Kwanini Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere hakunyanyua kalamu kuandika maisha yake?

Kwanini Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere hakunyanyua kalamu kuandika maisha yake?

Shetani / Ibilisi kazini katika muendelezo wa kumchafua Mwalimu
Mzizi...
Ningeandika kitabu kwa nia ya kumchafua Mwalimu kitabu changu ningekiua mapema sana kisingeendelea kuwa hai hadi leo.

Kitabu cha Historia ya TANU kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni kwa kuwa kiliandikwa kwa nia ya kufuta historia ya kweli kimekufa hakisikiki wala hakionekani popote pale.

Ikiwa unaona nimeandika kitu chochote ambacho si kweli ila ni kumchafua Mwalimu kiweke hapa wasomaji wote washuhudie ukweli wako.

Nami ningependa kukuuliza swali.
Ulikuwa unaijua historia ya Abdul Sykes na Julius Nyerere?

Huoni kama kwa mimi kuiandika historia hii tumeiongeza elimu katika historia ya Mwalimu binafsi na historia ya TANU na harakati za kupigania uhuru?

Hujaipenda historia hii?
Je, ungependa tubakie na historia ya Kivukoni peke yake?

1648439182288.png
 
Mzizi...
Ningeandika kitabu kwa nia ya kumchafua Mwalimu kitabu changu ningekiua mapema sana kisingeendelea kuwa hai hadi leo.

Kitabu cha Historia ya TANU kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni kwa kuwa kiliandikwa kwa nia ya kufuta historia ya kweli kimekufa hakisikiki wala hakionekani popote pale.

Ikiwa unaona nimeandika kitu chochote ambacho si kweli ila ni kumchafua Mwalimu kiweke hapa wasomaji wote washuhudie ukweli wako.

Nami ningependa kukuuliza swali.
Ulikuwa unaijua historia ya Abdul Sykes na Julius Nyerere?

Huoni kama kwa mimi kuiandika historia hii tumeiongeza elimu katika historia ya Mwalimu binafsi na historia ya TANU na harakati za kupigania uhuru?

Hujaipenda historia hii?
Je, ungependa tubakie na historia ya Kivukoni peke yake?

View attachment 2166567
We mzee uache ujinga wakati mwingine, kwani wewe unaijiua historia ya Mwl Nyerere na baba yangu?

Walishawahi kuwa pamoja kabla ya uhuru na wakasaidiana mengi tu, tunaoijua wachache tu...lkn haitusumbui!
Mwl Nyerere alishafanya kazi na watu wengi tu na wengine walikuwa muhimu sana.

Any way twende kwenye point yangu, shetani yuko hivi...akija kwa mtu hajitambulishi kuwa yeye ni yule shetani mlaaniwa, anajifanya mwema na mleta habari njema. Mahala pengine alileta na dini, watu wakawa tayari kuuakuitetea dini hiyo kumbe wanamtetea shetani!
 
Mzizi...
Ningeandika kitabu kwa nia ya kumchafua Mwalimu kitabu changu ningekiua mapema sana kisingeendelea kuwa hai hadi leo.

Kitabu cha Historia ya TANU kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni kwa kuwa kiliandikwa kwa nia ya kufuta historia ya kweli kimekufa hakisikiki wala hakionekani popote pale.

Ikiwa unaona nimeandika kitu chochote ambacho si kweli ila ni kumchafua Mwalimu kiweke hapa wasomaji wote washuhudie ukweli wako.

Nami ningependa kukuuliza swali.
Ulikuwa unaijua historia ya Abdul Sykes na Julius Nyerere?

Huoni kama kwa mimi kuiandika historia hii tumeiongeza elimu katika historia ya Mwalimu binafsi na historia ya TANU na harakati za kupigania uhuru?

Hujaipenda historia hii?
Je, ungependa tubakie na historia ya Kivukoni peke yake?

View attachment 2166567
Eti usingekuwa hai hadi sasa!..
Ona ulivyojaa hila wewe mzee mwovu, hapo unawafundisha "ndugu zako" kuwa Nyerere aliua na anaendelea kuua wanao mkosoa.

Mbona wewe na ndugu zako mnamwita laana Mwl na hamfi?

Kufa utakufa tu siku moja siku yako itakapofika wala sio kwa kumkosoa Mwl
 
KWA NINI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE HAKUNYANYUA KALAMU KUANDIKA MAISHA YAKE?

Naikumbuka siku hii kama jana vile.

Niko nje ya mipaka ya Tanzania ni nyakati za usiku niko kwa rafiki yangu mmoja ambae ajabu sana yeye ananiambia kuwa aliona kitu katika maandishi yangu toka enzi nikiandika na Africa Events.

