Kwanini Biblia ilituficha kuhusu uzao wa majitu/Wanefili?

 
Watu wengi sana hii kauli wameisema
Wala haihitaji Roho mtakatifu mimi huwa naipinga sehemu yoyote ile.Haingii akilini eti umepewa kuandika historia ya mtu mashuhuri na muhimu kabisa kama yesu halafu mwisho ulete hoja ya kitoto na kipuuzi tu
 
Wewe upo timamu kichwani kweli ? mbona umejichanganya sana kwenye hii comment yako na swali lako ....kabla sija kusaidia kukujibu nakushauri rudia kusoma tena hivyo vizazi utajua ujinga wako 😁😁😁😁
Sihitaji msaada wako wala sijakuomba unisaide. Ujinga wangu ndo unaonifanya nijue mengi zaidi maana najifunza kila nisichokijua.
 
Reactions: X2Z
Sihitaji msaada wako wala sijakuomba unisaide. Ujinga wangu ndo unaonifanya nijue mengi zaidi maana najifunza kila nisichokijua.
Huo mtiililiko wako umeacha baadhi ya watu ..bila ya kuonyesha matawi ya uzao wao hivyo hapo kuna watu wengi zaidi ya huo mtililiko tumia akili ...maswali yako tuulize sisi wenye kumiliki ubongo wenye qkili
 
Huo mtiililiko wako umeacha baadhi ya watu ..bila ya kuonyesha matawi ya uzao wao hivyo hapo kuna watu wengi zaidi ya huo mtililiko tumia akili ...maswali yako tuulize sisi wenye kumiliki ubongo wenye qkili
Sawa
 
biblia mahaoli flani imeandika wazi haikuandika mambo yote.Na walioandika walifanya hivyo kwa kuvuviwa na Roho mtakatifu mwenyewe.Tunaweza kusema yale Mungu aliyotaka yafunuliwe kwetu ndiyo yaliyofunuliwa
 
Ntajisumbua tu kueleza shika hapohapo unapoamini
 
Ni kazi rahisi kuelewa mtu anayebishana na anayetaka kuelewa mkuu.
Sijakubishia wewe umesema kuwa wanefili waliangamizwa kwenye gharika.Hapo nimekupa aya kabisa inayosema hao wapelelezi wali waona hao wanefili(wana wa anaki) Walichofanya kalebu na joshua ni kuwaondoa hofu wana israel Maana waliamini uwezo wa Mungu.

Kitabu cha torati kimewataja pia ni kakupa mfano mwingine wa Goliathi hakuwa binadamu wa kawaida. Sasa ubishi wangu upo wapi na nimekupa hadi maandiko ambayo ni miaka mamia baada ya gharika.

@
 
Niishie tu kusema Mariam alizaa watoto wengine pamoja na mumewe Yusufu. Ni wale wote wanaosemwa ndugu za Yesu, Yakobo na wenzie
 
Goliathi hakuwa mmoja wa wanefili ila ni kweli alikuwa mtu mwenye kimo kirefu na nguvu kuzidi wanadamu wengi. Vivyo hivyo kwa wana Anaki walikuwa ni binadamu wenye nguvu ambao baadaye Yoshua alikuja kuteketeza kizazi Chao.

Wanefili ilikuwa ngumu kushindwa kwa nguvu za kawaida za kibidamu. Uhalifu ulizidi ndio maana Mungu akaingilia kati. Watu warefu na majitu yenye nguvu hata leo wapo ila sio wanefili
 
Ukisoma baadhi ya biblia wameandikwa wanefili wala sio wana anaki.


PIA SOMA HAPA KUTOKA Robert Heriel Mtibeli

PROPAGANDA ZA KUKUZA UWEZO WA RWANDA KIJESHI ZINAHATARISHA USALAMA WA NCHI YETU HAPO BAADAYE.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kuna tabia ambayo imekomaa miongoni mwa watu ya kuisifia, kuitukuza, kuipamba, kuipa uwezo hata usiofaa nchi ya Rwanda katika sekta mbalimbali. Na Leo nitajikita kwenye sekta ya Ulinzi na usalama na hapa tunazungumzia Jeshi na Mbinu za kimedani.

Kwa Sisi Watibeli, Jeshi sio kuwa na watu wengi.
Jeshi sio kuwa na vifaa vya kisasa na vya kiteknolojia.
Jeshi sio ukubwa wa Miili au maumbile.
Jeshi sio kuwa na uchumi Mkubwa.

Jeshi ni zaidi ya hayo. Hayo ni Mambo madogo Sana Jeshini na yanatokea Nje ya Mwanajeshi.
Uanajeshi ni lazima uanzie ndani ya mwanajeshi mwenyewe.

Jeshi ni Mtazamo
Jeshi ni Imani
Jeshi ni Nidhamu
Jeshi ni Moyo wa Ujasiri
Hayo yote yapo ndani ya mwanajeshi. Mwanajeshi ili awe Mwanajeshi lazima awe na hayo Kwanza ndipo mafunzo, silaha, Mbinu n.k. ndio apewe.

Kwa namna hiyo Basi, utagundua lengo kubwa la Propaganda ni kuangusha ujasiri, Imani, mtazamo wa Mwanajeshi husika au jeshi husika katika upambanaji.

Kwa Sisi Wasomi wa Bibilia, Moja ya mambo makubwa ambayo yanajitokeza tokeza katika visa vya Biblia ni Propaganda ya kuwapa Waisrael Ujasiri, Imani, na mtazamo Chanya kuwa wao ni Bora kuliko watu wote Duniani.
Kisha ndipo Sheria za Torati zinawekwa ili kuwafanya wawe na Nidhamu.

