Kwanini asilimia 98 ya watanzania wanaojua Kingereza wanaongea Broken!! Tumerogwa au

Kwa mazingira ya TZ Kiswahili lazima tu utaongea. Kwa hiyo mkazo uwekwe kwenye Kiingereza. Kiswahili kiwe somo tu. Medium of instruction kwa masomo yote yaliyobaki iwe Kiingereza. Ndivyo ilivyo Kenya, Uganda, Malawi... Wao wanaongea lugha zao na Kiingereza kwa ufasaha. Sisi tumeweka mkazo kwenye Kiswahili ambacho hata usipoenda shule utazungumza tu.
 
Tatizo letu tunasoma masomo ya Kiingereza kwa Kiswahili. Mwl wa Physics anafafanua kwa Kiswahili. Chuo Ma lecturer wengi Sasa nao wanaandaa PPT kwa Kiingereza lakini wanasoma na kufundisha kwa Kiswahili, hapo Kama nchi hatuwezi kufika. Imagine Profesa Kama mama Yetu wa Kasulu mjini anaongea Kiingereza chenye ugoko vile, vipi ndugu zangu waliopo maji uko na vidiploma vyao?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nadhani badala ya kujikita kushadadia lugha tusiyoielewa (miaka zaidi ya 60 sasa tangu Uhuru), hebu tukuze lugha yetu ya Kiswahili. China, Urusi, nchi za Kiarabu na hata Ulaya wanajivunia lugha zao.
Mambo ya kukuza lugha ni ushamba, lugha huwa inakuwa yenyewe kwa sababu ya uhitaji na umuhimu wake katika muingiliano wa watu. Tunachotakiwa ni kuamua lugha moja ya kufundishia kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.
 
Hata baadhi ya waingereza huongea kiingereza kibovu.
 
KIKUBWA PUMZI BURE.
Kuna mchina,mjapan,mrusi n.k
Hyo NI lugha ya watu Kama unavyoona kimakonde,kimatumbi,kichaga n.k
 
Ni kweli.mimi siwezi kuongea kiingereza.ila mtu hawezi kuniteta kiingereza nikashindwa kumuelewa.
 
Midahalo ya Kiingereza hakuna kabisa amashuleni. Sisi wakati tunasome kuanzia shule ya msingi hadi sekondari kulikuwa debate sessions kila wiki, ambapo watu wanajipanga makundi mawili na kuepwa topici ya kubishana kwa kiingereza. Ilikuwa inasaidia sana uwezo wa kujenga hoja kwa kiingereza. lakini sasa watu wengi hupanga hoja zao kwa kiswahili halafu ndipo waziongee kwa kuzitafsiri kiingereza. Inatakiwa hoja ipangwe moja kwa moja kwa kiingereza. Kwa Mfano paper hii ya "Dr." Biteko unaona kuwa mawazo yake yalipangwa kwa kiswahili, na alipoamishia mawazo yake katika kiingereza akaandika broken tupu. Na huyo ni Dokta yaani Ph.D. holder.

 
Samahani, unaweza kukorect Ili nasi tujifunze kitu Mana wengine tunaweza Ina Kama amepatia
 
Shule ya msingi masomo 5 yote kiswahili moja tu ndo kingereza, secondary masomo 9-12 yote kingereza 1 tu ndo kiswahili elimu ya Tz inacheza sarakasi za hatari sana mtu unamaliza had form4 lakin hujui unasoma ili uwe nani, na hata ukitaka kuwa nani utakuja kufanya kazi ambayo hukuiwaza, wengi wanafanya kazi ambazo ni nje ya ndoto zao
 
Iwapo wanaongea broken ni dhahiri hawajui kiingereza
 
Kina ndalichako Na magu wajibu hili
 
Inawezekana kabisa. Tukiweka mjadala wa kitaifa jibu litaptikana.

Suala la Lugha linatuvuta nyuma saana.
Mkuu kama mambo mepesi hatujafanikiwa, unadhani hili ndilo tutafanikiwa? Kama hafi ujenzi wa madarasa ni shida hadi kumaliza tu ufisadi bandarini tumeshindwa walau hata ukapungua mizigo ikatoka kwa wakati, hili la kukuza lugha ndo tutaweza?
 
Nyie ndo mnasababisha broken isiishe,
Mna critique issue ndogo kwenye maongezi na mnaongeza uoga wa kuongea,
Watu wanakosea Kiswahili na hamuoni shida Ila mtu akikosea kingereza kwenye public speaking inakuwa nogwa.
Acheni hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…