Mkuu Enisekolopedia Buritanica, bandiko lako kiukweli limenigusa!, ni kweli tulipopata uhuru, Kagera ilikuwa ni miongoni mwa mikoa mitatu yenye uchumi imara!, ila uoimara huo ulitokana na wavumbuzi waliogundua mikoa hiyo kahawa inastawi, hivyo misheni zikajenga shule, Wahaya na Wachanga mkasoma sana kwa sababu wazazi wenu walikuwa na fedha za kahawa kuwalipia ada!. Wakuloni wakawadekeza sana na kuwanyenyekea hali iliyopelekea kuwa ni watu mnaojisikia sana na kujiona bora kuliko wengine!, ingawa nakiri Wahaya na Wachaga kuwa na akili sana, ila pia wanawake wenu ni wazuri!, Wachagga wazuri wa kutazama, na Wahaya ..usiseme!.
1. VITA YA KAGERA, 1978/79
Hii vita ilikuwa ni vita ya nchi nzima japo ilipiganwa kwenye mkoa mmoja wa Kagera na kuharibu baadhi ya miundombinu ya Masaka, daraja la Mto Kagera na kule Mtukula yote, Bukoba haikuguswa!, usitake kusingizia vita, Watanzania wote tulichangia na mikanda ya miezi 18 wote tulikaza nchi nzima!. Kitu ambacho nakubaliana na wewe, baada ya vita, reparations zililipwa na Libya na Uganda lakini hazikulipwa kufanya restorations, lakini hii sio sababu!.
2. JANGA LA UKIMWI 1983,
Sii kweli kuwa UKIMWI umeanzia Uganda, bali ulisambaa kwa kasi zaidi Uganda na Kagera sio kwa sababu ya utaratibu wa kufanya Biashara na Uganda, no way, ulisambaa kwa kasi kwa sababu ya zile tabia zetu, kwenye yale mambo!, kama hoja ni biashara, Uganda inafanya biashara kubwa zaidi na Kenya kuliko na Kagera!. Janga la UKIMWI, limepoteza nguvu Kazi kubwa sehemu nyingi, nenda kaangalie yatima wa Makete ulinganishe na hao wa Kagera!, hivyo hii sio sababu!.
3. AJALI YA MV BUKOBA
Japo hili janga lakini sii kweli limechangia kudhoofisha mkoa wa Kagera kwa sababu waliopoteza maisha sio watu wengi kivile!, kila siku ugonjwa wa malaria unaua watu wengi kuliko hata ukimwi, hiyo ajali imepoteza nguvu kazi gani kivile kuutia umasikini mkoa wote!. Hii sii sababu!.
4.1998 EL NINO
Sikweli kuwa Elnino imeathiri sana kanda ya ziwa kuliko kanda yoyote ile hapa nchini, El nino imeharibu miundombinu na ya maeneo mengi, imezoa mazao maeneo mengi, na kupoteza wazalishaji na uzalishaji mali, lakini sio sababu!.
5. KUSHUKA KWA BEI YA KAHAWA 1998 KWA UZEMBE WA SERIKALI.
Ni kweli Kagera ilitegemea sana Kahawa kama kitega uchumi chake kikuu, ila sii kweli kuwa ni uzembe wa serikali uliosababisha kushuka kwa bei ya kahawa, kwa kuhakikisha Kahawa inabaki na bei ya juu kwa sababu kushuka huko ni kwenye soko la dunia, ambako Tanzania sii mzalishaji pekee, hivyo hawezi kupanga bei, kumejitokeza wazalishaji wengi zaidi wa kahawa ambao wanazalisha kahawa boa zaidi kwa bei nzuri zaidi, ila pia hii sio sababu, kwa sababu hata Kilimanjaro ingeathirika!, na sii bei ya kahawa pekee, bei ya pamba imeshuka, bei ya katani imeshuka, bdei ya korosho imeshuka, bei ya chai imeshuka, bei ya pareto imeshuka, sasa why Kagea tuu?!.
