Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana

Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana

Siamini kama kweli anapretend. Binafsi najua watu wana tabia hiyo ya kucjanganya vilugha na kiswahili.

Hivi Pasco hujawahi kusikia watu 2/3 katika daladala wanaongea kilugha hata huelewi wanaongea nini? Sema wahaya wamezidi kidogo(hasa wanawake) wanatabia ya kusengenya mtu ambaye si mhaya kwa kutumia Kihaya tena huyo mtu akiwa karibu nao
Naomba nisiongeze wakanishukia kuwa nawezema!, ila jamaa zetu hawa wakikutana hata mekaa meza moja mko watatu, wao wawili wataongea kilugha na wewe kuwa left out!.

Kuna event niliwahi kutambulishwa, aliyenitambulisha akasema huyu ni mtangazaji wa DTV, jamaa akauliza hiyo DTV inapatikana channel number ngapi kwenye dish ya DSTV, akaambiwa ni local channel ya Tanzania (wakati huo DTV ndio TV ya pili baada ya TVZ!, jamaa akasema kuna tv Tanzania?, hakuna tv yoyote Tanzania, ni taka taka tuu, siwezi kuangalia!, TV ni CNN, BBC, Aljazeera, lakini hapa hakuna kitu!, imagine anabonda hivyo mbele yangu!. Unafika mahali na kujikuta uko out of place!.

Pasco
 
Bukoba hatuna chuo kikubwa cha serikali, Bukoba hakuna hadhi ya kuitwa manispaa mji umechoka sana hakuna juhudi za serikali za kuuendeleza kama miji mingine
Bukoba imekuwa kisiwa Biashara imekuwa hatari sana hakuna namna ya kufanya na wenzetu
BK kama ninavoifahamu mimi kwa sasa uchumi ni wa senene tu sjui kama kuna zaojingine kwa sasa maana migomba imekufa na ugonjwa yote pole sana bora kijengwe simiyu wasafirishe ng'ombe ulaya au maziwa moja kwa moja na pamba
 
Pasco ni kweli umezungumzia madhaifu na nguvu ya makabila husika.
Lakini ukichunguza kwa makini utagundua wahaya tofauti wa makabila mengine wameacha tamaduni mbaya mapema.
Mfano hatusikii maswala ya kurithi wanawake, usafi umekuwa utamaduni wa Mhaya, hausikii Mhaya akikeketa, umekuwa ni mkoa wa mwanzo kabisa kuabandon early marriages, lakini pia pamoja na Kagera kuwa mkoa wa kwanza kuwa na maambukizi ya UKIMWI Tanzania tena katika kipindi ambacho hakukuwa na uelewa hasa juu ya ugonjwa huu ni nini, huku imani za kishirikina zikitawala kuwa watu walikuwa wakilogwa, hatuuoni mkoa wa Kagera ukiwa mkoa wenye maambukizi makubwa ya UKIMWI kama mikoa mingine pamoja na ugojwa huo kuanzia huku. Wakati huo mkoa huu ukisifiwa kwa umalaya.
Nakubaliana na wewe, ila ukeketaji no!. Wao wana keketa kwa ukeketaji wa aina yao na kule vijijini, wanaendelea nao mpaka kesho!, naomba nisiutaje ikawa ni kutoa nje siri za makabila ya watu!.

Hili la umala.. pia kiukweli sio tatizo, wazungu ndio wamefanya tulione kama tatizo, Wahaya hawana haya, hivyo kutoa sio issue kwao, wanawake wengi tuu ni waachiaji wazuri, ila wana aibu ya kuonekana, tunapokutana huko kwenye ma semina au mikutano, ndio utajua hakuna cha mke wa mtu wala cha kuelewa, wanachohitaji ni kuwa descreet, Wahaya wao hawajali hata watu wakijua so what?!.

Ni kama mila ya Wamasai watu wa rika moja kula mzigo wa yeyote wa rika lao as long as mwenye mali hayupo na sio umala..

Pasco
 
Mkuu Dr. Rweyendera, jina kubwa, title kubwa lakini uchambuzi sifuri!. Na wewe pia unaugua lile lile tatizo kuu la Wahaya, kujisikia, kujikweza na kujiona bora zaidi!.

