Kwanini benki hakuna vyoo/maliwato kwa ajili ya wateja?

Kwanini benki hakuna vyoo/maliwato kwa ajili ya wateja?

Mkuu ndio maana kuna altenative Chanel Business kama Kutumia ATM, Mobile phone, internet banking n.k... sasa wewe unaona kabisa bank kuna folen halafu unajiunga nayo. tafuta bank ambazo hazina foleni sana. unang'ang'ania banki utafikiri ni mzazi?
unataka kuniambia customer base yote ya bank wanatumia ADC..?, Kuna benki ziko vijijini 70% ya customer wa eneo lile wana smartphone ila hawajui matumizi ya mobile banking utawakataza wasiende ndani kuhudumiwa..?
 
Halaf nilichogundua, kuna watu huwa wanadhani Tanzania ni Dar tu.

Unajua Tanzania ni kubwa sana, kuna maeneo kuna benki moja au mbili tu, hakuna altenative huku, Baclays bank tunaiona kwenye video tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
sehemu kama Nguruka, Kakonko, Namanyere, Ikwiriri wapi utazikuta bank zenye Premium na Executive, bank ni mbili au moja au mawakala tu
 
Huwa nikikuta water dispenser tena iwe ya cool blue nakunywa vijikome 2-3.
Kuhusu vyoo nahisi ni kwa usalama ndiyo maana hawapendi kila mtu atumie vyoo vyao hasa vikiwa vile vya ndani ya benki

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
We want your MONEY, not your [emoji90]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Banki ni sehem ambayo hutakiwi kukaa muda mrefu... ikizidi sana ni dakika tano sasa hiyo haja anaitoa wapi ndani ya dakika tano? ukikaa sana pia si vizuri kiulinzi.
Ukishakuta kuna watu 250 wanasubiri kutoa mishahara yao pale teller na kwenye ATM wapo 50 wengine, ivi utapata huduma kwenye dakika 5?
 
Hapo mwishon umeongea point ya msingi sana mtoa mada yani hua nakereka sana unaenda banki halafu unakutana na mlinzi ana lugha za ovyo ovyo halafu hua wanachukulia kama mteja ni muhalifu wanaboa sana kwakweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walinzi wababe sana kwenye mabanki yaaani kama Mwizi vile kumbe mteja
Hapo Mbagala nilisha ahirisha huduma sababu ya ubabe wa walinzi, nilikua nasoma account numbers kutoka kwenye simu jamaa linaniambia huruhusiwi kutumia simu tukabishana sana ikabidi tu nisepe kwa maudhi yao. Ile bank yenye rangi za chama pendwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom