Alexism
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 3,423
- 2,046
Tena tumepigwa hasara kubwa mtu asikuambieHako ka tawi wamekafuta
Tena tumepigwa hasara kubwa mtu asikuambieHako ka tawi wamekafuta
Ata mimi ilibidi nijiite jina la kabila la watu wa Kigoma aiseeLakin serikali inawachinjia mbali mpaka tumanza kujiita majina yasiyo ya kihaya
Apo umenena sanaMkuu umeongea jambo la msingi sana sana ila umeharibu sana kitu kimoja, kuutaja mkoa wa Kagera. Ukiutaja mkoa huu utashambuliwa na hata yule asiye na meno. Yawezekana tulipata bahati mbaya kuwa watanzania, naamini huu mkoa ungekuwa Uganda ingekuwa ni jambo jema zaidi kuliko ilivyo leo, ubaguzi ni mkubwa sana hapa Tz dhidi ya mkoa huu.i
Kama ni Umuhimu wa Airports basi kwanza tungejenga Viwanja vya Kila Mkoa . Tungehakikisha Mikoa Yote in viwanja vya kimataifa au bora all weather.
bado kuna mikoa haina viwanja vya uhakika,
na hili ndio lengo la serikali zote zilizopita. wamekua wakijenga viwanja vipya katika mikoa .
Chato hakuna sababu wala umuhimu labda kama cm wameamua kumjengea mkuu uwanja wa kutua akienda christmas
Waliotekekeza Kagera ni wana Kagera wenyewe.Watu wa Kagera popote wanapokuwa ndio kwake kafika hana mpango wa kagera wala nini kama wachaga.Kagera wanaenda tu sana sana labda mtu akifariki wanaenda kuzika au kuhani msiba! Kagera kuna wasomi na wenye pesa wamezagaa dunia nzima lakini hawana makazi ya kudumu bukoba na hawana mpango wa kuhamia kukaa kule au kufanya uwekezaji mkubwa kule.
Kila mtu wa kagera anayefanikiwa SANA anachofanya ni kutimukia DAR ES SALAAM ,MIKOA MINGINE.Marekani ,ULAYA NK
Kagera kulitakiwa kuwe na vyuo vikuu kibao.Maprofesa wastaafu wako weengi mno kule wangeanzisha mavyuo kibao walimu wakawa wenyewe na washomile wengine ambao wako every where in the world including UNITED NATIONS and other important UN agencies and ICC.
Kwa watu wa kagera kusubiri serikali ifanye mambo makubwa ni too low na ni aibu.
Tutalazimishwa kuongea kihaya nchi nzimaToeni rais na nyie mpate advantages
Miez 6Hivi mwili wa binadamu hujukuwa mda gani decay?
KabisaKutesa kwa zamu tehe mbona maofisini wamejaa wahaya hatusemi?
Mpango wa omukajunguti ni wa Siku nyingi
Je, mnatambua kuwa serikali imeshiriki katika kuudumaza mkoa kagera?
Hivi ndivyo mkoa kagera umeachwa yatima na serikali ya Tanzania,
Tulivyopata Uhuru kagera ilikuwa miongoni mwa mikoa mitatu yenye uchumi imara,
1. Dar es salaam
2. Kagera
3. Kilimanjaro
Lakin ukweli usiopingika Kagera imetelekezwa na serikali vya kutosha bila kujali majanga yaliyoikuta au michango ambayo Kagera imetoa kwa watanzania.
Kila MTU kutokea Kagera atakuwa ana kumbukumbu zinazomfanya kusononeka sana,
SABABU MUHIMU ZILIZOSABABISHA KAGERA KURUDI NYUMA KIMAENDELEO
1. VITA YA KAGERA, 1978/79
Vita ya nchi nzima ilipiganwa kwenye mkoa mmoja na kuharibu miundombinu vya kutosha , na ule ndo ulikuwa uwanja wa vita hasa, lakini hakuna sehemu yoyote kuna strategy za kuujenga upya mkoa, tunaishia kusikia maneno ya kashfa tu tena toka kwa viongozi wakubwa kwa wanakagera eti mmeshindwa kujenga hata chuo kikuu kimoja? Aliuliza Kikwete lakini kasahau kuwa yeye kama mkuu wa serikali hajajenga hata chuo cha kutoa cheti.