Kwenye jibu langu la msingi, nimekiri kuwa Wahaya na Wachagga mna akili ambazo sikujua zimetokana na nini, ila nikasema zimechangiwa na uwepo wa zao kuu la biashara, zao la kahawa, hivyo wazazi wenu kuwa na uwezo wa kiuchumi wa kuwapeleka watoto wao shule!. Msijivunie hizo akili kama hamna uwezo wa kuzitumia kuleta maendeleo kwenu!.

Kwenye cut of point, mimi sikuweka viwango ila nilisema zoezi hilo, lilifanywa na Mwalimu Nyerere kwa nia njema kabisa, ili kutoa fursa sawa kwa Watanzania wote kusoma sekondari, vinginevyo shule zote zingefurika Wahaya na Wachagga, hivyp hapa unachoeleza bado mnajiona kama mlidhulumiwa kutokana na umimi kwa kujenga hoja Mwalimu aliwabagua Wahaya pekee, ila alipofuatwa Rwamu, Rwiza na Mulokozi ndipo akawaingiza Wachagga na Wanyakyusa!. Upandishaji ulifanyika kwa awamu, lazima kuwa na pakuanzia. Uzi ni kuhusu kudumaa kwa maendeleo Bukoba, tafuteni solutions msilete hadithi!.

Pasco
halafu mbona vyama vya ushirika vimesharudishwa kwa wananchi japokuwa bado vinasua au vya Kagera havijarudishwa? Mbona wenzao Wachagga wanang'ang'ana kuinusuru KNCU?
 
Kwa mawazo ya huyu muanzishaji wa thread, sishangai kwanini Kagera ipo nyuma! Tatizo linaanzia kwa wenyeji wa mkoa kudhani kila kitu serikali inapaswa kuwafanyia kwa vile kwa jinsi mhusika anavyodai inamaanisha wako bora zaidi ya wengine!
 
PASCO!

Umeanza tena tabia yako ya kuuma na kupuliza! Matatizo ya kweli yaliyo kuwa itemised na mwenzetu hakuna hata moja unalokubaliana nalo, kila item wewe ni "nyet nyet" kama Boris Yelstin Rais wa zamani wa USSR, Pasco unapenda penda sana kufurahisha baraza - unaendeleza usanii wako wa kuwasema sema vibaya Wahaya kwa kujifanya you know them better kuliko a back of your hand - maigizo tu.

Unaweza kueleza members ni Wilaya zipi za Mkoa wa Kagera uliwahi kuzitembelea - nani kakwambia Mkoa wa Kagera wakazi wake wote ni wa kabila moja tu la Kihaya f.y.i kuna Wanyambo, Wazinza, Wasubi, Waangaza na Wahaya kila Kabila lina tamaduni zao wanavyo ishi vijijini, ujenzi wa nyumba zao nk - wewe una wa-lump pamoja like salmon/Sardines in a can!! Alafu unakuja jamvini na kuwazuga watu eti unawajua vizuri Wahaya walivyo eti "wanashindwa kuendeleza kwao!"

Ebu twambie nyinyi kwenu Usukumani mnashi vipi vijini kwenu? ,je, kuna maendeleo yoyote to speak about kuanzia ujenzi wa nyumba za kuishi, maji mnayo kunywa pamoja na ng'ombe wenu, uharibifu wa mazingira - mmekata kata miti ovyo mmegeuza aridhi yenu kuwa jangwa alafu mnataka kwenda Mkoa wa Kagera wanao jua kutunza misitu ili muendeleza fyeja fyeja yenu, mnajali mifugo yenu kuliko binadamu na mazingira, nendeni kusini kwa Wamakonde mjifunze jinsi ya kujali mazingira na ujenzi wa nyumba zenye staha vijijini.

Mmekuwa kero kwa Wakulima wa Mikoa ya Mororogoro, Wilaya ya Rufiji, Katavi na Mikoa ya Kusini mnajifanyia lolote as if you own this Country kwa kuwatwanga risasi wakulima masikini wanapo lalamika mifugo yenu kula mazao yao shambani.