6. UBAGUZI ULIOJIFICHA TOKA KWA VIONGOZI ( INDIRECT DISCRIMINATION TOWARDS HAYA TRIBE)
Sii kweli kuwa Wahaya waliwekewa mizengwe katika baadhi ya sekta, hata kwenye elimu , na japo ni kweli, walipandishiwa alama za ufaulu sio ili wachache waendelee na elimu ya juu, bali kuwazuia ku dorminate elimu zote za juu nchi nzima!, na sii Wahaya pekee waliopandishiwa, hata Wachagga. Hili lilifanywa na Mwalimu Nyerere, kufuatia mikoa hii kuwa na fedha kutokana na kahawa, wazazi wote waliweza kusomesha hivyo shule za sekondari zote zilijaa makabila mawili, ndipo cut off point ikapandisha ili Watanzania wengine nao wapate fursa, bila hivi, kina Magufuli wangeishia kuchunga mbuzi, kina Kikwete wangeishia kuvua samaki, na kina Mkapa wangeishia kuokota korosha na kuvuna chamaki nchanga!.
7. KUTENGWA NA NCHI KIJIOGRAFIA
Kagera iko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, waliowahi kufika uko ndio wanaelewa namaanisha nini, Kagera imekuwa kama kisiwa maana jinsi ya kufika kule inabidi ukatishe kilometer kadhaa za msitu, ili uingie Kagera, au upite ziwani kwa meli ndio uende mikoa mingineyo ambayo ni ya Tanzania, hivyo basi wana Kagera walikuwa na urahisi wa kufanya Biashara na Uganda kuliko mikoa mingine ya Tanzania, lakini serikali ilikataza biashara hiyo , wakajikuta wamebaki kama kisiwa ndani ya nchi yao wenyewe, hii ni kweli, ila pia histoia hiyo hiyo inaonyesha Kagera ilikuwa chini ya ufalme wa Bunyoro!, ni wakoloni tuu ndio waliiacha upande wetu, ila kiukweli Wahaya ni watu wa kule kitabia, maneno, lugha hadi matendo!.
8.KAGERA KIMBILIO LA WAKIMBIZI MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA 1994 NA MACHAFUKO TANAYOENDELEA UKANDA ULE.
Wanyarwanda wameiteka Kagera hasa wilaya ya Karagwe na Muleba na kujichukulia ardhi , pia wamekuwa watekaji wa magari na kudhalilisha wana kagera , kitu amabacho kimerudisha nyuma uchumi wa mkoa, kwa kasi, majambazi wametamalaki na kufanya uharamia ambao umefanya kusiwepo hali ya utulivu na kujenga uchumi, serikali imechelewa kuchukua hatua, hili pia ni kweli ila sio sababu, kwa sababu wakimbizi pia wametawanywa sehemu mbalimbali na wamechangia katika kudumaza maendeleo ila sio sababu!.
9. KUTOJUMUISHWA KATIKA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO KIKANDA
Kila kanda imetengwa katika kanda fulani ya mkakati wa maendeleo lakini kanda ya ziwa ambayo ndipo kuna mkoa Kagera hakuna ilipoainishwa katika mpango wa maendeleo.Kagera Umekuwa ni mkoa wa kujitegemea kwa kila kitu ni kweli, na sababu ni zile nilizokupa, you don't belong here, you belong there!. Ndio maana hata ile barabara, ilikuwa ipite Biharamulo, Magufuli akaichepusha ikapita Chato!. Poleni!
Taarifa hii kumhusu Kato, ni taarifa muhimu sana, kwa sababu Kato japo anajulikana ni mtu wa kule, ila anatabia za ajabu ajabu kama za watu wenu, kiasi cha kutufanya wengine wetu tuhoji asili yake ni wapi haswa, wazazi wake asili yao ni wapi?, jee ni watu wa kule kweli au ni wahamiaji tuu, na jee huyo ni mtoto wa familia hiyo kweli au ni wale wakuja tuu?!.
Sisi babu yetu mzaa babu alikuwa tajiri wa ng'ombe, mchunga ngombe wake alikuwa Mtusi, alipofariki, babu akawachukua watoto wake akawafanya ni ndugu zetu mpaka leo wamekuwa ni ndugu kabisa hawapajua tena kwao zaidi ya kwetu, na ni wenzetu kabisa, ila asili yao ni ile ile ya walikozaliwa na sio walikokulia!. Kabila letu tunapenda sana watoto na tuna asili ya wanawake wengi!, kwetu haijalishi ujauzito ni wa nani, ila watoto wote ni wa kwetu!.
Tuhadithie zaidi kuhusu huyu Kato wa kwa Mzee Machalila, huyo Mzee Machalila yupo, watu tufunge safari kuchimbua historia halisi ya Kato?!.
Pasco