Kila tulipokutana alinisisitiza kuwa nipunguze kuandika katika magazeti na majarida na niwe mwandishi wa vitabu.

Wakati ule nilikuwa hili naliona jambo nisiloliweza kabisa.
Huyu rafiki yangu ni ‘’publisher,’’ yaani mchapaji vitabu tena mchapaji wa sifa.

Sasa siku hii tumekaa nyumbani kwake baada ya chakula cha jioni na tunazungumza kuhusu mswada wa kitabu changu cha maisha ya Abdul Sykes.

Rafiki yangu huyu alikuwa kausoma mswada wote akaniambia, ‘’Mohamed umemwandika sana Nyerere tena kwa undani na umakini mkubwa sijapatapo kusoma popote pale mwandishi ambae amemuandika Nyerere kwa kiasi hiki ulichofanya wewe.’’

Huyu rafiki yangu akaendelea, ’’Mimi niliomba miadi na Nyerere na akakubali kukutana na mimi Butiama.

Tulipoonana nikamwambia kuwa kuna mchapaji angependa kufanya mradi wa kuandika maisha yako.’’

Rafiki yangu akaniambia kuwa jibu la Nyerere lilikuwa, ‘’Mimi sizungumzi na mtu wa kati waambie hawa jamaa zako waje wanione mimi mwenyewe binafsi.’’

Rafiki yangu akanambia kuwa huo ndiyo ukawa mwisho wa mazungumzo yao akanyanyuka na kuondoka kuwahi ndege arudi Dar es Salaam.

Huyu rafiki yangu ndiye alikuwa mwakilishi wa hawa wachapaji katika kanda ya Afrika ya Mashariki na Kati na Mwalimu akiwafahamu vyema hawa wachapaji.

Rafiki akanambia hakuona kama kulikuwa na haja ya yeye kulisema hili kwani anasema Mwalimu hili akilijua fika.

Sahib yangu huyu alinifahamisha kuwa jibu lile alilitegemea kwa kuwa yeye kabla ya kuja kumuona Mwalimu alikuwa amefanya utafiti wake na taarifa alizopata zilikuwa Nyerere hataki maisha yake yaandikwe ingawa aliwaruhusu waandishi wawili kutoka Maryknoll, W. R. Duggan na J. R. kuandika maisha yake, ‘’Tanzania and Nyerere,’’ (1976).

Tukawa tunashughulisha fikra zetu kwa nini Mwalimu Nyerere hataki kuadikwa na kwa nini yeye mwenyewe hanyanyui kalamu yake kuandika maisha yake.

Huyu rafiki yangu akaniambia kuwa yeye angependa sana kuchapa kitabu changu lakini hataweza kwa sababu ya ‘’conflict of interest,’’ kwani yeye anafanya biashara na Serikali ya Tanzania na ana wasiwasi na yale maudhui ya kitabu changu.

Akaniambia kuwa kwa uzoefu wake hakuna mchapaji Tanzania atakaechapa kitabu changu.
Kauli hii ilinitia huzuni sana.

Nikamuuliza kwa nini wachapaji hawataki kukigusa kitabu changu?

Rafiki yangu akanijibu kwa ufupi sana, ‘’Wewe unaandika historia ya Julius Nyerere bila ya idhini yake.’’

Rafiki yangu akaniambia, ''Mohamed you have to learn the trade.''
Kwa hakika nilihangaika sana na kitabu changu kwa miaka mingi.

Miaka ile nilikuwa kijana mdogo nisiyejua siasa za Afrika zinavyochezwa na biashara ya vitabu inazunguka katika mzunguko na muhimili upi.

Lakini baadae kama mtu aliyegutushwa kutoka katika njozi likanijia wazo nijaribu kuwasilianana na wachapaji wa Uingereza.

Hakika kila kitu kinakwenda kama Allah alivyokipanga.
Kitabu kikachapwa London.

Baada ya kuchapwa kitabu hiki changu ndipo ikaonekana lazima kitabu cha Maisha ya Mwalimu Nyerere kiandikwe.

Hiki ni kisa kingine hapa si mahali pake kukieleza.

Lakini laiti Mwalimu mwenyewe angenyanyua kalamu kuandika maisha yake kwa hakika tungestarehe sana na kalamu yake.

Mimi hukaa peke yangu kimya nikajifanya mimi ndiye Julius Kambarage Nyerere na sasa naandika maisha yangu.

In Shaa Allah iko siku nitakuonyesheni nilichoandika.
Nimepata kumuonyesha maandishi haya yangu publisher mmoja.

Ajabu sana akaniambia hiki ni kitabu lakini ni riwaya ya aina yake akanihimiza nikamilishe kazi hii.

