Kwanini CCM imejitenga na msiba wa Profesa Sarungi??

Kwanini CCM imejitenga na msiba wa Profesa Sarungi??

Maria ni Maria ana mamlaka na utashi wake Binafsi na Mzee Sarungi ni mwana CCM. Kwa iyo ya Maria yaachwe Kwa Maria kwani Maria ni mtu mzima na Marehemu Sarungi asingeweza kumwamuru Kwa lolote lile
Maria hajawahi kumtukuna Samia bali anamkosoa. Kama rais hana uwezo wa kuongoza na akatokea raia wake akasema kuwa hafai, hilo siyo tusi.
 
Prof. Sarungi amelitumika taifa hili ktk ngazi na nyadhifa mbalimbali.
1. Amekuwa daktari bingwa wa mifupa.
2. Amekuwa mbunge na waziri ktk wizara tofauti.
3. Amekuwa RC ktk mikoa tofauti.
4. Amekuwa mwanachama wa ccm mtiifu ktk uhai wake wote.

Ni kwann serikali inayoongozwa na Samia imejitenga na msiba huu mkubwa wa prof. Sarungi?
Watakuambia hawajapata mualiko
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Watu wengi wanapenda kufanya siasa za mihemko na za maji taka mpaka kwenye misiba.

Profesa hata hajazikwa, msiba unasubiri ndugu warudi, wapambe washasema CCM imeutenga msiba.

Tumuheshimu huyu Mzee jamani, kwa nini watu wanataka kupenyeza siasa kwwnye msiba wake?
Inawezekana watu wanatumia uzoefu wa misiba mingine punde ilipotokea hali ilikuwaje na wanaona mambo yanaenda tofauti kwa mzee wetu ukizingatia leo ni siku ys tatu.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Kwani Samia ni lazima ajihusishe na kila msiba?

Mbona kama mnataka kumpa umuhimu ambao hana?

Una hakika familia ya Sarungi inataka rais Samia ajihusishe na msiba wao?
Dah!
 
Kwa hiyo unataka kusema huyu Professor ambae mwanae anshinda mitandaoni kumktukana Rais usiku mchana unaona ulikuwa ni sahihi? SSH nae ni binadamu pia ,hata ungekuwa ni wewe matusi ya mariah sarungi hayavumiliki
kila nafsi ihukumiwe kivyake, kama ni hivyo raisi na ccm ni dhaifu sana, sarungi atazikwa hata na watu wakawaida ila ccm na raisi wataonekana maadui kwa taifa na familia
 
Kwani huyo Mungu wenu wa kike ataishi milele?
Issue siyo mungu ila tanzaniani nchi yetu wote na yule ni raisi wetu kuna kukosoa , kutukana , kudhalilisha na kufitinisha hivyo ni vitu tofauti lazima ujue tofauti yake
Unapotukana na kudhalilisha nchi au taasisi ya raisi hilo siyo sawa, hata aje raisi gani mapungufu na kukosolewa kupo ila siyo kutukana na kudhalilisha
 
Sijaona Maria akitukana serikali zaidi ya kuongoza mijadala,Je Mtoto Ndio afanye kazi ya baba yake ipuuzwe? Tena mtoto aliezidi miaka 18 na ana familia yake?
Mi nimeona mara nyingi tu akitukana na kudhalilisha hata taasisi ya raisi
 
Profesa Sarungi hakuwa mtu wa hivihivi tu. Kinachotushangaza ni ukimya wa baadhi ya viongozi wakubwa akiwemo Rais kwenye msiba huu. Hawalazimiki kufanya chochote lakini kwa utamaduni wetu hata salamu tu ya rambirambi ingetosha. Watu wanatoa pole kwa vifo vya wasanii na kwa watu wa nje lakini siyo kwa kiongozi mstaafu aliyeacha alama kubwa kwenye taifa hili. Inshashangaza sana. Hawalazimiki ila tunawashangaa tu. Yote haya ni kwasababu mtoto wa marehemu anaikosoa serikali?
Kumbe watu wanabeba hasira na chuki vifuniani mwao hata wakati wa mwezi huu mtukufu.
Hata Taasisi ya mifupa (MOI) aliyoingoza kwa muda tu wanakuwa wana kigugumizi Cha kutoa hata pole kwenye page yao kisa Maria Sarungi.
 
