DR.RWEYENDERA
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 403
- 386
Pasco we huyaelewi mambo ya kagera na pengine sina hakika na umri wako usingecomment ulivyocomment kama huna uhakika si unakaa kimya,Mkuu Britanicca, sisi Watanzania tuna tatizo kubwa sana la kutopenda kuambiwa ukweli, na mtu ukiwa mkweli daima ni problem, na hili ndilo tatizo langu pekee!, umekuja na maelezo marefu sana kuhusu Kagera, na ukayaweka in point format ili watakaokujibu, wasikujibu in blanket statement, umeweka points zako nimepangua moja baada ya nyingine!.
1. Kuna mkazi wa Mara au mtwara au kigoma ambaye si mwanajeshi na mzalishaji alikufa tokana na vita ile? Hivohivo jiulize kuna wahaya ambao walikufa na ni wazalishaji haijarishi ambao ni raia wa kawaida?
2. Kuna watoto chini ya miaka 18 ambao ni taifa LA baadae kiuchumi walikufa kutokea morogoro au mbeya? Je wa kagera wapo waliokufa?, yes Kagera walikufa,na poleni kwa msiba, lakini hao waliokufa what do they have na kudidimia kwa Kagera?!.
3. Nauliza swali lingine pasco , je kuna kiwanda kinachitoa ajira eneo husika ambacho kipo uchagani au katavi kiliharibiwa wazawa wa hapo wakakosa ajira? Hivyo hivyo Jiulize kagera VIP kuna viwanda vilivyoharibika?. Yes ni kweli kiwanda kiliharibiwa na vita na watu wakokosa ajira, lakini bado sio sababu, kama issue ni kukosa tuu ajira, Mwanaza tulikuwa na Mwatex, na gineri nyingi za pamba zimefungwa, hivyo watu wamekosa ajira!, nimekubali imechangia lakini sio sababu!.
4. Je mwaka 1978-1979 miez 12 hiyo watu wa njombe walishinda kwenye andaki bila kuzalisha? Je watu wa kagera ilikuwa hivyo?-Poleni kushinda kwenye handaki mwaka mzima bila kuzalisha, hii ni kama hoja iliyotangulia, imechangia lakini sio sababu!.
5. Je kama taifa lilitangaziwa kufunga mkanda kwa miezi 18 je hiyo adha haikuwahusu wahaya pia? Na hapa ndo makabila mengine yanasema kuwa yalipata shida je mngepata mateso kama ambavyo wahaya walipata si ndo ingekuwa mnasema ilikuwa vita ya tatu ya dunia?-Poleni sana kwa mateso lakini sio sababu!.
Tunapozungumzia maendeleo, tunazungumzia facts, usitake kutafuta sympathy hapa kuhusu Bukoba, utajiri wenu ni kahawa, bila kahawa bukoba ni masikini wa kutupwa!. Kuanguka kwa kahawa hata Kilimanjaro kahawa imeanguka, mbona kule kuna afadhali?!.
Maemdeleo ya kweli huletwa na watu, na maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu, angalieni wenzenu Wachagga wanavyothamini kwao!, jiangalieni nyinyi Wahaya tena mlivyobarikiwa kuwa na akili nyingi, robo ya wasomi wabobezi wa taifa hili ni Wahaya, huwezi amini nikienda jiji New York, nafikia nyumbani kwa mama mmoja wa Kihaya pale Mt. Vernon!, Wahaya wasomi wametapakaa duniani kote na huku mijini wana kazi nzuri, majumba mazuri, magari mazuri, wanawake wazuri, na watoto wazuri lakini nenda kwao!.
Bahati nzuri kutokana na kazi yangu ya uandishi, nimefika mahali pengi, huko kwenu ndio mnaafadhali bora hata usizungumze, charty begins at home, kama hamuwezi kujenga kwenu, msitegemee mtu aje awajengee kwenu, tena mnabahati na Kato ni mtu wenu aliyejiegesha huku kwetu, msipomtumia vizuri, itakuwa ndio basi tena kwa sababu very soon nchi hii itaanguakia kwa wenyewe na hapo sijui mtaliaje?!.
Kwa huku mijini mko well organized kwenye sherehe na misiba!, lakini kwenye maendeleo ya kwenu...!
Poleni, leta habari za Kato!.
Pasco
Sisi tuliokuwepo kuhusu suala cut off points ilikuwa hivi
Mwalimu nyerere baada ya kupandisha passmark kwa kagera , alifuatwa na wazee watatu
1.simoni rwamugila ( alikuwa UN)
2. Akafuatwa na mzee Leonard rwizandekwe,
3. Bernad Mulokozi katibu mkuu kuwa mbona mazingira haya hatuelewi??
Ndo akaamua hata Kilimanjaro apandishe passpmark kipundi hicho yanafanyika masomo mawili( hesabu na mengine yamechanganywa yote,) passmark za kagera 95/100 kwenda sekondari,
Kwa moshi kipindi kile abdunuru Suleiman akiwa mkuu wa mkoa wa arusha na baadae kilimanjaro akapewa maagizo hapo umeshapita muda wa miaka miwili kuwa wao wapandishiwe hadi 80/100,
Kule mbeya wao ilikuwa si kivile ni 70 mpaka 75, sasa we we leo unapotosha ili iweje