Akatanitania akaniambia, ''Mohamed umekuwa Irving Wallace?''

Huyu Irving Wallace ni mwandishi wa riwaya akiandika vitabu vyake kutokana na matukio ya kweli katika jamii.

Ukweli ni kuwa mimi sikumgeza Irving Wallace.
Mimi nimemuiga Shafi Adam Shafi jinsi alivyoandika kitabu chake maarufu, ''Haini.''

Lakini uweli utabakia kuwa laiti Mwalimu angeandika kumbukumbu zake tungepata kitabu ambacho si cha kawaida.

Historia ya Mwalimu Nyerere na TANU na uhuru wa Tanganyika ina ladha ya pekee sana waandishi wa kitabu chake hawakuweza kuionyesha ladha hii katika mseto waliopika.

Mseto wao chooko na mchele haukuwa sawia.
Sikuambii mchuzi wa papa wa kulia mseto.

Viungo havikukamilika.

View attachment 2153570
Aliacha historia ijiandike, maana alifanya mengi. Ila hawa wanaofosi kutuandikia story za maisha yao zilizorembwa, wanatuchanganya tu
 
We mzee uache ujinga wakati mwingine, kwani wewe unaijiua historia ya Mwl Nyerere na baba yangu?

Walishawahi kuwa pamoja kabla ya uhuru na wakasaidiana mengi tu, tunaoijua wachache tu...lkn haitusumbui!
Mwl Nyerere alishafanya kazi na watu wengi tu na wengine walikuwa muhimu sana.

Any way twende kwenye point yangu, shetani yuko hivi...akija kwa mtu hajitambulishi kuwa yeye ni yule shetani mlaaniwa, anajifanya mwema na mleta habari njema. Mahala pengine alileta na dini, watu wakawa tayari kuuakuitetea dini hiyo kumbe wanamtetea shetani!

Historia ya Tanganyika na kwa makusudi nataka nianze na hii kwa kuwa mimeitafiti na kuandika kitabu ambacho naamini sote tunakifahamu.

Umuhimu wa historia hii unasimama kwenye historia ya kudai uhuru chini ya TANU.

Chuo Cha CCM Kivukoni kilichapa kitabu cha historia ya TANU mwaka wa 1981.

Kitabu hiki kilichapwa baada ya Abubakar Ulotu kuandika historia ya TANU kutoka mswada ulioanza kuandikwa na Abdul Sykes na Dr. Wilbard Kleruu labda mwaka wa 1962.

Uandishi wa kitabu hiki uliingia katika matatizo na Abdul Sykes akajitoa kazi ikakamilishwa na Dr. Kleruu peke yake.

Tatizo katika utafiti huu lilikuwa kwanza nafasi ya baba yake Abdul, Mzee Kleist Sykes katika uasisi wa African Association mwaka wa 1929.

Tatizo jingine likawa nafasi ya Abdul Sykes katika TAA baada ya kifo cha baba yake mwaka wa 1949.

Halafu pakawa na tatizo la Julius Nyerere.
Nini mchango wake katika kuunda TANU?

Abdul alipojitoa katika uandishi wa historia hii ikawa kwa uamuzi ule umetoa fursa kwa waliobakia kuandika historia waliyoitaka wao.

Abdul Sykes akafutwa kwenye historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Mswada huu haukuchapwa na ukawa Maktaba ya TANU Mtaa wa Lumumba na hivi ndivyo ulivyoangukia mikononi kwa Abubakar Ulotu na yeye akachapa kitabu kwa jina lake.

Historia iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni haina tofauti na ile "aliyoandika," Abubakar Ulotu.

Miaka ikapita.

Mwaka wa 1998 mimi nikachapa kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kitabu kilichoeleza historia ya TANU na harakati za kudai uhuru.

Kitabu hiki kilipindua historia ya TANU juu chini.

Kitabu kilimleta Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kama chanzo cha kuundwa kwa TANU na harakati za uhuru.

Kadhalika kitabu katika hili kitabu kikamleta Chief David Kidaha Makwaia katika juhudi za kutafuta kiongozi wa kuongoza harakati za kudai uhuru.

Kuna watu hawakuridhika na kitabu hiki hasa kwa kuwa kilionyesha mchango mkubwa wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Watu hawa wakataka kiandikwe kitabu kuonyesha mchango wa Julius Nyerere katika kuunda TANU.

Kitabu hiki kipo sokoni hivi sasa.

Swali la kujiuliza ni hili.

Je kuna mapya ndani ya kitabu hiki ambayo yanabadilisha yaliyomo kwenye historia ya TANU iliyokwisha andikwa?

Tutegemee nini katika historia hii mpya inayotayarishwa hivi sasa?