2. JANGA LA UKIMWI 1983,
Kama inavyojulikana Kagera iko mpakani mwa Uganda, na UKIMWI umeanzia Uganda, na kwa kuwa wana Kagera wana utaratibu wa kufanya Biashara na Uganda , haikukwepeka kupata UKIMWI, nguvu Kazi kubwa ilipotea sana miaka hiyo na kusababisha uchumi kurudi nyuma,
3. AJALI YA MV BUKOBA
Janga la pili ambalo linafanya kudhoofisha mkoa wa Kagera ni kuwa , watoto wengi yatima wameongezeka , nguvu kazi imepungua kutokana na ajali ile.
4.1998 EL NINO
Hii wengi mnaelewa kuwa imekumba sana ukanda wa kanda ya ziwa kuliko kanda yoyote ile hapa nchini , imeharibu miundombinu na kupoteza wazalishaji Mali,
5. KUSHUKA KWA BEI YA KAHAWA 1998 KWA UZEMBE WA SERIKALI.
Inajulikana Kagera ilitegemea sana Kahawa kama kitega uchumi , kwa uzembe wa serikali hakukuwepo utaratibu wa kuhakikisha Kahawa inabaki na bei ya kuridhisha badala yake ikapuuza mpaka wananchi wakakata mibuni maana haikuwa na maana tena,
6. UBAGUZI ULIOJIFICHA TOKA KWA VIONGOZI ( INDIRECT DISCRIMINATION TOWARDS HAYA TRIBE)
Miaka ya nyuma hakuna ambaye hajui kuwa wahaya waliwekewa mizengwe katika baadhi ya sekta, hata kwenye elimu , walipandishiwa alama za ufaulu ili wachache waendelee na elimu ya juu maana walionekana kuwa wao ndio wanafaulu na kujaza madarasa mengine, lakin ili kuitamka sentensi hii (INAHITAJI UJIFANYE MWENDA WAZIMU KIDOGO)
7. KUTENGWA NA NCHI KIJIOGRAFIA
Kagera iko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, waliowahi kufika uko ndio wanaelewa namaanisha nini, Kagera imekuwa kama kisiwa maana jinsi ya kufika kule inabidi ukatishe kilometer kadhaa za msitu, ili uingie Kagera, au upite ziwani kwa meli ndio uende mikoa mingineyo ambayo ni ya Tanzania, hivyo basi wana Kagera walikuwa na urahisi wa kufanya Biashara na Uganda kuliko mikoa mingine ya Tanzania, lakini serikali ilikataza biashara hiyo , wakajikuta wamebaki kama kisiwa ndani ya nchi yao wenyewe,
8.KAGERA KIMBILIO LA WAKIMBIZI MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA 1994 NA MACHAFUKO TANAYOENDELEA UKANDA ULE.
Wanyarwanda wameiteka Kagera hasa wilaya ya Karagwe na Muleba na kujichukulia ardhi , pia wamekuwa watekaji wa magari na kudhalilisha wana kagera , kitu amabacho kimerudisha nyuma uchumi wa mkoa, kwa kasi, majambazi wametamalaki na kufanya uharamia ambao umefanya kusiwepo hali ya utulivu na kujenga uchumi, serikali imechelewa kuchukua hatua,
9. KUTOJUMUISHWA KATIKA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO KIKANDA
Kila kanda imetengwa katika kanda fulani ya mkakati wa maendeleo lakini kanda ya ziwa ambayo ndipo kuna mkoa Kagera hakuna ilipoainishwa katika mpango wa maendeleo.Kagera Umekuwa ni mkoa wa kujitegemea kwa kila kitu utasikia
Ukumbi wa mkutano unajengwa Arusha, sijui chuo cha utalii Dar, chuo cha ufugaji Tabora.
