Kwanini asilimia 98 ya watanzania wanaojua Kingereza wanaongea Broken!! Tumerogwa au

Hata South Africa, Kenya, Malawi na Zimbabwe wana matatizo ya English.

Binafsi, ninachoona kina-miss ni kidogo sana hasa juhudi binafsi za kujifunza lugha.

Mtu akiamua kukaza kujifunza lugha anaijua vizuri tu.

MIfano halisi ni WAMASAI tena ambao hawakwenda shule kabisa.

Kuhusu lugha ya kufundishia, mkitaka mkae gizani kwenye huu ulimwengu kijiji ipotezeeni English.
 
Wamaasai English ni Lugha yao ya pili...hawajui kiswahili [emoji3][emoji3].

Hapana kwa Kenya nakubali Ila Zimbabwe na South Africa wapo level nyingine.

Najua viongozi wetu wanaogopa kuchukua maamuzi maana mara nyingi huja na lawama. Siynaona tunavyomnanga mzee Maghembe kwa mabadiliko ya mitaala hadi leo.
 
Tatizo la kuzungumza lugha ya kiingereza linaumiza waswahili kuliko waingereza.
 
Kama muda wote unaongea Kiswahili kamwe huwezi kuongea kiingereza fasaha, lugha lazima uifanyie mazoezi, hata kilugha huwezi kuongea kilugha fasaha kama alivyo mtu wa kijijini ambaye muda wote anaongea kilugha
 
Maisha yenyewe mafupi haya, Huo muda wa kupasua kichwa kuongea kingereza unautolea Wapi

Watu wanajadili namna kwenda Mars, Sisi ndio kwanza tunataka tuandae mdahalo wa Taifa kuhusu Lugha ya Kingereza

Haya ni matokeo ya Mfumo wa Elimu tuliorithi kutoka kwa Mkoloni, Sisi tunaandiliwa na Elimu kuwa Watuma Mpaka katika Lugha
 
Sisi tumewekeza kufanya Kiswahili kiwe lugha ya taifa ili kupambana na mabeberu.Tunataka tutumie kiswahili mpaka cheo kikuu.Tumesahau kuwa kujua lugha nyingi ni hazina katika zama hizi za utandawazi.
 
Acha dharau ongea namimi hapa sasaivi, sema Jf hakuna ujumbewa sauti ungetafuta pakutokea mkuu.
 
ungekuwa wa maana kama hoja hii ungeileta kwa kingereza.
 
Waziri Ndalicheko anaweza kujibu hili kwani naye ni mmojawao!!
Merikebu inapigwa upepo mkali!!
 
English ya kusoma ni tofauti na kuzaliwa au uwe umelelewa na wazungu au ukikutana na guide wa muda mrefu
 
Bro unataka mtu azungumze kwa 100℅ ili iweje????? Kwani hiyo Broken English haieleweki??? Mbona tunaelewana tu vyema na wazungu kwa Broken hiihii!!!.

Nenda Ujerumani, China, France nk usikilize hao wachache wanaozungumza Kiingereza kama Kimenyooka.

ACHENI ULIMBUKENI BHANA
 
Kaka nimecheka sanaa hahahahahah
 
Una nafuu
Mimi nikiongea sekunde 50 niko hoi kiu ya kunywa maji hatari.
 
hili ni janga la kitaifa japo wengi watakwambia wachina, warusi, wajerumani, waitaliano na wafaransa hawaongei kingereza lakini wanasonga mbele.

wanasahau kwamba hao ni watu wanaotokana katika mataifa ambayo yapo stable kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

sisi hatuna sababu ya kukikwepa kingereza kwasababu taifa letu ni changa kiuchumi, kijamii na kitamaduni. utamaduni wetu na lugha yetu haviwezi ku-influence taifa lolote.

wazazi msipotoshwe na fikra mgando za wanasiasa wa tz hususani wa chama tawala kuhusu kingereza.

muwasisitize watoto wenu wajifunze kuzungumza kingereza ili waje kuwa competent kwenye soko la ajira za kimataifa ambazo nyingi hunyakuliwa na wakenya.
 
Tatizo ni Kiswahili kutumika kama Lugha kuu ya Mawasiliano (Lugha Mama ya Nchi/Taifa).
Vigezo na masharti ya kuongea hayapo sehemu za kazi /kiuchumi au kwenye huduma za kijamii.
Hata hivyo ni wajibu wetu/muhimu kujifunza lugha nyingine nyingi ili kukidhi mahitaji ya ukuaji wa Uchumi wa Dunia.
 
Upo sahihi kabisa, ila kujitia ujuaji kujua kiingereza na kuwadhihaki wengine wapo vizuri......acha wakenya waendelee kutucheka.
 

Icho kichwa cha habari tu nimecheka kifala[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hatujarogwa mkuu!!! Tatizo ni hao walimu wa kingereza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…