Picha hiyo hapo chini ilipigwa siku TANU wanamsindikiza Julius Nyerere uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO 1955.

1648463193315.png
 
Asichotaka kukubali huyu Mjahdina ni kuwa wazee wake walianzisha harakatti za Uhuru ,wakawa hawana Vision namna ya kusonga mbele!
Wakampata kijana smart ,wakaona wampe kijiti,Julius akaichuakua TAA na kuipeleka juu kileleni!
Tatizo Liko wapi,inakuuma Nini!
Mbona Nyerere na Historia inawatambua wale wote nchi mzima!
Hii kuimba Sykes ,mara Dosa ...kunaboa !
Historia inabeba Tanganyika na Wala Si mzizima!
 
Asichotaka kukubali huyu Mjahdina ni kuwa wazee wake walianzisha harakatti za Uhuru ,wakawa hawana Vision namna ya kusonga mbele!
Wakampata kijana smart ,wakaona wampe kijiti,Julius akaichuakua TAA na kuipeleka juu kileleni!
Tatizo Liko wapi,inakuuma Nini!
Mbona Nyerere na Historia inawatambua wale wote nchi mzima!
Hii kuimba Sykes ,mara Dosa ...kunaboa !
Historia inabeba Tanganyika na Wala Si mzizima!
Makulaga,
Kipi kinakughadhibisha kufikia kutoa matusi?
Kwani kuwa ''Mujahid,'' hakuruhusiwi?

Mbona tunao walokole nchini petu wengi tu?

Kuwa wazee wangu hawakuwa na ''vision,'' hii si kweli kwani wameunda African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.

Vyama vyote hivi vimepigania uhuru wa Tanganyika.

Hafla ya kumuaga Nyerere safari ya kwanza UNO 1955 ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya.

Iko barua ya 1933 Mzee bin Sudi President wa AA akimwandikia Kleist Sykes kukumbusha umuhimu wa kuitoa Tanganyika katika mikono ya wakoloni.

Soma kitabu hiki: ''Modern Tanzanians,'' (1973) kimehaririwa na John Illife utakuta mengi usiyoyajua.

Ikiwa uko ''bored,'' na kalamu yangu dawa ni kutonisoma siyo kunitukana.
Lakini kuna wengi wanapendezewa na ninayoandika na wananisoma kila uchao.

Hujalazimishwa kuingia ukurusa huu.

1648470779167.png
 
Asichotaka kukubali huyu Mjahdina ni kuwa wazee wake walianzisha harakatti za Uhuru ,wakawa hawana Vision namna ya kusonga mbele!
Wakampata kijana smart ,wakaona wampe kijiti,Julius akaichuakua TAA na kuipeleka juu kileleni!
Tatizo Liko wapi,inakuuma Nini!
Mbona Nyerere na Historia inawatambua wale wote nchi mzima!
Hii kuimba Sykes ,mara Dosa ...kunaboa !
Historia inabeba Tanganyika na Wala Si mzizima!
Huyu mzee ni tapeli, kawashika sana akili ndugu zake waliozoea kugeuziwa uongo kuwa ukweli!
 
Kila mtu Aandike historia katika nchi hii nani Atasoma sasa!
 
Kila mtu Aandike historia katika nchi hii nani Atasoma sasa!
Kiok...
Haijawa kila mtu kuandika.

Historia ya uhuru wa Tanganyika imeandikwa na Judith Listowel (1965), John Iliffe (1968), Kimambo na Temu (1969), Abubakar Ulotu (1971), Chuo Cha CCM Kivukoni (1981), Mohamed Said (1998) na Shivji, Saida Othman na Ngwazi Kamata (2020).

Hawa hawajawa kila mtu kwani ni wachache sana.

Wasomaji wa vitabu ni maelfu ya watu.
 
Nyerere alikuwa mtu smart sana tofauti na yule hayati wa Chato ambae alikuwa ana mienendo yenye kuutia dosari udaktari wake
 
Huyu mzee ni tapeli, kawashika sana akili ndugu zake waliozoea kugeuziwa uongo kuwa ukweli!
Mzizi...
Kuwa mimi ni mwizi labda ni hasira ndizo zimekuzidi sasa huwezi tena kupima kauli zako unatokwa na matusi bila kujijua.

Mimi niko JF kwa miaka mingi sana na wengi wananifahamu.
Tulia akili zirejee mahali pake utanifahamu vyema.

Angalia picha hiyo hapo chini.
Naamini unamfahamu Bwana Mkubwa huyu.

Alikuja nyumbani kwangu kunikabidhi zawadi ya simu Infinix Note 10 na cheti nilichotunukiwa na JF kwa uandishi wa makala za historia.

