ya kiingereza,
-kutokuwa na mtiririko wa kimazoea kuiongea lugha hiyo,
-kukiongea kiingereza kwa kukitafsiri kichwani kwanza kutoka kiswahili kwenda kiingereza.Na hapo tunazalisha kitu kinaitwa tafsiri sisisi.Maana yake kutafsiri maneno moja kwa moja bila kuzingatia ukweli wake,mazingira na urahisishaji wa maelewano,
-kutanguliza hofu/woga na kuhisi watu wanakufuatilia uongeaji wako(Kutojiamini).
TUFANYAJE KWENDA MBELE.
-Kutoiogopa lugha hiyo na kujifunza/kufundisha wengine kwa mapenzi,
-kukifundisha kiingereza kwa kutumia kiingereza.Kama tufanyavyo kumfundisha mtoto Kiswahili kwa Kiswahili mpaka ajue,-kupenda kuongea (promptly) ili kuzoea misamiati,ufasaha,mitindo na miundo,
-kujiongezea utundu wa lugha kwa kusoma vitabu vyake na kutazama au kusikiliza wenye lugha yao kupitia television,magazeti,radio n.k,
-Ongea...weye ongea tu hadi lugha ikuzoee Usiogope kukosea.Mbona hata kiswahili tunachapia Mara nyingi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…