Chuo cha reli tabora, chuo cha science cha nelson Mandela arusha,
Chuo cha serikali cha ugavi, Chuo cha ushirika Moshi Mara..
Chuo cha mbao Iringa, kwanini Kagera hakuna mipango endelevu, sasa upo wapi uwanja wa Mukajunguti wa ndege na ulishaahidiwa kuwa wa kimataifa na kutengewa bajeti kipindi cha Mkapa?,Rais Magufuli halioni hilo?
Kagera wanekuwa wa kupandia kama daraja, Kikwete kaenda Bukoba katoa ahadi ambayo imerudiwa na Magufuli sana, eti ntawapa meli ,mbona hata mtumbwi haujaweka,
We unayesoma hapa nitajie chuo chochote kilichojengwa na serikali kuazia cheti mpaka degree, imekuwa vipaumbele kujenga Dodoma na mnasahau kuna deni Kagera inadai kwa taifa hili.
Kilichosaidia Kagera ni vishirika vya wazungu tu kama partage, world vision, gses, yaan serikali haijatenda haki huko.
SOMA HII SASA SERIKALI INA KITU KINAITWA SUBJECTIVE AND OBJECTIVE PLANNINGS,(BIG FOUR REGIONS) IKO HIVI
1.KANDA YA KUSINI AU NYANDA ZA JUU KUSINI
Imetengwa kama kanda ya kilimo hapa kuna mikoa
Njombe
Mbeya
Katavi
Ruvuma
Na Iringa .
2.KANDA NYINGINE KANDA YA KASKAZINI
Hii imeahinishwa na kupewa kipaumbele kama kanda ya utalii,
Mikoa ni
Arusha,
Kilimanjaro na Manyara,
3.NYINGINE NI KANDA YA KATI ,
Taasisi za siasa na Elimu ya juu
Mikoa ni
Morogoro,
Dodoma,
Singida,
4. KANDA YA MASHARIKI INEPEWA Kanda ya viwanda na Biashara, mikoa ni
Dar es salaam,
Mtwara
Lindi
Pwani
Tanga
KANDA YA ZIWA ANBAYO KUNA KAGERA IKO WAPI, ?
Sasa inafika hatua tunapaswa kuusema ukweli ,
Mheshimiwa rais huu ulikuwa ninwakati wa Kujenga MUKAJUNGUTI INTERNATIONAL AIRPORT SIYO CHATO. TUNGEPOZWA ANGALAU NA UWANJA UO MAANA TUMESUBIRI NEEMA KWA MIAKA MINGI LAKIN WAPI
Wengi watasema umejenga huko kwakuwa ni kwenu, lakini pia hata KAGERA KARAGWE NI KWENU KWA MZEE MACHALILA, NA JINA LAKO LA KIHAYA NI KATO (wengi hawajui hii), sasa kama ndo sababu ya kujenga nyumbani anza nyumbani ambapo pako kwenye mipango ya Siku nyingi,
Kajunguti International Airport - Wikipedia, the free encyclopedia
Britannica
Mkuu britanicca , they are competent, ila ajali ni ajali, ila kama huu uwanja wa Omukajunguti ungejengwa, labda haya yasingetokea!.Mara nyingi siwaamini marubani Waswahili hawa Watanzania.
Uwa na nikipanda za Tanzania nfano kutoka DSM to Bukoba, nikasikia Welcome on board,This is Captain LUSUNGU talking, au Captain BYAMUNGU, huwa naishiwa nguvu siwaamini kabisa.
View attachment 1279332
Je, hawa ma-captiain wako competent vya kutosha?
Mkuu britanicca , they are competent, ila ajali ni ajali, ila kama huu uwanja wa Omukajunguti ungejengwa, labda haya yasingetokea!.
Poleni kwa ajali ya ndege Bukoba!. Bukoba sijui vipi?, Tangu Vita vya Kagera, ndio vita iliyoua watu wengi Tanzania kuliko vita nyingine yoyote nchini Tanzania. Ukaja ugonjwa wa Ukimwi, ukiitwa Juliana, Bukoba ndio the most hit kabla ya kusambaa kungine kote!. Ikaja ajali ya MV Bukoba ni Bukoba, hii ndio ajali kubwa ya meli iliyouwa watu wengi kuliko ajali nyingine yoyote ya meli Tanzania!. Likaja Tetemeko la Ardhi Bukoba, ndilo tetemeko kubwa kuliko matetemeko yote Tanzania, na sasa hii ajali ya ndege ya Precision Air Bukoba, ndio ajali kubwa ya ndege iliyo ua watu wengi kuliko ajali zote za ndege nchini Tanzania, imetokea ni Bukoba!.
Pamoja na majanga haya, pia kuna mambo mazuri ya Bukoba. Ingefanywa sensa ya wasomi wa kiwango cha Ph.D unaweza kukuta watu wa Bukoba ndio wanao ongoza kwa idadi ya Ph.D na ma profesa,
Chakula kinachoongoza kwa protein ni senene akifuatiwa na kumbikumbi wanapatikana Kagera.
Kuna fani fulani ambayo Baganda women wanaongoza bara la Africa, baada ya Baganda wa pili ni Bahaya!.
Pia kwenye tiba asili Bukoba wanaongoza kwa most effective tiba asili wakifuatiwa na Wamasai na pia Bukoba ndio wanao ongoza kwa utaalamu wa mambo fulani, hivyo vitu kama shuntama na limbwata is real na sii mchezo bila kusahau kile kijiji cha ile siku ya Gulio ya kwenye kitabu cha Kiswahili Darasa la 4 la zamani!.
Poleni sana ndugu zetu wa Bukoba.
P
Siku ya gulio Katerero...[emoji16]...we mzee acha uhuni!Mkuu britanicca , they are competent, ila ajali ni ajali, ila kama huu uwanja wa Omukajunguti ungejengwa, labda haya yasingetokea!.
Poleni kwa ajali ya ndege Bukoba!. Bukoba sijui vipi?, Tangu Vita vya Kagera, ndio vita iliyoua watu wengi Tanzania kuliko vita nyingine yoyote nchini Tanzania. Ukaja ugonjwa wa Ukimwi, ukiitwa Juliana, Bukoba ndio the most hit kabla ya kusambaa kungine kote!. Ikaja ajali ya MV Bukoba ni Bukoba, hii ndio ajali kubwa ya meli iliyouwa watu wengi kuliko ajali nyingine yoyote ya meli Tanzania!. Likaja Tetemeko la Ardhi Bukoba, ndilo tetemeko kubwa kuliko matetemeko yote Tanzania, na sasa hii ajali ya ndege ya Precision Air Bukoba, ndio ajali kubwa ya ndege iliyo ua watu wengi kuliko ajali zote za ndege nchini Tanzania, imetokea ni Bukoba!.
Pamoja na majanga haya, pia kuna mambo mazuri ya Bukoba. Ingefanywa sensa ya wasomi wa kiwango cha Ph.D unaweza kukuta watu wa Bukoba ndio wanao ongoza kwa idadi ya Ph.D na ma profesa,
Chakula kinachoongoza kwa protein ni senene akifuatiwa na kumbikumbi wanapatikana Kagera.
Kuna fani fulani ambayo Baganda women wanaongoza bara la Africa, baada ya Baganda wa pili ni Bahaya!.
Pia kwenye tiba asili Bukoba wanaongoza kwa most effective tiba asili wakifuatiwa na Wamasai na pia Bukoba ndio wanao ongoza kwa utaalamu wa mambo fulani, hivyo vitu kama shuntama na limbwata is real na sii mchezo bila kusahau kile kijiji cha ile siku ya Gulio ya kwenye kitabu cha Kiswahili Darasa la 4 la zamani!.
Poleni sana ndugu zetu wa Bukoba.
P
Mkuu Bukyanagandi , naomba kwanza ku declare ya interest, mimi ni rafiki na mtu aitwae Namajeje wa Bukyagandi, pili, this is from the bottom of my heart, kiukweli kabisa nawependa sana sana Wahaya. Ila lazima niukubali udhaifu wangu, mimi ni mkweli tuu much!. Chochote ninachosema kuhusu Wahaya ni ukweli mtupu uwe ni ukweli mzuri au ukweli usiopendeza, na pia nikiri udhaifu mimi ni mpenzi wa kale kamchezo na kuikweli kwenye yale... Mhaya hana mpinzani wala mshindani!. Hadi niliwahi kuuliza Anatomical Question on Squirting: Why Only Some and Why So Much Fluid!.Mayalla,binafsi huwa sipendi tabia yako ya kukejeri kabila la Wahaya indirectly - please revisit comments zako za miaka ya nyuma linapo kuja suala la Wahaya - unaonekana wazi wazi anakuwa driven na rabid hatred ya Wahaya lakini you so crafy kiasa cha kwamba mtu akisoma comments zako kijuu juu mtu anaweza kuhadaika kirahisi na kufikiri labda unazungumza mambo ya kawaida, kumbe hiyo si kweli hata kidogo.
Yes yes chambua tuu!, hata mimi mwenyewe japo ni Msukuma tunajikubali japo sisi ni wachapakazi sana bali pia ni washamba sana!, japo ndilo kabila ambalo wanaume wetu wanaongoza kwa kupenda na kuhonga kwasababu sio wabahili, tatizo letu wengi ni kupenda wengi!. Kwenye ukabila kuna ukabila mzuri na ukabila mbaya. Ukabila mzuri ni kuyaeleza mazuri ya kabila fulani ili wengine waige, na ukabila mbaya ni ule ukabila wa upendeleo uitwao nepotism, Wasukuma sio wakabila wabaya wa nepotism Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi! sasa kwa vile JPM alituhumiwa kwa ukabila mbaya, nikashauri Wito kwa Bunge letu tukufu: Mkithibisha hii Nepotism ya ajabu na zile Boeing ni TT, then hatufai!.Sasa swali,je,na sisi tukihamua kuchambua kabila lako la Wasukuma unafikiri hapa patakalika??
Asante hili nimelipokea, na kiukweli niko obsessed na wadada zenu, kwasababu the first impression last longer!, mimi ni mtoto wa Driven Flats hivyo nipoingia kwenye ujana, my first experience ya mambo yale ni kuingia Msasani Mikoroshoni kwenye vile vibanda vya udongo na koroboi, hivyo ni kweli I love them na wametusaidia sana!.Bottom line is: Tanzania tuko huru ku-comment chochote members wakakuelewa lakini unapo fikia hatua ya kukejeri makabila fulani latently hii haileti picha nzuri hata kidogo, kwa nini unakuwaga overly obssesed ma wenyeji wa Kagera specifically HAYAS - nimeona hili niliweke wazi kwa kuwa umezoea sana kujifanya unawasifia Wahaya lakini humo humo unatumbukiza kejeri na dharau unafikiri people are so naive hawana uwezo wa ku-read between the line na ku-unmask your true colour, wewe ni mwana sheria unajua vizuri ninacho maanisha, hacha kabisa tabia zako za kuuma na pululiza. I hope this serves you right,safari nyingine utajaribu kuwa makini kidogo na comments zako. CHEERS ALL THE SAME.
DahToeni rais na nyie mpate advantages
MhUkichukua Rugemarila family na Kyaruzi family unapata nusu ya utajiri wa nchi hii waulize kwanini hawawekezi kwao?