1648485651854.png
 
Stories/myths zilizozaliwa, kukua na kukomaa ndizo zimeibua na kuangusha mataifa, falme na empires. Watawala wengi wanafahamu hilo ndio maana wanapatwa na hofu na kufanya kila njia kunyamazisha sauti za mawazo tofauti hata kama ni ndogo sana.
Nilijua tangu mwanzo ulikuwa unazunguka tu lakini nia yako ipo katika sentensi ya mwisho.

Mwl Nyerere kamwe hawezi kuhofia Mambo madogo madogo,Huyu ni jabali wa siasa za Afrika hawezi kuhofia wenyeji wa Tandamti na Msikiti wa Manyema.
 
Bi Kidawa utafanya uchafuzi tu hapa, hembu kaa kimya wenye busara wazungumze.
Nafsi ilikuwa inamsuta, sio muda. Kama alikuwa na muda wa kutafsiri ngano za Shakespeare asingeweza kuandika ukweli kuhusu yeye mwenyewe?
 
Kwa watu wanaomfahamu Nyerere ni nadra na tabu kupata kauli yake akisema '' mimi au Nime''. Nyerere hakupenda kutajwa kama yeye bali alitumia sana wingi '' Sisi, tuli.. n.k'

Akiwaaga Wazee wa Dar es Salaam pale Diamond kwa nadra nilimsikia akisema '' Nilikuwa Mkristo peke yangu''. Katika siku nadra sana hiyo ilikuwa moja akitumia neno ''Nili..''

Tatizo la kuandika kitabu chake ni kwa kutambua alishirikiana na watu wengine na ni ngumu sana kuandika 'Memoir' yake . Nyerere hakujifaragua wala kujikweza

Nyerere alifahamu kuandika 'Mmemoir' angegusa mambo mengi kama ugomvi wake na akina Abdul Sykes, Bibi Titi, Rais Karume, ujamaa, kutaifisha mali, Bakwata, Mali za Kanisa n.k. na pengine angeligawa Taifa zaidi kwa kitu kidogo cha kuepukika.

Nimesoma kitabu cha AH Mwinyi na BW Mkapa. Ukweli wamekwepa vitu vingi vya msingi.
Hiyo yote ililenga kutoleta mjadala wa kuligawa Taifa. Mkapa hakupenda alilazimika tu. Hivyo kuna sababu za kwanini hakutaka na kwanini alikubali baadaye

Nyerere alikubali baadaye kwasababu aliona bila sauti yake upotoshaji ulikithiri.

Hoja kwamba aliingizwa siasa na wazee wa Dar es Salaam haina msingi na ni ya kupuuzwa.

Nyerere kabla ya kufika Dar es Salaam alikuwa katika siasa.
Nyerere alikwenda masomoni Scotland ambako alikutana na wanasiasa wa dunia.

Kwa ujio wake Dar es Salaam mambo mengi yalibadilika.

Nyerere aliandika au '' kunukuu'' katiba iliyoitwa ya TANU. Hakuna aliwahi fanya hivyo kabla

Nyerere akasambaza chama kwa nguvu sana nchi nzima, hakuamini siasa za Mzizima pekee
Mwalimu akaungwa mkono na Watanganyika na kupata 'uhalali' wa kwenda UNO.

Uwezo wa Mwalimu unathibitika ndani ya baraza la wazee wa TANU(rejea picha ya Mohamed Said). Mwl aliwakuta na harakati, akafanya nao kazi asilimia 98 ikiwa ni Waislam.

Nyerere akawaongoza kufikia Uhuru wa nchi. Huyu anafundisha au anafundishwa?

Hii haina maana Mwalimu alikuja na harakati, la hasha, vyama vilikuwepo.

Kilichomsaidia Nyerere ni elimu na kuwa na ufahamu wa dunia na siasa za dunia.
Hiyo ndiyo siri ya kupokelewa kisha kuwaongoza! na si kuingizwa !

Ngongo Kiranga
Alishirikiana na nani kuuondoa mfumo wa vyama vingi kwenye hii nchi mwaka 1967?
 
Hilo alishajibiwa mwengine...


Dudu kaandika hayo hapo chini na mimi nimeona nifungue uzi mpya niweke maelezo katika hayo maneno yake ili kusahihisha makosa ya historia ya TANU ambayo yamekuwa yakijirudia sasa nusu karne:

MAKOSA YANAYOJIRUDIA KATIKA HISTORIA YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE NA TANU

Dudus said:

''... watu wa pwani walikuwa na advantage ya Kiswahili kwa wakati huo kiliwabeba sana. Ningeletwa mimi mhadzabe na Kiswahili wapi na wapi! Inasemekana hata Nyerere wakati anafanya urafiki na wazee wa Kariakoo hadi wakamkabidhi TANU, Kiswahili kilikuwa kinampa shida to some extent; ila kimalkia ungedhani anaishi kwenye corridor za Buckingham.''