Zipo Makumi ya aya zinazoeleza kuwa Muisrael Mmoja atakimbiza watu Mia WA mataifa mengine. Hiyo ni propaganda

Kuna kisa kingine ambacho Musa aliagiza Wapelelezi Kumi na mbili Kwenda kuipeleleza Nchi ya Kanaani. Wapelelezi wale Kumi na mbili waliporudisha ripoti. Wapelelezi Kumi wakatoa ripoti Yao kuelezea Jinsi nchi Ile ilivyo na watu wake walivyo Wakubwa na wenye nguvu na hodari. Kwa jinsi walivyokuwa wanaoelezea ni Kwa namna ya kuwakatisha tamaa na kuwatisha waisrael Jambo ambalo ni Kweli Waisrael waliingiwa na Hofu.

Lakini kwa Bahati, wapelelezi Wawili ambao ni Joshua na Kalebu wao wakatoa ripoti Yao inayokinzana na ripoti ya wale wapelelezi kumi. Wao wakasema in a positive ways.
Kusifia nchi wanayoiendea(Lengo Lao), kusifia Jeshi lao na Waisrael kwa ujumla, na mwisho kueleza sifa za maumbile ya adui Zao in a negative ways.
Wakasema, ni kweli wale watu ni Wakubwa Sana, wanamiili Mikubwa Mno na nguvu za Kimwili, lakini mioyoni mwao wanahofu juu yetu. Mambo makubwa tuliyoyafanya kuanzia kwa Farao, bahari ya shamu na kupiga mataifa yote tuliyokutana nayo imewanyong'onyesha Sana.
Hivyo waisrael na Jeshi la Israel Halina Sababu ya kuogopa watu hao kwani ni ukubwa wa Pua tuu ambao haulingani na wingi wa makamasi.

Ari, ujasiri, imani kwa Waisrael na Jeshi lao ikarejea lakini Musa kama kiongozi wa kijeshi na mwenye hiyo Movement akatoa maamuzi wale wapelelezi kumi wauawe ili wasije waletea Hofu na kuambukiza Hofu hiyo watu wengine.

Muhtasari huo tunajifunza mambo mengi lakini kubwa zaidi linaloendana na Mada hii ni nguvu ya propaganda na maneno katika Ulinzi na usalama na wanajeshi wetu.

Jeshi imara linatokana na wananchi imara.

Hawa watu wanaendesha propaganda za kuishusha nchi yetu na kuidunisha hasa kijeshi(kiulinzi na KIUSALAMA), sio tuu wanatukosea Bali wanahatarisha usalama wa nchi kwa wakati ujao.

Kama ikiendelea hivi itajengeka dhana kwenye jamii yetu kuwa Warwanda ni watu hodari kuliko Sisi. Sisi ni Duni mbele ya Warwanda Jambo ambalo ni Uongo lakini likiendelea litafanya mitazamo ya Watanzania kuligeuza Jambo hilo ni KWELI.

Hawahawa wananchi ndio baadaye watajiunga na Jeshi. Yaani watu wenye kujiona Duni na hofu dhidi ya Warwanda ndio watakuwa wanajeshi hata ikitokea vita watakuwa waoga na kushindwa mbele za adui Zao Warwanda.

Nini chakufanya?

1. Kitengo cha Propaganda hasa za kijeshi kisilale. Kijiimarishe na kuweka mipango na mikakati kufanya Watanzania waliamini Jeshi Lao.
Kwa sababu Jeshi likianza kutiliwa Mashaka hata ufanisi wake utapungua.
Kwa USA na mataifa mengine tunaona wo vitengo vya propaganda viko kila idea, huko Hollywood kwenye Filamu, kwenye Masuala ya kisayansi, na mambo ya Waandishi wa riwaya na tamthilia.
Kwamba ati Mwanajeshi Mmoja wa kimarekani anaweza kushughulikia maadui Mia moja wa mataifa mengine

2. Kutokana na baadhi ya watu kutokuwa na Akili au kuwa na chuki na nchi. Iundwe Sheria za kuzuia watu kuzungumzia mambo ya kijeshi na kiusalama kwa namna ya kudhalilisha, kumshusha heshima ya jeshi, kukejeli, kushusha morali au kudunisha.
Hii itaepusha na kuzuia wale wapiga propaganda zenye maudhui ya kudunisha Jeshi la nchi.

3. Watu wapewe uwezo wa kutoa maoni Yao lakini yawe maoni ya kujenga sio yenye lengo la kutukuza taifa jingine kuliko taifa kwa namna ya kukejeli taifa letu.

4. Mafunzo ya JKT yaendelee kutolewa kwa wanaomaliza kidato cha sita na kwa wale Wa kidato cha nne ambao wataendelea na vyuo vya Kati.

Ninawahakikishia, Maneno haya yakiendelea hivihivi watu na jamii itayaamini. Na matokeo ya kuyaamini Maneno ya aina hii hayatakuwa mazuri.

Lazima Sisi kama taifa tujitambulishe sio tuu kwa upendo wetu, umoja wetu Bali pia tujitambulishe kama watu wenye AKILI kubwa, na watu wenye kufanya mambo magumu.

Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato
 
hatupo kubishana kabisa mkuu hii sio siasa ni kweli unaweza ukawa sahihi kwa100% na usiwe sahihi pia kulingana na unachokiamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…