Pasco ebu tweleze nyinyi mmendeleza nini cha maana Usukumani i.e Wasukuma wamejenga viwanda vingapi vya maana Mwanza, shule ngapi, vyuo vya ufundi,Vyuo Vikuu- nani ambaye hajui viwanda karibu vyote vimejengwa na wageni i.e wazungu, Waarabu na Wahindi pamoja na Serikali sana sana nyinyi kama nyinyi mmefanya kitu gani cha kujivunia Mkoani kwenu mnaishia kwenye uvuvi wa dagaa, sangara na sato, kujenga guest houses na ma Bar na magari ya kubeba ya abiria, hata kivuko cha Busisi mpaka aje mzungu, je, huo ndio uwekezaji - Wahaya wana kitu gani cha kujifunza kutoka kwenu wakati mji wa Mwanza ume endelezwa na Serikali,Wageni na makabila mengine kabisa!

Pasco, soma tena para yako ya mwisho unaendeleza mipasho yako ya vijiweni wakati wewe ni msomi mwenye elimù ya Chuo Kikuu, ya nini kujiabisha mpaka ufikie hatua ya ku stoop so..., kuna haja gani ya wewe ku join band wagon ya ku-demonise WAHAYA as if Kabila hilo ni some monster kwani waliwahi kula binadamu gani dead or alive - tumechoshwa na kejeri zenu za kitoto - nyingi zakiwa ni za kizushi tu, nashauri kama baadhi ya members have nothing +ve 2 contribute ni vema wakikae kimya.

Nimalizie kwa kukupa ushauri wa bure Pasco - hili saula la kumzulia binadamu mwenzako kwamba una uhakika jina lake alisi ni Kakulu au Kato na madai mengine chungu mzima uliyo wahi kuandika jamvini siku za nyuma kumuhusu yeye - if I were you ningejirudi..
Umemwambia jambo zuri sana ambalo nimelipenda
 
Nlmsikia Rugemalira akitangaza mkakat wke wa kujenga HOSPITALI YA KISASA na kubwa zaid ya KANSA km ckosei,ataijenga apo Kagera .itahudumia Afrika Mashariki yote.cjui mkakat umeishia wap
Hiyo ni kweli rugemalila yupo kwenye mpango uo
 
Mkuu, kila nikikutana na jina lako, namkumbuka Namajeje wa Buchanagandi!.
Na wewe umeingia kwenye kundi lile lile la kuhamaki mnapoambiwa ukweli!. Kama Bukoba ni ya Wahaya, then mtu unafanya reference kwa Mhaya unayemjua na kiukweli nimebahatika kuwafahamu vizuri sana baada ya kumbahatikia dada yenu mmoja, hicho kidogo nilichoeleza ndio nimawastahi!, ningetoa ya ndani tungetafutana humu!, ila sisi wengine ni tuna wingi wa fadhila!, kwanza nimewakubali sana Wahaya kwa akili, na tangu primary niliwahi kuongoza darasa kwa somo la hesabu!, nikaja kupitwa na dada wa Kihaya!, just imagine ngosha anavyokuwa mdogo kama piriton, tangu hapo kwenye brain power, kwa Wahaya ni heshima, adabu. Ila pia kwa upande wa dada zetu, tukubali tukatae, kungekuwa na mashindano ya somo hilo, kiukweli ni mabingwa!.

Nikirudi kwetu Wasukuma, sisi ni masikini wa mali lakini matajiri wa roho!, hata waliosoma vipi, hatuchanganyi kilugha na Kisukuma kuashiria usomi, na tukija kwenye material things kiukweli nakiri tuko nyuma sana!, mtu ana ng'ombe 100!, wake 10, watoto ndio usiseme, lakini anaishi nyumba ya tope na nyasi!. Almasi babu zetu wamechezea bao!, wazungu wakatuletea gololi, tukabadilisha kwa almasi na tunafurahi!. Leo hii kanda inayoongozi kwa migodi ya dhahabu na almasi ni kwetu, angalia pato la eneo letu ulinganishe na umasikini wetu!, umasikini kwetu ndio jadi na wala hatulalamiki wala hatutatizwi na umasikini huo!, nimeridhika na umasikini wetu!.

Hili la Kato sio langu, limeletwa na mwenzio, na wewe sasa umetuongezea jina la Kakulu!, kanuni namba moja ya mwandishi wa habari kokote duniani ni "tell nothing but the truth", tukiongozwa na muongozo wa "the right to know", kuwa the public has the right to know all the truth kumhusu Kakulu Kato!, everything!. Waliondika zaidi kumhusu Nyerere ni wazungu kwa sababu nyakati hizo hatukuwa na waandishi wa kutosha!, nyakati hizi waandishi tupo, kuna haja ya kusubiri wazunge ndio waje watuandikie historia ya Kakulu Kato?!.