Jibu langu kwake hili hapo chini:

Dudus,
Mwalimu Nyerere hakupokelewa Dar es Salaam na mzee yeyote alipofika mwaka wa 1952.
Hii ni katika moja ya makosa yaliyomo katika historia ya TANU.

Nyerere mtu aliyekuwa anajuananae kwa karibu sana alipofika Dar es Salaam ni Joseph Kasella Bantu.

Kasella Bantu akiishi Temeke.

Ilikuwa wakati mwingine Mwalimu akija mjini basi atalala kwa Kasella Bantu siku ya pili atarejea Pugu.

Kasella Bantu ndiye aliyempeleka Nyerere kwa Abdul Sykes.
Abdul Sykes alikuwa ndiye Secretary na Act. President wa TAA.

Hicho chama cha TAA kimetokana na African Association chama ambacho baba yake Abdul, Kleist Sykes alikuwa katibu muasisi mwaka wa 1929.

Hakuna mzee yeyote aliyempokea Nyerere alipofika Dar es Salaam kutafuta viongozi wa TAA wala hakuna mzee yeyote aliyemkabidhi Mwalimu chama cha TANU.

Wala Mwalimu hakupata kujulikana hadi pale alipokuja kusuhubiana na Abdul Sykes katika siasa za TAA kuelekea kuundwa kwa TANU.

Hii ilikuwa kati ya mwaka wa 1952 - 1954.

Katika historia ya TANU kutokea TAA wazee waliokuwa ndani ya uongozi wa TAA na wao kushiriki katika kuweka msingi wa kuunda TANU walikuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Said Chaurembo aliyekuwa Liwali Mahakama ya Kariakoo.

Hawa walikuwa wajumbe katika TAA Political Subcommittee ilyoundwa mwaka wa 1950.

Wajumbe wa TAA Political Subcommttee walikuwa Dr. Vedast Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Sheik Hassan bin Ameir, John Rupia na Sheikh Said Chaurembo.

Wala si sawa kusema kuwa Nyerere aliunda TANU.

Historia ya TANU inaanza mbali sana kwa karibu ni mwaka wa 1945 Abdul Sykes, Ally Sykes na askari wenzao katika 6th Batallion KAR Burma Infantry wakiwa Kalieni Camp Bombay hapo ndipo katika mkesha wa Christmas, 1945 walipoamua kuunda TANU kudai uhuru wa Tanganyika na jina hili lilitolewa huko.

Hapo Kalieni Camp askari Waafrika kutoka Afrika ya Mashariki walikuwa wanasubiri kurudishwa makwao baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945).

Urafiki wa Nyerere na wazee wa Dar es Salaam ulianza baada ya TANU kuundwa 1954 na mzee aliyekuwa karibu sana na Mwalimu alikuwa Mzee Mshume Kiyate mwaka wa 1955.

Ukipenda unaweza ukawaongeza na wengine kama Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi na Max Mbwana.

Historia hii nimeiandika kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).

Kulia ni Mzee Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Mzee Max Mbwana na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi.

Inasikitisha kuwa baada ya uhuru miaka 60 hadi leo hatuijui historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere wala historia ya TANU.

Kulia ni Mzee Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Mzee Max Mbwana na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi Uchaguzi wa 1962.
Sasa ilikuaje Mwalimu akawazidi wote aliowakuta mjini na waliomtangulia akawa nyota wa mchezo kitaifa na kimataifa!
Kubalini tu yule alikuwa mjanja kuwazidi wengi hadi watoto wa mjini.
 
Mohamed,
Kugombana si lazima kutoleana kauli kali. Unachokiita 'ubaridi' ndio ugomvi wenyewe.
Abdul sykes kujiunga na AMNUT ni kiashirio cha ugomvi. Hivyo ugomvi ulikuwepo

Kwamba Ally Sykes aliktaa kumpa Mwalimu nyaraka za AA na TAA ni kitu kinachojibu aya ya tatu ya bandiko . Kama hakutaka nyaraka zitolewe alihodhi historia na kuipoteza mwenyewe, Buckingham palace wanamsemo '' If it's not documented, it didn't happen''.

Kuhusu Abdul kumpokea Mwalimu lina utata kutoka kwako. Bandiko lako la nyuma umeeleza Nyerere kutambulishwa na.... na kuna siku alilala Temeke.
Kwahiyo si Abdul aliyempokea wala Wazee, Nyerere alikuja Dar kama Mwalimu kutoka Scotland

Utata zaidi ni kwamba Nyerere alikuja mkutano wa chama mwaka 1948 kama katibu wa Tawi la Tabora. Kwa mantiki tayari alishakutana na viongozi wa chama akiwa kiongozi wa Tawi.
Kwamba alikutana na Abdul mwaka 1952! inawezakanaje akutanaye naye mara 2 na mara ya 2 iwe ya kwanza?