Mimi naomba kujua wenye kujua uyu Maria ikiwa ametukana au anatukana oky. Nataka kujuq Mzee Profesa Sarungi amewai kumkemea mtoto wake adhalani kupitia Media???????

Sababu nakumbuka karume ashawai mkemea mtoto wake.

Uyu Profesa kwenye Uhai wake aliwai kutoa neno kuusu mtoto wake??? Kabla Sijatoa maoni yangu.!!!!
 
Prof. Sarungi amelitumika taifa hili ktk ngazi na nyadhifa mbalimbali.
1. Amekuwa daktari bingwa wa mifupa.
2. Amekuwa mbunge na waziri ktk wizara tofauti.
3. Amekuwa RC ktk mikoa tofauti.
4. Amekuwa mwanachama wa ccm mtiifu ktk uhai wake wote.

Ni kwann serikali inayoongozwa na Samia imejitenga na msiba huu mkubwa wa prof. Sarungi?
Mbona me nilifiwa CCM ikanitenga sijalalamika binadamu wote sawa hata ww utatengwa kama hujitambui
 
Inawezekana watu wanatumia uzoefu wa misiba mingine punde ilipotokea hali ilikuwaje na wanaona mambo yanaenda tofauti kwa mzee wetu ukizingatia leo ni siku ys tatu.
Watu wanampa rais nguvu asizokuwa nazo. Vivyo hivyo kwa chama na serikali.

Profesa Sarungi mtu wa watu, kaishi na watu vizuri, ana familia kubwa.

Mfano asipotokea mtu yeyote wa serikali wala chama kumzika, yeye Profesa atapungukiwa nini? Familia yake itapungukiwa nimi?

Kwa nini tunaifanya serikali na rais kama ni vitu gulani vyenye umuhimu ambao havina?

Mbona hatusemi uongozi wa Simba haujatokea kumzika Mzee wao aliyekuwa shabiki mkubwa sana wa Simba?

Kwangu mimi uwepo wa Simba kwenye msiba ni muhimu kuliko uwepo wa serikali.

From Mo Dewji.

"Mohammed Dewji
Owner & President | MeTL Group

Tanzania has lost an exceptional leader, and I have lost a dear friend. Professor Philemon Sarungi was not only a distinguished surgeon and statesman but also a devoted member of the Simba Sports Club family.

His passion for the club ran deep—he was a loyal supporter who championed Simba’s growth and success. As the Director-General of Muhimbili National Hospital, he ensured that Simba players received the best medical care whenever they needed treatment, always looking after their well-being. His dedication to the club was above and beyond—he truly cared for the players, their welfare, and the club’s legacy. His dedication was recognized when I had the honor of presenting him with the Simba Lifetime Achievement Award, a well-deserved tribute to his lasting impact on the club.

Beyond football, Prof. Sarungi was a towering figure in Tanzania’s healthcare and public service sectors. A highly skilled surgeon and educator, he shaped the country’s medical field and later served in key ministerial roles, including Health, Education, Transport, and Defense. His contributions to the nation were profound, leaving a legacy of excellence, leadership, and service.

His loss is deeply felt, but his influence will live on. May his soul rest in eternal peace 🙏🏽"
 
Sijaona Maria akitukana serikali zaidi ya kuongoza mijadala,Je Mtoto Ndio afanye kazi ya baba yake ipuuzwe? Tena mtoto aliezidi miaka 18 na ana familia yake?
Marehemu hahitaji kutembelewa msibani,kuzikwa,hayo ni mahitaji ya walio hai,sasa Maria anahitaji kutembelewa zaidi kuliko sarungi,ye ndiyo anafeel the pain
 
Bora tuwe na katiba kama wenzetu Wakenya kuna freedom of Speech,Ruto anatukanwa mtandaoni kila siku lakini yeye anaendea kupiga kazi licha ya upinzani mkubwa unaomtikisa, hapa kwetu duuuh
 
Dah vipi mkuu?

Watanzania wanapanga nani aende kwenye msiba wa nani kama wanajua mahusiano ya watu vile.

Kwa mtaji huu, wanaweza kulazimisha kitu ambacho marehemu hakukitaka.

Si kila mtu anataka kuzikwa na wanasiasa.
 
Back
Top Bottom