Kwanini Chadema wanaamini wazungu kwenye harakati zao za kisiasa?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance aliinyooshea kidole Ulaya kuwa haina demokrasia kwa watu wao wenyewe. Wakati huohuo bunge la Ulaya linainyooshea vidole Africa kuwa hakuna demokrasia.

Nimemsikia Tundu Lissu akidai kesi yake iliyoko mahakamani ifutwe kwakuwa dunia inatuangalia (the world is watching)kwa jicho baya. Anasema Tanzania inachafuliwa na kesi yake. Yaani watanzania 65,000,000 wanachafuliwa na Lissu kuwa mahabusu. Tena wanachafuka huko Ulaya.

Wazungu watakuwa wapumbavu kama wanaiona Tanzania kama nchi inayochafuka kwakuwa Lissu ameashitakiwa mahakamani na kesi inaendelea kusikilizwa, ila Marekani haikuchafuka wakati Trump alipokuwa na msululu wa kesi zinazomkabili.

Chadema wanapush hard wazungu watuadhibu kama vile wazungu ndio wanaodhamini harakati zao za kuelekea Ikulu.
 
Wazungu walitutawala na lugha yao ndo tunaitumia kwenye mambo yetu mengi ikiwemo sheria zinazotuongoza.
Mpaka fedha ya uchaguzi wazungu wameombwa kutupiga tafu,hivyo ni desturi yetu watanzania kuwaamini wazungu,chadema wako sahihi.
 

..wazungu ndio wanawaweka Ccm na serikali mjini.

..hukuona hata Kagame na Tshisekedi, walipuuza usuluhushi wa, Sadc, na Eac, wameenda kusuluhishwa na Marekani?

..Waafrika wangekuwa wanaheshimika na watawala wetu Chadema wangetafuta kuungwa mkono na nchi za Afrika.
 
Wazungu walitutawala na lugha yao ndo tunaitumia kwenye mambo yetu mengi ikiwemo sheria zinazotuongoza.
Mpaka fedha ya uchaguzi wazungu wameombwa kutupiga tafu,hivyo ni desturi yetu watanzania kuwaamini wazungu,chadema wako sahihi.
Tuache kufuata sheria zetu kwakuwa the world is watching? Yaani baraza la Ulaya lituangalie sisi na kuacha kuiangalia Cameron ambako Rais Paul yuko madarakani kwa miaka 43 Sasa, iache kuangalia Uganda na Rwanda ambako hakuna vyama vya upinzani kabisaa,.
 
Wazungu walitutawala na lugha yao ndo tunaitumia kwenye mambo yetu mengi ikiwemo sheria zinazotuongoza.
Mpaka fedha ya uchaguzi wazungu wameombwa kutupiga tafu,hivyo ni desturi yetu watanzania kuwaamini wazungu,chadema wako sahihi.
Kama Hawa wakoloni weusi wamekuwa mashetani tunawarudia wale weupe!
 
Kwasababu wazungu wamewapa hifadhi nje ya nchi familia zao kwahiyo wanataka kulipa fadhila wakishika madaraka
 
Mnafuata sheria zenu zipi zinazotaka mtuhumiwa awekwe gerezani kwanza ndipo muanze kutafuta ushahidi wa makosa yake?
 
Kwasababu wazungu wamewapa hifadhi nje ya nchi familia zao kwahiyo wanataka kulipa fadhila wakishika madaraka

..wazungu ndio wanaotoa misaada na mikopo kwa serikali ya Ccm.

..kwasababu hiyo Ccm inaheshimu na kusikiliza wazungu kuliko wananchi wa Tanzania.

..hivyo basi kama Chadema wana malalamiko dhidi ya Ccm ni lazima waende wakashtaki kwa wazungu.
 
Hangaika uwezavyo ,lakini Wazungu hawajawahi kushindwa kitu. Take it from me Tanzania tupende tusipende lazima TUNDU Lissu aachiwe na turekebishe SHERIA za uchaguzi ili CHADEMA ishiriki. Vinginevyo kilio hakiko mbali.
 
Nje ya topic; naomba kuuliza, James Delicious alichukua form ya kugombe ubunge kupitia ccm, wajumbe wamempa KURA kiasi gani? Hongera sana ccm kwa demokrasia, kweli chama hakina ubaguzi
 
Tahira hivi nyinyi matahira mnafikiri ccm ikifa na nyie mtakufa maana sio ujinga huu.
 
Unaota ndoto za alinacha uzeeni. Eti Chadema wanategemea Ulaya, kwani CCM wanategemea wapi? Hao Waarabu wa UAE, Qatar, na Saudi? Kwa nini hamuategemei Syria, Yemeni, Irani, au Lebanon? Ni kwa sababu UAE, Qtar, Bahrain, Kuwait , Saudi hao wanaheshimu sana Wazungu ndiyo existence yapo iona. Wale wabishi wote si umeona juzi Irani (ingawa hii siyo nchi ya Kiarabu) ilivyosambaratishwa (ingawa sifurahi), Lebanoni nk. UAE, Qatar, Saudi wote kicheko, maana ndiyo Usalama wao. Sasa watu kama nyie, kwa sababu ya hizo satanic verses mnaanza upuuzi ati utambishia nani. Anza kwanza kujilisha, kujinunulia chupi unayovaa, na shati unayovaa ndiyo uanze matusi. UAE, Saudi, Qatar, Kuwait umewahi kumskia anamtukana mzungu? Paka.

Kwa sasa ni umalay tu, ati mtamgeukia Mchina au Mrusi, kaangalie Zimbabwe, Yemeni, Irani, standard zote zimeshuka, kwa sababu mchina naye masikini kama wewe, haji burebure ni kama kwavi.

So far Chadema are on the right track
 
Jikite kwenye kiini, justification ya kesi husika na si kutafuta cheap excuse eti Wazungu hivi mara Wazungu vile. Linapokuja suala la Wazungu kukupangia ukumbuke loans na grants huwa zina strings attached lakini mengi ya behind the scenes hufichwa, bila hiyo nguvu hakuna ambaye angekuwa na guts kuingilia mambo ya ndani ya nchi yoyote. Mkiweza kujitegemea fully(of which I don't see how) hakuna mtu yoyote atakaye thubutu kuingilia internal affairs zenu, viongozi wenu wanaongea blah blahs nyingi za kujitutumua lakini wakikutana na hao Wazungu behind closed doors wanawalamba miguu na kulialia wakiomba kusaidiwa. Misaada mnayoiona/mnayoisikia ni baada ya viongozi kulialia sana wakiiomba ili angalau mifumo iweze kuendeshwa na watu waamini kuwa it's a smooth ride.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…