Kuhusu katiba kuandikwa au kunukuliwa hili nalo unalitia utata bila sababu.

Ikiwa kuna mtu aliwahi kuandika katiba au kunukuu kwanini huweki wazi?

Kuna msemo kutoka Sandrigham house kwamba '' the end justifies the means'' kwa maana nzuri tu, kwamba, Nyerere ndiye aliona uhitaji wa kitu katiba na kukiingiza katika mfumo wa chama.

Ikiwa kauli hii si kweli,tuonyeshe katiba ya AA au TAA iliyowahi kuwa ya chama.
Hata kama kuna sub committee , committee etc kama hawakuweka wazi, Nyerere anabaki mwandishi '' by default''

Nasisitiza ili kumuondoa Nyerere katika historia ya uandishi , unukuu au utakavyo, tuonyeshe katiba nyingine ya AA , TAA kabla ya Mwalimu, nani aliandika na iliwasilishwa wapi.

Bila hivyo hili halina mjadala '' the end justifies the means' Nyerere ni mwandishi 'by default'

Kusambaza chama. Rejea picha hapo juu na nyingine Nyerere akiwa Mafia.
Ipo video akiwa Lindi n.k.. Chama kilikuwepo, hoja ni kuwa aliyeamsha hamasa ni Nyerere.

Tunarudi kule kule, kama si Nyerere tuonyeshe kiongozi wa makao makuu AA au TAA aliyewahi kufanya ziara kama za Mwalimu na TANU kwa hamasa na uwazi kama Nyerere

Kuhusu EAMWS, hili sijui kwanini unaliongelea.

Nasema hivyo kwasababu ni aibu ''shame on ' wazee wako.

Unanikumbusha kisa cha jamaa aliyefanyiwa 'unyama' na wenzake. Asubuhi alieleza kila mtu
alichotendewa ili kupata sympathy bila kujua alikuwa anaanika '' dirty laundry'' hadharani.

Nyerere kama mtawala wa siasa na kama ilivyo kwa watawala wote ikiwemo viongozi wa dini hawapendi tishio katika kutawala. Kuundwa kwa EAMWS kulikuwa na sababu kuu mbili.
1. Hasira za kudai uhuru na kuachwa nyuma kielimu. Ilikuwa ni AMNUT 2.0

2. Waislam kuziba pengo la elimu lililoletwa na ukoloni.
Mfano, Mohamed Said mwandishi alianza kindergaten kanisani.
Elimu yake ya kati akasoma shule ya mission Dar es Salaam.
Huko Moshi hakukuwa na shule za Waislam, na ndivyo historia ilivyo

Wakati EAMWS inaundwa baraza la TANU lilikuwa na Wazee asilimia 98 Waislam(rejea picha ya Mohamed Said hapo juu). Baraza la TANU liliridhia kuvunjwa kwa EAMWS.

Nyerere alijua EAMWS ilikuwa na nguvu, na alitafuta chombo atakachokidhibiti, BAKWATA

Wazee wa baraza la TANU kwasababu ya kukosa maono, kukosa elimu na ufukara wa kipato wakaukubaliana na wazo hilo, hawakupinga, vinginevyo asilimia 98 ikiwa na 'support mikoani' kama Mohamed Said anavyoonyesha (rejea bandiko na majina ya Waislam hapo juu) Nyerere asingeweza kuvunja EAMWS

Waliokwenda kwa Sheikh Takdir ni Waislam. Waliounga mkono BAKWATA ni Waislam.
Nyerere single handedly asingeweza kuvunja EAMWS na kuwaweka akina Nasib.

Kumlaumu Nyerere ni makosa kwasababu alifanya akijua anafanya nini na alifanikiwa vizuri sana. Kumlaumu ni kuficha ukweli na udhaifu uliokuwepo na uliopo hadi sasa.

BAKWATA ni ile ile ya Nyerere .

Ukiangalia kwa undani factor ni mbili, elimu na ufukara wa kipato unaolazimisha watu kununuliwa kinyume na Imani yao. Haya si maneno mepesi na najua hayatakupendeza, bila kuyasema utakuwa unaidanganya jamii yako na utaendelea kuidanganya kwa kukwepa ukweli.

Narudia tena si maneno mepesi. Kule Windsor castle wanasema '' Call a spade a spade'

Swali unalotakiwa kulifanyia research ni hili, Nyerere aliwezaje' ku- overcome' asilimia 98 Waislam? Jibu lake litasaidia jamii kwa miaka mingi na si kuficha ukweli au kulalama.

