Kwanini CHADEMA wanawatukana sana watu wa kanda ya ziwa na kuwaita Sukuma gang?

Kwanini CHADEMA wanawatukana sana watu wa kanda ya ziwa na kuwaita Sukuma gang?

Dunia inaenda kwa haraka sana. Na mambo yaenda kwa kasi sana.

Tangu mwaka 2019 CHADEMA imekuwa na msemo wa kuwaita watu wa kanda ya ziwa sukuma gang.

Nimekuwa na jiuliza kwa muda mrefu sana ni nini sababu ya hawa watu kuwaita watanzania wenzao majina yenye kuashiria kutugawa watanzania? Mpaka leo natafuta kujua hawa CHADEMA wapo na lengo gani na jambo hili?

Maana ukipitia kwenye mitandao ya kijamii taarifa nyingi wanazieneza na kuwatusi watanzania wa kanda ya ziwa. Sujui lengo kubwa ni nini?
View attachment 2486017

Sasa nawaombeni wenzangu humu JF tujadili suala hili tulimalize. Hawa CHADEMA lengo lao ni nini kuanza kuwasakama watu wa kanda ya ziwa?
sisi kama wasukuma tunawubiri 2025 kama kawaida kampeni ni kisukuma tu, ili Sukuma gang ieleweke vizuri
 
Usifikiri Wasukuma ni wajinga hawaelewi huu mchezo wako wa kijinga kutaka kutumia kabila lao kwa malengo yako ya kipumbavu. Humpati mtu utabaki na hao wajinga wajinga wenzako masalia ya yule Mhutu dhalim.
Jamani kuuliza swali unaanza kubwatuka hivi. Kama hujui jawabu lake waache wenzako CHADEMA wanajawabu lake.
 
Kama siyo jamii nzima ya wasukuma ni jamii ipi ya wasukuma? Na kwanini sasa mfanye hivyo. Huoni kuwa mnawachafua wasukuma kwa ujumla wao? Je, nyie CHADEMA wasukuma wamewakosea nini?

Kwasababu Mbowe ni mchaga tuwaite Chaga gang mtafurahi?

..ukisema ITALIAN MAFIA walengwa sio Waitaliano wote.

..vivyo hivyo SukumaGang walengwa sio Wasukuma wote.

..pia ChagaGang haimaanishi Wachaga wote.

..MsogaGang haimaanishi kila mtu anayeishi au anayetokea Msoga.
 
Ni tusi kubwa mno. Yaani unawaita wasukuma kuwa ni majambazi.
Kumbe hujui maana ya gang.
.
Screenshot_20230118-174753_Chrome.jpg
 
..ukisema ITALIAN MAFIA walengwa sio Waitaliano wote...
Sasa hizo gang zingine hazipo. Umeziweka wewe.

Hapa tunaongelea jambo ambalo lipo. Tena jambo hilo ni ovu na la kutubagua watanzania.

Tunaongelea mnapo waita wasukuma kuwa sukuma gang maana yake ni nini? CHADEMA nipeni jawabu.
 
Sasa hizo gang zingine hazipo. Umeziweka wewe. Hapa tunaongelea jambo ambalo lipo. Tena jambo hilo ni ovu na la kutubagua watanzania.

Tunaongelea mnapo waita wasukuma kuwa sukuma gang maana yake ni nini? CHADEMA nipeni jawabu.

..wabaguzi ni hao SukumaGang waliokuwa wakifanya siasa za kikabila bila haya mpaka wanahutubia kwa kilugha ktk sherehe za uhuru wa Tanganyika.
 
..wabaguzi ni hao SukumaGang waliokuwa wakifanya siasa za kikabila bila haya mpaka wanahutubia kwa kilugha ktk sherehe za uhuru wa Tanganyika.
Kwahiyo ndio sababu yenu kuanza kuwaita wasukuma kuwa ni kundi la harifu? Nyie CHADEMA, mnatafuta sababu za kuwachafua wasukuma. Sababu zenu ni mfu kabisa.
 
Mods mna ushirika na CCM kuigombanisha Chadema na Wasukuma.

Asubuhi kuna mshirika wenu mwingine alianzisha uzi wa kuigombanisha Chadema na KKKT.

Nina uhakika mnazisoma na mnajua kabisa kuwa huu ni uchochezi lakini kwa kuwa inayohujumiwa ni Chadema mumeuchuna tu,this is not fair
 
It has more just one meaning, lakini kwangu binafsi Sukuma gang ni kikundi cha criminals na mifano ni Sabaya, Bashite, wale waliommiminia risasi Lissu, wewe mwenyewe unayelalamika hapa JF pamoja na kundi lote la wasiojulikana.
Hiyo mifano haiondoi maana ya walengwa kuwa walikuwa ni wasukuma. Yaani wasukuma wasipate mafasi yoyote ya kazi maana mmeshawati kuwa ni majambazi.

Inauma sana kuanza kuwabagua watanzania kwa makabila yao.
 
Back
Top Bottom