Pasco
Pasco umejenga heshima kubwa hapa jamiiforuns kwa kuchambua mambo mengi vizuri tu , lakin ni vizuri ungeilinda heshima hiyo kwa kuwa kimya pale unapochambua masuala ambayo huna uhakika Nayo yatashusha credibility yako , watu watakao kuwa na ujuzi au taharifa na jambo alafu ukalileta visivyo itawafanya wawe na walakini
 
Pasco ni kweli umezungumzia madhaifu na nguvu ya makabila husika.
Lakini ukichunguza kwa makini utagundua wahaya tofauti wa makabila mengine wameacha tamaduni mbaya mapema.
Mfano hatusikii maswala ya kurithi wanawake, usafi umekuwa utamaduni wa Mhaya, hausikii Mhaya akikeketa, umekuwa ni mkoa wa mwanzo kabisa kuabandon early marriages, lakini pia pamoja na Kagera kuwa mkoa wa kwanza kuwa na maambukizi ya UKIMWI Tanzania tena katika kipindi ambacho hakukuwa na uelewa hasa juu ya ugonjwa huu ni nini, huku imani za kishirikina zikitawala kuwa watu walikuwa wakilogwa, hatuuoni mkoa wa Kagera ukiwa mkoa wenye maambukizi makubwa ya UKIMWI kama mikoa mingine pamoja na ugojwa huo kuanzia huku. Wakati huo mkoa huu ukisifiwa kwa umalaya.
Hiyo umeongea point kubwa , lakin vipi omukajunguti inajengwa au ilikuwa kuzuga tu?
 
  • Thanks
Reactions: Izc
Kauli za hovyo hovyo kama hizi zilizo kaakaa ki UKUTA UKUTA hazina tija.Mbona hukuwahi kuandika kulaani operation hovyo ya ukuta?.
Haya mambo yakujenga hoja kikabilakabila sijui kwanini wahaya mnayapenda sana?
Hii ni ishara kwamba lile linalosemwa kwamba ninyi ni wakabila ni lakweli.
Raisi yupo mbioni kununua meli kubwa lake victoria ili itoe huduma huko kwenu,mbona hujalalamika kwamba amewapendelea akawaacha wengine?
Hemu mwacheni raisi afanye kazi
ndugu usikimbilie ukabila we soma hoja tambua amemaanisha nn ndo utoe utatuz usiwe kama mgema
 
Naomba nisiongeze wakanishukia kuwa nawezema!, ila jamaa zetu hawa wakikutana hata mekaa meza moja mko watatu, wao wawili wataongea kilugha na wewe kuwa left out!.

Kuna event niliwahi kutambulishwa, aliyenitambulisha akasema huyu ni mtangazaji wa DTV, jamaa akauliza hiyo DTV inapatikana channel number ngapi kwenye dish ya DSTV, akaambiwa ni local channel ya Tanzania (wakati huo DTV ndio TV ya pili baada ya TVZ!, jamaa akasema kuna tv Tanzania?, hakuna tv yoyote Tanzania, ni taka taka tuu, siwezi kuangalia!, TV ni CNN, BBC, Aljazeera, lakini hapa hakuna kitu!, imagine anabonda hivyo mbele yangu!. Unafika mahali na kujikuta uko out of place!.

Pasco
Jamaa hakuwa sawa ila kwa upande wa pili alikuwa sawa kabisa ebu jitafakari na kujifikiri zaidi weka mbali njaa yako. Fikiri out of the box.
 
Unachosema ni kweli hatutaki viongozi wa kitaifa tunataka maendeleo
Kwa nyongeza ya hapo Mwl. Nyerere amekuwa kiongozi wa Taifa hili miaka mingi lakini hakuikumbuka Mara, hivyo uongozi wa kitaifa sio tija kwa maendeleo ya sehemu fulani. Tuwe wazalendo tuipende Tanzania yetu, tuiendeleze kwa pamoja. Vipaumbele vya kitaifa vifanyiwe kazi kwanza.
 
Back
Top Bottom