Mwisho, kuhusu Nyerere kuingiwa na hofu napenda kukuhakikishia kuwa Nyerere ameshiriki mamb mengi sana ya Tanzania, Africa na Dunia.

Kitabu chako kisingemnyima usingizi.Kilichomsumbua ni upotoshaji akijua kwamba siku atakapokuwa hayupo upotoshaji utaangamiza Taifa.
Nyerere alijali sana Taifa lake kuliko yeye mwenyewe.

Kuandika kitabu kusingejibu hoja ya Tanganyika pekee, Mwalimu angezungumzia ukombozi wa Africa, ugomvi wake na Nkrumah, ushiriki wake wa siasa za kusini mwa Africa, mashariki ya kati , NAM na dunia kwa ujumla. Kuna mambo angeyaeleza yangeligawa Taifa, nitakupa mfano

Nyerere alivunja uhusiano na Israel kwa msingi ya kukiuka haki za binadamu na kuwakandimiza Palestina. Rais Magufuli alirudisha uhusiano huo bila hoja ya msingi.

Tulishuhudia Taifa lilivyogawanyika.
Wapo walioamini Nyerere alikuwa Sahihi kutoka pande zote za mzozo.
Wapo walioamini Magufuli yupo sahihi kutoka pande zote, lakini, suala la Magufuli lilichagizwa sana na hoja ya Udini. Mijadala ikaondoka katika 'core issue' ya uhusiano na Israel ikawa malumbano ya DINI. Hili ndilo Mwalimu alilikwepa, imagine angeweka yote mezani!

Kuweka yote mezani haina maana ya 'ubaya' lakini Wabaya wangeyatengenezea njia, kuyaandikia makala au vitabu kwa mitazamo yao na si uhalisia. Yanatokea sasa seuse angeyaandika.

Masalam

Ngongo JokaKuu Pascal Mayalla
Maelezo yako ni ngumi ya uzito wa heavyweight haswa ila hapo uliposema Mwalimu hakutaka kuweka na ilikuwa sahihi kutoweka mambo yote kwenye maandishi mezani ndipo umeharibu. Ni bora yote yangewekwa katika historia huru na ya wazi tu, yasingetugawa bali yangemulika mwanga mkubwa katika historia yetu.
US historia ya utumwa, ubaguzi na vita vya wenyewe kwa wenyewe imewekwa wazi hadi kwenye shule za msingi na imesaidia kusahihisha na kuliimarisha sana taifa hilo.
 
Sasa ilikuaje Mwalimu akawazidi wote aliowakuta mjini na waliomtangulia akawa nyota wa mchezo kitaifa na kimataifa!
Kubalini tu yule alikuwa mjanja kuwazidi wengi hadi watoto wa mjini.
Yoda,
Mwalimu hakuwa nyota peke yake ukiwa unakusudia kuwa mtu aliyeweza kuongoza harakati za kudai uhuru.

Wewe umemfahamu Mwalimu kwa sifa hiyo kwa kuwa hapakutolewa nafasi ya kueleza historia ya kweli ya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Ikawa kama vile ni mwiko kwa mtu kueleza historia nyingine yeyote ila hii ya Nyerere ya kuwa ni yeye pekee hakuna mwingine.

Wala halikuwa suala la kuwazidi wote.

TAA ilikuwa na watu hodari sana mfano wa Dr. Wilbard Mwnjisi, Dr. Michael Lugazia, Dr. Vedasto Kyaruzi aliyekuwa President wa TAA hata kabla ya Nyerere 1950.

Nafasi ya rais wa TAA kisha kuundwa TANU nafasi hii Abdul Sykes alimkusudia Chief David Kidaha Makwaia wa Siha.

Kisa hiki nimekieleza mara nyingi sana hapa barzani.

Hamza Mwapachu yeye aliona Nyerere anafaa zaidi kwa nafasi hiyo kuliko Chief Kidaha na tangiapo Chief Kidaha hakuonyesha nia ya kuitaka nafasi ile.

Mwapachu alitoa sababu zake za kumtaka Nyerere ashike nafasi ile.

Ni kisa kirefu kina mambo mengi lakini ikutoshe kuwa hata uchaguzi ulipofanyika mwaka wa 1953 kutafuta rais wa TAA kati ya Abdul Sykes na Nyerere, Mwalimu alishinda kwa kura chache na hivyo ile ''inner circle,'' kamati ya ndani ya TAA ilikubaliana Nyerere lazima ashinde uchaguzi ule TANU iundwe mwaka unaofuatia 1954 na Nyerere aongoze mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom